2026.04.13 Papa akizungumza na Waandishi wa habari akiwa kwenye ndege 2026.04.13 Papa akizungumza na Waandishi wa habari akiwa kwenye ndege   (@Vatican Media)

Papa:Mimi si mwanasiasa nazungumza Injili.Viongozi wa dunia,nawaambia:vita viishe!

Wakati wa safari ya ndege ya kwenda Algiers,kituo cha kwanza katika safari yake ya kitume kwenda Afrika,Papa Leo XIV aliwasalimia waandishi wa habari wapatao 70 waliosindikizana naye:“Hii ni safari maalum,ya kwanza nilitaka kufanya.Fursa muhimu sana ya kukuza upatanisho na heshima kwa watu.” Papa aliulizwa kuhusu ukosoaji wa Trump:“Sitaki kuingia kwenye mjadala.Ujumbe wangu ni Injili na ninaendelea kusema kwa nguvu dhidi ya vita.”

Na Salvatore Cernuzio–Kwenye ndege Roma/Algiers.

"Habari za asubuhi nyote, karibuni kwenye ndege!" Papa Leo XIV alionekana mtulivu na mwenye shauku kubwa kuhusu ziara hii ya tatu ya kimataifa ya Kitume barani Afrika, ambayo inaanza leo, Aprili 13. Ziara hii ndefu itamwona Papa wa Marekani akihiji hadi Alhamisi ijayo, tarehe 23, nchini Algeria, Cameroon, Angola, na Guinea ya Ikweta. Mahali ambapo, kama asemavyo, atapeleka "ujumbe wa Kanisa, ujumbe wa Injili: heri wajenzi wa amani." Kwa sababu hii ni jukumu la Papa: si la "mwanasiasa," Papa Leo  aliwambia waandishi wa habari takriban 70 wanaombatana naye kwenye safari hiyo, ambao, saa moja baada ya kupaa, aliwasalimia mmoja baada ya mwingine wakati wa safari ya ndege kwenda Algiers. Ni desturi ya ziara zote za kitume, kuwa  fursa ya kubadilishana zawadi na leo hii pia kutoa maoni—kwa msukumo wa waandishi wa habari—kuhusu kauli mbaya dhidi yake zilizotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Ukweli wa Kijamii.

Papa akiwa kwenye ndege
Papa akiwa kwenye ndege   (@Vatican Media)

Kuzungumza dhidi ya vita

"Sioni jukumu langu kama mwanasiasa, mimi si mwanasiasa, sitaki kuingia katika mjadala naye," Papa alisema, akimrejea rais. "Sidhani kama ujumbe wa Injili unapaswa kutumiwa vibaya kama wengine wanavyofanya. Ninaendelea kuzungumza dhidi ya vita, nikitafuta kuhamasisha amani, kukuza mazungumzo na ushirikiano wa pande nyingi na nchi ili kutafuta suluhisho la matatizo. Watu wengi sana wanateseka leo, watu wengi wasio na hatia wameuawa, na naamini mtu lazima asimame na kusema kuna njia bora zaidi." Kwa hivyo, ujumbe ambao Askofu wa Roma alitaka kurudia ni "sawa kila wakati: amani. Ninasema hivi kwa viongozi wote wa dunia, si yeye tu: tujaribu kukomesha vita na kukuza amani na maridhiano."

Waleta Amani

Kwa mwandishi wa habari wa Marekani aliyeuliza swali hilo hilo, Papa alirudia: "Siogopi utawala wa Trump. Nitaendelea kusema kwa sauti kubwa kuhusu ujumbe wa Injili, ambao Kanisa linafanyia kazi." "Sisi si wanasiasa," Leo alirudia, "hatuoni sera za kigeni kwa mtazamo huo huo. Lakini tunaamini katika ujumbe wa Injili kama waleta amani."

Safari Maalum

Na kujenga amani ndio lengo kuu la Ziara  ya kwenda Afrika. Safari hii, Leo XIV mwenyewe alielezea kwenye kipaza sauti, "ilitakiwa kuwa safari ya kwanza ya upapa wangu." "Tayari mwaka jana, mwezi Mei, nilisema ningependa kufanya ziara yangu ya kwanza kwenda Afrika. Wengine walipendekeza mara moja Algeria kwa ajili ya Mtakatifu Agostino,” aliongeza, akisema “anafurahi sana kutembelea nchi ya Mtakatifu Agostino tena, ambayo inatoa daraja muhimu sana katika mazungumzo ya kidini.”

Fursa ya kutembelea maeneo ya maisha ya Askofu wa Hippo, ambayo sasa ni Annaba, kwa hivyo, kulingana na Papa Leo, “ni baraka kwangu binafsi na kwa Kanisa na ulimwengu. Kwa sababu lazima tutafute madaraja ya kujenga amani na upatanisho.” Kwa mtazamo huu, ziara ya kitume “kiukweli inawakilisha fursa muhimu sana ya kuendelea na sauti ile ile, na ujumbe ule ule, kwamba tunataka kuhamasisha amani na upatanisho na heshima na kuzingatia watu wote.”

Zawadi kutoka Visiwa vya Kanari

Zawadi nyingi alizopokea Papa wakati wa ziara hiyo na waandishi wa habari, wapiga picha, ni vitabu, michoro, barua, na sanamu ndogo ya Mama Yetu wa Shauri Jema, inayoheshimiwa na Shirika lote la Mtakatifu Agostino ambalo anatoka. Miongoni mwa zawadi za mfano zaidi hakika ilikuwa ile ya mwandishi wa habari wa Radio ya Hispania, Eva Fernández: mfano kwa sababu inaunganisha ziara yake barani Afrika na ziara yake ya Hispania mwezi  Juni ujao

Ni kipande cha moja ya "cayucos" nyingi, jina lililopewa boti za msingi zinazotumiwa na wahamiaji wa Kiafrika kuondoka nchini mwao na kushuka karibu na La Restinga, kwenye kisiwa cha El Hierro. Karibu watu 10,600 walifika katika sehemu hii ya kusini kabisa mwa Hispania mnamo 2025 pekee, karibu idadi ya watu wa kisiwa hicho walio chini ya 12,000. Njia ya Visiwa vya Kanari inachukuliwa kuwa miongoni mwa njia hatari zaidi duniani, huku watu wakiwa baharini kwa juma moja karibu.

Papa alisalimiana na waandishi wa habari na kupokea zawadi
Papa alisalimiana na waandishi wa habari na kupokea zawadi   (@Vatican Media)

Kama inavyojulikana, Papa Leo XIV atatembelea Visiwa vya Kanari, akihitimisha ziara yake kwenda Hispania kuanzia tarehe 6  hadi 12  Juni 2026. Papa Leo, alikubali kwa shukrani zawadi hiyo, iliyobarikiwa na Askofu wa Tenerife na inayotoka Senegal na Gambia, akirudia "gracias" kwa Kihispania mara kadhaa. Pia kuhusiana na Hispania, zawadi nyingine kwa Papa Leo ilikuwa nakala ya kilele cha mnara wa Mtakatifu  Bernabé wa Famila Takatifu  ya Kipekee uliyojengwa wakati wa uhai wa Gaudí, kwani alitaka kuhakikisha unakamilika kabla ya kifo chake ili kutumika kama mfano wa minara mingine.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

13 Aprili 2026, 11:59