Papa Leo XIV aanza Ziara yake ya Kitume Afrika-hatua ya kwanza Algeria
Vatican News.
Baba Mtakatifu Leo XIV ameanza Ziara yake ya Tatu Kimataifa ya Kitume barani Afrika, kwa kuondokea Uwanja wa Kimataifa wa Roma - Fiumicino kwa kuanzia na Taifa la Algeria kati ya mataifa atakayotembelea kuanzia tarehe 13 hadi 23 Aprili 2026 ambayo ni Cameroon, Angola na hatimaye Guinea ya Ikweta.
Ratiba ya Papa: Siku yake ya mwanza nchini Algeria ni nzito
Ratiba ya Papa Leo XIV akiwa Nchini Algeria kwa siku ya tarehe 13 Aprili, baada ya kufika, saa 4.45 atatembelea mnara wa mashahidi wa Maqam Echahidi, na kutoa salamu.
Saa 5 :15 Ziara kwa Rais wa Jamhuri katika Jumba la Rais.
Saa 6.00 mchana atakutana Mamlaka na vyama vya kiraia na kikundi cha kidiplomasia katika Kituo cha Mikutano cha “Djamaa el Djazair,” ambapo Papa atatoa hotuba.
Saa 9.45 alasiri atatembelea Msikiti Mkuu wa Algeri na wakati saa 10.35 jioni atatembelea kwa faragha kituo cha upendo na urafiki cha Watawa wa Kiagostiniani, wamisionari huko Bab El Oued .
Na hatimaye saa 11.10 anatarajiwa kufanya mkutano na Jumuiya ya Walgeria katika Basilika ya Mama Yetu wa Afrika, ambapo Papa Leo XIV atahutubia.
Telegram kwa Rais wa Italia
Papa Leo XIV akiwa ndani ya Ndege amemtumia telegramu Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella kuwa,“Wakati ambao ninafunga mkanda kutimiza ziara ya kitume nchini Algeria, Cameroon, Angola na Guinea ya Ikweta, kwa kuhuishwa na shauku hai ya kukutana na ndugu katika Imani na wakazi wa Mataifa hayo pendwa, ninayo furaha ya kukuelekea wewe Bwana Rais, salamu zangu, ambazo zinasindikizana na sala "kwa ajili ya mema na ustawi wa watu wote wa Italia."
Mwisho wa sasisho la habari hii ni saa 3.59 asubuhi Jumatatu tarehe 13 Aprili 2026
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
