Papa,atoa wito kwa Trump na vongozi wa Ulimwengu:tafuteni suluhisho kumaliza vita!

Papa Leo XIV akiwa huko Castel Gandolfo Machi 31,alirudia kutoa wito wake wa amani duniani na kutumaini kuwepo kwa amani kwa ajili ya Pasaka:Papa alisema hayo kwa waandishi wa habari nje ya Villa Barberini na kuwaalika viongozi wote wa dunia kuwa:“Ni wakati Mtakatifu zaidi kurudi mezani kwa mazungumzo na kutafuta suluhisho ili kupunguza vurugu."

Vatican News

"Nimeambiwa kwamba Rais Trump hivi karibuni alisema anataka kukomesha vita. Tunatumaini anatafuta njia ya kutoka, tunatumaini anatafuta njia ya kupunguza vurugu, na mabomu. Itakuwa mchango mkubwa katika kuondoa chuki inayoundwa, ambayo inaongezeka kila mara Mashariki ya Kati na kwingineko." Siku chache kabla ya Pasaka, Papa Leo XIV alirudia akiwa  Castel Gandolfo wito wa amani kwa ulimwengu uliojeruhiwa na migogoro na vurugu. Katika taarifa iliyotolewa usiku wa Jumanne tarehe 31 Machi 2026, kwa waandishi wa habari nje ya Villa Barberini, Papa aliwaelekea viongozi wote wa dunia, akiwasihi: "Rudini mezani kwa mazungumzo, tutafute suluhisho la matatizo, tutafute njia za kupunguza vurugu tunazochochea. Na amani, hasa wakati wa Pasaka, iwe mioyoni mwetu."

Pasaka, wakati wa amani

Pasaka yenyewe Papa alisisitiza alikumbushwa kwamba "inapaswa kuwa wakati Mtakatifu zaidi na Mtakatifu zaidi kwa mwaka mzima. Ni wakati wa amani, wakati wa kutafakari sana, lakini kama tunavyojua sote, tena duniani, katika sehemu nyingi, tunaona mateso mengi, vifo vingi, hata watoto wasio na hatia." Papa aliendelea: "Tunaendelea kuomba amani, lakini kwa bahati mbaya, watu wengi wanataka kukuza chuki na vurugu, vita. Kwa hivyo ninawaomba kila mtu, hasa ​​Wakristo, kuishi siku hizi, wakitambua kwamba Kristo bado amesulubiwa leo. Kristo bado anateseka leo,  kwa wasio na hatia, hasa wale wanaoteseka kutokana na vurugu, chuki, na vita." Kwa njia iyo "Tuwaombee, kwa ajili ya waathiriwa wa vita, tuombe kwamba kweli kuwe na amani mpya, iliyofanywa upya, ambayo inaweza kutoa uhai mpya kwa wote.” Papa Leo XIV alihimiza hayo kwa waandishi wa habari, huku akionesha, “matumaini yake kwamba Pasaka inaweza kuleta amani kutokana na migogoro.”

Msalaba wa Njia ya Msalaba

Papa pia aliulizwa kuhusu uamuzi uliotangazwa Machi 31, kwamba Yeye mwenyewe atabeba Msalaba wakati wa Vituo 14 vya njia ya Msalaba siku ya Ijumaa Kuu, kando ya Gofu la Kale ( Colosseum.) Kwa kujibu alisema: “Nadhani kwamba itakuwa ishara muhimu kwa sababu ya kile ambacho  Papa anawakilisha: kiongozi wa kiroho duniani leo, ni sauti hii ya kusema kwamba Kristo bado anateseka” Papa aliongeza : “Na mimi pia, ninabeba mateso haya yote katika maombi yangu." Kuanzia hapo, aliwasihi zaidi "watu wote wenye mapenzi mema, watu wa imani, watembee pamoja, watembee na Kristo aliyeteseka kwa ajili yetu, atupe wokovu, na kutafuta kuwa wabebaji wa amani."


Safari ya Kuelekea Hispania

Kabla ya kusalimia kundi kubwa la watu waliokusanyika barabarani nje ya Villa Barberini, akiwemo meya wa Albano, Papa pia aliulizwa anachotarajia kwa safari yake kwenda Hispania iliyopangwa kufanyika mwezi Juni ujao: "Imani, upendo mwingi, ukarimu, na ukaribisho wa joto." Papa aliongeza: "Nimekuwa nikitembelea Hispania kwa zaidi ya miaka 40 na siku zote nimekutana watu wenye imani kubwa na mapenzi mema," ana hivyo Papa anatumaini "kwamba tunaweza kusherehekea haya yote wakati wa ziara hii pia."

MAHOJIANO PAPA KWA WAANDISHI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

01 Aprili 2026, 10:26