Rais,Macron wa Ufaransa atakuwa mjini Vatican kwa Papa Leo XIV Aprili 10
Vatican News
Rais wa Ufaransa Bwana Emmanuel Macron atakutana na Papa Leo XIV, mjini Vatican siku ya Ijumaa, tarehe 10 Aprili 2026. Mkuu wa nchi ya Ufaransa ataambatana na mkewe, Bi Brigitte.
Hili lilitangazwa na Matteo Bruni, Msemaji mkuu wa Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu, asubuhi tarehe 1 Aprili 2026, akiwathibitishia waandishi wa habari, matukio yanayotarajiwa na vyombo vya habari vya Ufaransa na pia kutolewa na Jumba la 'Elysée,' yaani 'Ikulu ya Ufaransa.'
Huu utakuwa mkutano wa kwanza wa Bwana Macron na Papa Leo XIV. Rais Macron alikuwa amekutana na Papa Francisko mara kadhaa, na mara ya mwisho ilikuwa ni mnamo tarehe 14 Desemba 2024, huko Ajaccio, wakati wa ziara yake ya Kitume huko Corsica.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
