2026.04.14 Papa atembelea Kituo cha Dada wadogo cha kutunzia wazee. 2026.04.14 Papa atembelea Kituo cha Dada wadogo cha kutunzia wazee.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV katika kituo cha wazee Annaba:Moyo wa Mungu uko pamoja na maskini,si kwa wenye kiburi

"Moyo wa Baba Yetu haupo na waovu,na wenye vitisho na wenye viburi:Moyo wa Baba huko na walio wanadogo na wanyenyekevu na wanaopeleka mbele ufalme wake wa upendo na wa amani,siku kwa siku.Kama mnavyofanya hapa katika huduma ya kila siku katika upendo na kuishi pamoja."Alisema hayo Papa Leo XIV katika Mkutano kwenye Nyumba ya wazee huko Annaba,inayohudumiwa na Dada Wadogo wa Maskini,Aprili 14,2026,ikiwa ni siku yake ya Pili akiwa huko Algeria.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa huko Annaba alitembelea Kituo cha kutunzia wazee cha ‘Ma Maison,’ Jumanne tarehe 14 Aprili 2026. Akianza salamu zake aliwasalimia habari za asbubuhi  hata kwa ‘As-salamu alaykom!’ Papa aliwashukuru kwa kumkaribisha katika nyumba hiyo. Alionesha furaha “kwa sababu anaishi Mungu, kwani mahali palipo na upendo na huduma hapo kuna Mungu.” Baba Mtakatifu aliwashukuru Watawa, Dada Wadogo wa Masikini pamoja  na wafanyakazi wa Nyumba hiyo. Alimshukuru Mama Filomena “kwa maneno yake ya kumpatia makaribisho.”

Papa na wazee
Papa na wazee   (@Vatican Media)

Baba wa Mbingu na dunia anayewaficha wenye hekima na akili akawafunulia watoto

Baba Mtakatifu Leo XIV aidha alimshukuru Askofu kwa maneno yake ya kugusa! Papa aliongeza kwamba “kwa kumsikiliza na kuona uwepo wa hapa  kati ya kaka na dada wazee, inakuja hivyo haraka kusifu Mungu na kumshukuru.” Kama Yesu alivyofanya siku moja, ambayo alijazwa na Roho Mtakatifu na kusema: “Nakushukuru, Baba, Bwana wa Mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza”(Lk 10,21).

Papa alikwenda kutuo cha kutunzia wazee
Papa alikwenda kutuo cha kutunzia wazee   (@Vatican Media)

Moyo wa Mungu umejaribiwa na vita,vurugu,ukosefu wa haki na uongo

Papa alimshukuru Bwana Salah Bouchemel kwa ushuhuda wake namna hiyo nzuri na ya kufariji. Papa alifikiria kuwa “Bwana kutoka Mbinguni, kwa kuona nyumba kama hiyo, mahali ambapo wanatafuta kusali pamoja katika udugu, inawezekana kusema kwamba ‘kuna tumaini’.” “Ndiyo kwa sababu Moyo wa Mungu umejaribiwa na vita, vurugu, ukosefu wa haki na uongo. Lakini moyo wa Baba Yetu haupo na waovu, na wenye vitisho na wenye viburi: Moyo wa Mungu uko na wadogo na wanyenyekevu na wanatafuta kupeleka mbele Ufalme wake wa upendo na wa amani, siku kwa siku. “Kama mnavyofanya hapa katika huduma ya kila siku, Baba Mtakatifu aliongeza “katika urafiki na katika kuishi pamoja.” Na hatimaye Papa Leo XIV aliwashukuru tena wote kaka na dada katika mkutano huo. Na kuwaambia anavyowapeleka katika moyo wake na kuwaachia baraka yake.

Dada Wadogo
Dada Wadogo   (@Vatican Media)
Dada Wadogo
Dada Wadogo   (@Vatican Media)
KITUO CHA WAZEE

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

14 Aprili 2026, 14:44