Katika Maadhimisho ya Pasaka ya Bwana 2026 Baba Mtakatifu Leo XIV anapenda kuwashirikisha uwepo wake wa karibu wanakijiji cha Debel, Lebanon na kwamba, kamwe wasikate tamaa, bali waendelee kuwa na ujasiri. Katika Maadhimisho ya Pasaka ya Bwana 2026 Baba Mtakatifu Leo XIV anapenda kuwashirikisha uwepo wake wa karibu wanakijiji cha Debel, Lebanon na kwamba, kamwe wasikate tamaa, bali waendelee kuwa na ujasiri.  (AFP or licensors)

Ujumbe wa Papa Leo XIV Kwa Wanakijiji wa Debel, Lebanon Msikate Tamaa!

Baba Mtakatifu Leo XIV katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa wanakijiji wa Debel, kilichoko Kusini mwa nchi ya Lebanon, na kusomwa na Askofu mkuu Paolo Borgia, Balozi wa Vatican nchini Lebanon kama sehemu ya Maadhimisho ya Pasaka ya Bwana, anapenda kuwashirikisha uwepo wake wa karibu na kwamba, kamwe wasikate tamaa, bali waendelee kuwa na ujasiri, Kristo Mfufuka yu pamoja nao!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa wanakijiji wa Debel, kilichoko Kusini mwa nchi ya Lebanon, na kusomwa na Askofu mkuu Paolo Borgia, Balozi wa Vatican nchini Lebanon kama sehemu ya Maadhimisho  ya Pasaka ya Bwana, anapenda kuwashirikisha uwepo wake wa karibu na kwamba, kamwe wasikate tamaa, bali waendelee kuwa na ujasiri. Ujumbe huu, ulikuwa umeambatana na msaada wa mahitaji msingi kwa wananchi hawa, ambao wanaendelea kuteseka kutokana na vita kati ya Israeli na Hezbollah. Hawa ni waamini walioamua kubaki katika maeneo yao, licha hatari kubwa iliyoko mbele yao. Huu ni msaada ambao umekusanywa na Ubalozi wa Vatican nchini Lebanon, Shirika la Misaada ya Kanisa Katoliki Lebanon, Caritas Lebanon pamoja wanajeshi kutoka Ufaransa, UNIFIL.

Papa Leo XIV: Katika mateso na mahangaiko yao Kristo Yesu yu karibu nao!
Papa Leo XIV: Katika mateso na mahangaiko yao Kristo Yesu yu karibu nao!   (AFP or licensors)

Itakumbukwa kwamba, kitendo cha kuzuia msaada wa kibinadamu kuwaendea waathirika wa vita ni ukiukwaji mkubwa wa Sheria za Kimataifa. Baba Mtakatifu Leo XIV mwaka 2025 alifanya hija ya kitume nchini Lebanon kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 2 Desemba 2025, ikiongozwa na kauli mbiu "Heri Wapatanishi; Maana hao Wataitwa Wana wa Mungu" (Mt 5:9.) Hija hii ya kitume ililenga pamoja na mambo mengine: Kuleta ujumbe wa haki, amani, na utulivu katika eneo hilo lenye vita, kinzani na mipasuko ya kijamii. Baba Mtakatifu anapenda kuwaonesha wanakijiji hawa wa Debel, ukarimu wake wa kibaba kwa wale wote wanaoteseka. Baba Mtakatifu Leo XIV katika maadhimisho ya Pasaka ya Bwana 2026, huku wakiwa wamegubikwa na hisia za: Huzuni, uchungu na maombolezo makubwa, anawaombea faraja kubwa nyoyoni mwao kwa sababu Kristo Yesu ameshinda dhambi na mauti, amefufuka kwa utukufu.

Katika mateso na mahangaiko yao Kristo Yesu yuko karibu sana nao!
Katika mateso na mahangaiko yao Kristo Yesu yuko karibu sana nao!   (AFP or licensors)

Katika msiba wao mkubwa, katika dhuluma wanayoteseka na katika hisia ya kutelekezwa wanayopitia, lakini watambue kwamba, Kristo Yesu, yuko karibu sana na wao. Katika Sherehe ya Pasaka, Kristo Yesu ameshinda dhambi na mauti; ameshinda nguvu za uovu! Kumbe, hakuna sababu ya kukata tamaa na kuvunjika moyo! Watambue kwamba, hakuna sala, matendo ya mshikamano wa udugu wa kibinadamu, mateso na uchovu ambayo yatapotea. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, Bikira Maria, Mama wa Lebanon huifadhi kila kitu na kukipeleka kwa Mwanaye Mpendwa, Kristo Yesu. Mwishoni, akawapatia baraka zake za kitume. Wakati huo huo, Patriaki Béchara Boutros Raï wa Kanisa la Wamaroniti wa Antiokia, ameoneshwa kusikitishwa kwake kwa Serikali ya Lebanon kuzuia msafara wa msaada wa mahitaji msingi kwa wananchi wa Lebanon ambao wameathirika na vita kati ya Israeli na Hezbollah kwa hakika ni ujumbe wa masikitiko!

Ujumbe wa papa Lebanon
08 Aprili 2026, 15:02