2026.04.13 Ziara ya Kitume chini Algeria: Kutembelea Mnara wa Kumbukumbu ya Mashahidi -Maqam Echahid. 2026.04.13 Ziara ya Kitume chini Algeria: Kutembelea Mnara wa Kumbukumbu ya Mashahidi -Maqam Echahid.  (@Vatican Media) Tahariri

Mrithi wa Petro arudi Afrika kama mmisionari wa amani

Mhariri wetu Mkuu wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano alitafakari maneno ya kwanza ya Papa Leo XIV baada ya kutua katika ardhi ya Algeria,ambapo alitoa wito wa msamaha wa pande zote kama ufunguo wa kujenga mustakabali.

Andrea Tornielli

Mrithi wa Petro amerudi Afrika. Miaka mitatu baada ya ziara iliyofanywa mwanzoni mwa 2023 na Papa Francisko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini, Papa Leo XIV ameanza hija ndefu katika bara la Afrika, alianza ziara yake Jumatatu Aprili 13 nchini Algeria na katika siku zijazo nchini Cameroon, Angola, na Guinea ya Ikweta. Ni ziara ya siku 11 ya kimisionari, iliyooneshwa na ratiba kali ya kukutana na watu wa bara ambalo limedhoofishwa na matatizo na migongano, lakini pia ni hifadhi ya furaha na matumaini. Haiwezekani kusahaulika kwamba,"ni wakati wa kihistoria" ambapo ziara hii inafanyika, huku kukiwa na wasiwasi unaoongezeka kuhusu kinachoendelea Mashariki ya Kati na tishio la kuongezeka kwa migogoro kufuatia kushindwa kwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran.

Papa katika Mnara wa Kumbu Kumbu ya mashahidi wa Algeria
Papa katika Mnara wa Kumbu Kumbu ya mashahidi wa Algeria   (@Vatican Media)

Kwa hivyo ilikuwa muhimu kwamba amani iliibuka kama mada kuu katika hotuba ya kwanza ya Papa Leo XIV nchini Algeria, wakati wa ziara yake kwenye Mnara wa Ukumbusho wa Mashahidi (Maqam Echahid): "Katika mahali hapa, tukumbuke kwamba Mungu anataka amani kwa kila taifa: amani ambayo si tu kutokuwa na migogoro, bali kuonesha haki na utu. Amani hii, ambayo inaturuhusu kukabiliana na mustakabali kwa roho ya upatanisho, inawezekana kupitia msamaha tu. Mapambano ya kweli ya ukombozi yatapatikana tu wakati amani mioyoni mwetu itapatikana."

Wito wa msamaha na amani ya moyo umejaa uhalisia wa kina. Sio tu kwamba ni cha ujumbe wa Kikristo, bali pia unawakilisha njia pekee inayofaa ya kujenga mustakabali. "Ninajua jinsi ilivyo vigumu kusamehe," Papa alisema. "Hata hivyo, kadri migogoro inavyoendelea kuongezeka  ulimwenguni kote, hatuwezi kuongeza chuki juu ya chuki, kizazi baada ya kizazi." Mtu anawezaje kushindwa kutafakari kuhusu chuki inayotokana miongoni mwa vizazi vichanga kutokana na mauaji ya raia huko Gaza na sasa Lebanon? Na swali hilo hilo linawezaje kutoulizwa kuhusu vita nchini Ukraine na maeneo mengine mengi yaliyoathiriwa na chuki na vurugu?

Hata kama viongozi wengi wanaamini kwamba njia ya kusonga mbele ya matukio kama hayo iko katika kupanga matumizi ya silaha, kunaufaika kwa wafanyabiashara wa kifo , Papa Leo XIV, akizungumza kutoka Algiers, alitukumbusha kwamba: “Mustakabali ni wa wanaume na wanawake wa amani,” na kwamba “haki itashinda dhuluma kila wakati, kama vile vurugu, licha ya kuonekana kwa kila kitu, hazitawahi kuwa na neno la mwisho.” Sauti ya amani ya Mrithi wa Petro, Mwakilishi wa Mwana wa Mungu wa wasio na ulinzi aliyechagua njia isiyo na vurugu ya kujitolea Msalabani, inasikika kwa nguvu zaidi inapoinuka kutoka nchi hii, ambapo Kanisa ni la waamini wachache kabisa na ambapo ushuhuda wa Wakristo wachache sana ni muhimu zaidi, uliojengwa katika huduma na katika kushirikisha furaha na mateso ya wote.

Papa akiwa katika Mnara wa Kumbu Kumbu ya mashahidi wa Algeria
Papa akiwa katika Mnara wa Kumbu Kumbu ya mashahidi wa Algeria   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

13 Aprili 2026, 16:23