Papa Leo XIV na Rais Herzog:kufungua tena njia za kidiplomasia
Vatican News
Katika siku ya jumaa Kuu Takatifu asubuhi tarehe 3 Aprili 2026 , Baba Mtakatifu Leo XIV alizungumza kwa simu na Mheshimiwa Isaac Herzog, Rais wa Nchi ya Israeli, katika fursa ya siku kuu ya Pasaka. Haya ni maelezo kutoka taarifa za Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu. “Wakati wa mazungumzo hayo, taarifa inasomeka, “ hitaji la kufungua tena njia zote zinazowezekana za mazungumzo ya kidiplomasia lilirudiwa, ili kukomesha mzozo mkubwa unaoendelea, kwa lengo la kufikia amani ya haki na ya kudumu Mashariki ya Kati yote.”
Taarifa hiyo aidha imebainisha kuwa, “Mazungumzo hayo pia yalilenga umuhimu wa kuwalinda raia na kuhamasisha heshima kwa sheria za kimataifa na za kibinadamu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
