Papa Leo XIV:Kanisa linalozaliwa halina mkataba wa kijamii ni maelewano na upendo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza ibada misa Takatifu katika Basilika ya Mtakatifu Agostino huko Annaba, Jumannne tarehe 14 Aprili 2026 ikiwa ni siku yake ya Pili akiwa katika Ziara yake ya Kitume ambpo imeongozwa na mvua nyingi kama wasemavyo kuwa ni baraka ya Mungu. Akianza mahubiri yake alisema “Kaka na dada, Neno la Mungu linapitia historia na kupyaisha na sauti ya kibinadamu ya mwokozi. Leo tunasikia Injili, habaria Njema kwa nyakati zote, katika Basilika hii ya Annaba ya Mtakatifu Agostino, Askofu wa Hippo ya Zamani. Katika karne nyingi, maneneo waliyokuwamo yalibadilishwa jina, lakini Watakatifu wanabaki kuwa kama wasimamizi wao na mashuhuda waamini waliofungamana na ardhi hiyo inayotoka Mbinguni. Na ndiyo mwendelezo huo ambao Bwana anaangaza katika usiku wa Nikodemu: Na katika nguvu ambayo Kristo anaingiza katika udhaifu wa imani yake na uthabiti wa utafutaji.
Kuzaliwa kutoka Juu
Kwa kutumwa na Roho Mtakatifu ambaye, ni “Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui inakotoka wala inakokwenda”(Yh 3,8), Yesu kwa Nicodemu ni mgeni maalum. Anamwita kiukweli maisha mapya na kupatia mwingiliano wake na hata sisi, kazi ya kushangaza “unapaswa kuzaliwa kutoka juu(Yh 3,7). Na tazama mwaliko kwa kila mwanaume na mwanamke anayetafuta wokovu. Kutoka wito wa Yesu ndipo utume unaanza wa Kanisa lote, na hivyo kwa Jumuiya nzima ya kikristo ya Algeria: kuzaliwa kwa upya kutoka juu yaani kwa Mungu. Katika muktadha huo, imani inashinda ugumu wa ardhi na neema ya Bwana inafanya kuchanua maua katika jangwa. Pamoja na hayo uzuri wa ushauri huo unapelekea jaribu, ambalo Injili inatualika kupitia pamoja,” Papa alielezea.
Maneno ya Yesu yana nguvu za uwajibikaji:Tuzaliwe upya kutoka juu
Maneno ya Kristo kiukweli, yana nguvu zote za uwajibikaji, kwamba “lazima tuzaliwe upya kutoka juu! Ulazima huo unasikika katika masikio yetu kama amri isiyowezekana. Kwa kusikiliza kwa makini, Yule anayetoa, tunaelewa, lakini kuwa si jambo gumu la kuwekewa, wala kulazimishwa au zaidi kuhukumiwa kushindwa. Kinyume chake, jukumu lililoelezwa na Yesu kwetu sisi, ni zawadi ya uhuru, kwa sababu inatuonesha uwezekano usiotarajiwa kuwa “kwa neema ya Mungu tunaweza kuzaliwa upya kutoka juu.
Lazima kufanya hivyo kwa hiyo kwa mujibu wa mapenzi yake , ambayo yanatamani kupyaisha ubinadamu kwa kuuita katika muungano wa maisha ambayo yanaanza na imani. Wakati Kristo anatuomba kupyaisha kuanzia mwanzo maisha yetu, pia anatupatia nguvu za kufanya hivyo. Alisema hayo vizuri Mtakatifu Agostino ambaye anasali hivi: “Kutoka kwa Bwana ambaye ana amri na kuamuru kile anachopenda (Maungamo, X, 29, 40).
Kuuliza jinsi gani inawezekana wakati ujao wa haki na amani na maelewano na wokovu
Kwa hiyo tunapojiuliza jinsi gani inavyowezekana wakati ujao wa haki na amani, wa maelewano na wa wokovu, tukumbuke kuwa tuko tunauliza maswali kwa Mungu yale ambayo Nikodemu aliuliza: “Ni kweli kwamba historia yetu inaweza kubadilika? Sisi ambao tumejazwa hivi matatizo, mitego na mahangaiko! Kweli maisha yetu yanaweza kuanza mwanzo? Ndiyo! Papa alithibitisha na kuongeza Uthibitisho wa Bwana, uliojaa hivyo upendo, unajaza mioyo yetu ya matumaini. Haijalishi jinsi tulivyo kandamizwa na uchungu au dhambi: Msulibiwa anachukua uzito huu na sisi na kwa ajili yetu. Haijalishi tumekata tamaa namna gani, katika udhaifu wetu: ni hasa hapo ambapo inajionesha nguvu ya Mungu, ambaye alimfufua Kristo kutoka kwa wafu kwa kutoa maisha Ulimwenguni. Kila mmoja anaweza kufanya uzoefu wa ushuhuda wa maisha mapya ambayo yanatokana na imani katika Mkombozi.
Mfano wa Mtakatifu Agostino:Nisingekuwa hivi kama usingekuwa ndani mwangu
Baba Mtakatifu alieleza tena kuwa Mtakatifu Agostino, anatupatia mfano: kabla ya hekima yake, tunazama Yeye uongofu wake. Kuzaliwa upya , kwa uweza wa kimungu unasindikizwa na machozi ya mama yake Mtakatifu Monika , ambaye kwake yeye alitamka “ Mimi nisingekuwa hivyo, Mungu wangu, nisingekuwa hivyo katu, Wewe ulikuwa ndani mwangu. Au bora zaidi nisingekuwa hivyo kama wewe usingekuwa ndani mwangu”(Maungamo, I, 2). Kwa hiyo Wakristo wanaozaliwa kutoka juu, waliozaliwana Mungu kama kaka na dada wa Yesu na Kanisa ambalo linamwilishwa kwa Sakramenti ni umbu linalokaribisha watu wote wa dunia. “Kama ilivyo sikika somo la Matendo ya mitume ambalo linatoa ushuhuda kwa kusimulia mtindo unaotambulisha ubinadamu uliopyaishwa na Roho Mtakatifu (Mdo 4,32-37). Papa Leo XIV alisisitiza kuwa hata leo hii inahitajika kukaribisha na kutimiza kanuni hiyo ya kitume, kwa kutafakari kama muktadha wa mageuzi ya kikanisa: mageuzi ambayo yanaanzia moyoni ili kuwa kweli, na kutazama wote, kuwa na ufanisi.
Kanisa linalozaliwa halina mkataba wa kijamii,bali maelewano katika imani na upendo
Awali ya yote kiukweli wengi walioamini, walikuwa na moyo mmoja na roho moja(Mdo 4,32). Umoja huu wa kiroho ni maelewano: ikiwa inamaanisha vema muungano wa mioyo ambayo inadunda pamoja, kwa sababu umeungana na ule wa Kristo. Kanisa linalozaliwa halitegemea mkataba wa kijamii, bali katika maelewano katika imani, katika upendo, mawazo na chaguzi za maisha ambayo kiini chake ni upeno unaofanywa na mtu ili kuongoa watu wote wa dunia. Katika sehemu ya pili ni kushangazwa na matokeo hayo ya umoja wa kiroho wa waamini ni kwamba, “Kila kitu kilikuwa pamoja katika ushirika”(Mdo 4,32). Wotu walikuwa na kila kitu, kwa kishirikishana mema ya kila mtu kama wajumbe wa mwili mmoja. Hakuna aliyekosa chochote, kwa sababu kila mmoja alishirikisha kile alichokuwa nacho.
Kwa kubadilisha hivyo zawadi binadamu, ile ya kuweka pamoja kidugu, haiwakilishi utopia ikiwa si mioyo ya ushindani kati yao na mioyo ya uchoyo binafsi. Kinyume chake, imani katika Mungu mmoja, Bwana wa Mbingu na dunia anayeunganisha watu kwa mujibu wa haki kamili, na kualika wote katika upendo, yaani kupenda kila kiumbe kwa upendo ambao Mungu aliutoa katika Kristo. Kwa njia hiyo hasa mbele ya umaskini na ukandamizaji, wakristo wana msimbo msingi wa upendo: “Tuwafanyie wale walio karibu nasi kile ambacho tungependa kutendewa sisi(Mt 7,12).” Kwa kuhuishwa na sheria hii ambayo Mungu aliandika katika moyo, Kanisa daima linazaliwa kwa sababu mahali palipo na kukata tamaa, liwashe tumaini, mahali palipo na taabu, lilete hadhi, penye migogoro lilete upatanisho
Upendo kabla ya kuwa jukumu la kimaadili ni ishara ya wokovu
Papa alielezea sehemu ya tatu kuwa katika Matendo ya mitume” tunapata msingi wa maisha mapya ambayo yanazungukia watu wa kila lugha na tamaduni. “Na kwa nguvu nyingi mitume walitoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu, na neema nyingi ikawa juu yao wote(Mdo 4,33).” Upendo uliowahuisha kabla ya kuwa jukumu la kimaadili, ni ishara ya wokovu: Mitume walitangaza kuwa maisha yetu yanaweza kubadilisha kwa sababu Kristo amefufuka katika wafu. Shughuli ya kwanza ya mitume, wahudumu wa Injili ni kutoa ushuhuda kwa Mungu ulimwenguni kwa moyo mmmoja na roho moja, bila wasiwasi inyotuharibu kwa hofu na wala namna ya kudhoofisha hadhi.” Pamoja nao ndug wa kiaskofu na kwa wote, Papa Leo XIV alisema kupyaisha kila wakati utume huo kwa ajili ya wote , na kwa wale ambao wamekabidhiwa kwao ili Kanisa zima liweze kuwa katika huduma ya ujumbe wa maisha mapya, kwa wale ambao wanakutana nao.
Wakristo Algeria kama Ishara nyenyekevu
Katika nchi hiyo, Papa Leo XIV alisema wakristo wa Algeria, wabaki kama ishara nyenyekevu na aminifu ya upendo wa Kristo. Washuhudie Iinjili kwa ishara rahisi, uhusiano halisi na mazungumzo ambayo ni kuishi siku hadi siku na kwa hiyo wanaweza kutoa ladha na mwanga mahali wanapoishi. Uwepo wao katika Nchi unafanya kufikiria ubani: chembe inayowaka ambayo inasambaza harufu nzuri kwa sababu inatoa utukufu kwa Bwana na furaha na faraja kwa kaka na dada wengi. Ubani huo mdogo, ambao ulikuwa katikati, Papa alisema unaalika “kuwelekeza mioyo yetu kwa Mungu, kutia moyo mwingine ili kuhifadhi katika matatizo wakati uliopo.” Kutoka katika kichungi cha moyo wetu, inainuliwa sifa kweli, baraka, maombi na kuwa harufu ya manukato(Ef 5,2) ya huruma, ya sadaka na ya msamaha. Kwa kuhitimisha Papa alisema kuwa historia yao imefanywa kwa ukarimu wa makaribisho, thabiti katika majaribu ambapo hapo walisali, mashahidi, hapo Mtakatifu Agostino alipenda zizi lake kwa kutafuta ukweli kwa shauku na kuhudumia Kristo kwa imani inyaowaka. Papa aliwaomba wawe warithi wa tamaduni hiyo wakishuhudia kwa upendo kidugu na uhuru wa yule anayezaliwa kutoka juu kama tumaini la wokovu kwa ulimwengu," Papa alihitimisha.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
