Katika nyayo za Kiagostino,Papa Leone XIV kwa kimya na sala katika mabaki ya Hippo
Tiziana Campisi–Mwakilishi Annaba na Angella Rwezaula–Vatican.
Mvua kubwa ilinyesha Annaba; ikawa siku ya kijivu. Lakini miongoni mwa magofu ya Hippo ya kale, yaliyopita na ya sasa yalionekana kuungana. Enzi mbili tofauti, zilizotenganishwa zaidi ya karne kumi na sita, lakini ambazo ujumbe huo huo unafikia ulimwengu, kutoka kwa Mtakatifu Agostino na Papa Leo XIV: tunaweza kuishi kama ndugu tukijenga amani pamoja. Ni siku ya pili ya Ziara yake ya kitume ya Papa kuwa barani Afrika, moja ya siku zinazotarajiwa sana.
Papa wa kiagostino, kupitia mvua iliyoonyesha, alitembea sehemu fupi ya eneo la akiolojia, sehemu ya barabara inayopitiwa mara nyingi na Askofu Aurelius Augustinus, mzaliwa wa Thagaste, sasa Souk Ahras, na Askofu wa jiji la bandari linalostawi. Kwa kupanua mtazamo wa macho, mtu anakumbatia kilima cha Annaba na Kanisa kuu au Basilika ya Baba wa Kanisa. Kwa hiyo jana na leo, na Papa wa kwanza katika ardhi ya Algeria anayemheshimu Baba yake wa kiroho, na kukusanya urithi wake na kutoa sauti tena kwa mwaliko wake wa kuishi kwa amani, ili kuwe na amani miongoni mwa watu. Kwa sababu, kama laivyo sisitiza "amani ndiyo mwisho wa mema yetu," aliandika Agostino katika "Mji wa Mungu," katika sura ya XIX (11), ambapo anarudia neno "amani" zaidi ya mara mia moja.
Miongoni mwa magofu ya jiji ambalo Agostino aliishi
Akisalimiwa kwenye mlango wa uchimbaji na Afisa wa eneo hilo, Papa Leo XIV alibanisha akiguswa sana, magofu ya Hippo Regius, yaliyokaliwa hadi karne ya 5 na wavuvi, mabaharia, Askari, wafanyabiashara, mafundi, maafisa, na wakulima, pamoja na familia tajiri, wamiliki wa meli.
Hali mbaya ya hewa ililazimisha sherehe iwe fupi, ambapo Papa Leo XIV, chini ya Tenti, kwa msaada wa Skauti wawili wachanga, aliweka shada la waridi nyeupe na njano na kisha akapanda mzeituni, ishara ya amani na inayokumbusha mti wa mzeituni wa karne nyingi katika mji wake wa nyumbani, ambao mila na tamaduni inashikilia tangu wakati wake.
Baba Mtakatifu Leo XIV alibaki amezama katika maombi kwa muda mfupi, mikono yake ikiwa imeshikamana. Wakati huo huo, njiwa weupe waliachiliwa kwenye anga lenye , lililojaa mvua, huku kwaya ya Taasisi ya Muziki ya Annaba ikiimba nyimbo kwa Kilatini, Berber, na Algeria, huku maandishi ya Askofu wa Hippo kuhusu amani na udugu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
