Papa Leo XIV:Kanisa lishughulikie kwa ukomavu matatizo mengi ya familia

Katika ujumbe wa video kwa ajili ya Kongamano la XVI la Kitaifa la Familia lililofanyika,Jumamosi,Mei 30,huko Aparecida,Brazili,Papa Leo XIV alitoa mwaliko wa "kuzitazama familia kwa uhalisia na huruma,"huku akikumbusha "dhamira yao ya msingi na isiyoweza kubadilishwa kama waelimishaji wa amani."

Vatican News

Ukomavu na uhalisia, Huruma na upole. Mbinu mbili ambazo, katika maono ya Papa, lazima ziungane ili kushughulikia vikwazo vinavyozikumba familia  ulimwenguni kote leo. Hili ndilo tumaini lililotolewa katika ujumbe wa video uliochapishwa Jumamosi, Mei 30, wakati wa Kongamano la Kitaifa la Familia, lililoandaliwa na Tume ya Maisha na Familia ya Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Brazil (CNBB) huko Aparecida. “Ninahisi kukubaliana sana nanyi na kazi mnayofanya pamoja, kwa sala na tafakari ya kila mmoja, kuhusu mada muhimu sana: familia.” Alisema Papa kwa lugha ya kihispania.

Mbinu ya huruma na Utambuzi wa Busara

Papa Leo XIV  anakumbusha mafundisho ya Kanisa kwamba familia ndiyo "kiungo cha kwanza na muhimu cha kijamii, na kwa hivyo lazima ilindwe na kuhamaishwa”. Kwa upande wake, familia inaitwa kutangaza upendo wa Mungu katika jamii ya leo hii, ikielewa kikamilifu utambulisho wake kama "jumuiya ya kipekee ya watu iliyoundwa na mwanamume na mwanamke" pale tu "inapomtazama Bwana Yesu na sadaka aliyoitoa msalabani kwa ajili ya Bibi Arusi wake, Kanisa."

Hata hivyo, ni muhimu kuziona familia kwa uhalisia na huruma, zikijua matatizo mengi yanayowakumba, yaani, udhaifu wao, migogoro, mateso, na hali nyingine nyingi za mateso. Yote haya yanahitaji mbinu ya rehema na utambuzi wa busara na uliokomaa kutoka kwa Kanisa na wafanyakazi wa kichungaji.

"Familia ni yenye kuelimisha Amani kwanza"

Baba Mtakatifu Leo alitoa mfano wa Familia Takatifu ya Nazareti ili kutafakari "fadhila ndogo na za msingi za nyumbani" na kuzitumia kwa kuzingatia mifano ya Mtakatifu Yosefu na Bikira Maria. Kiukweli, kama Papa Benedikto XVI alivyoonesha, familia inatekeleza utume mkuu na usioweza kubadilishwa kama "Yenye Kuelimisha Amani."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

30 Mei 2026, 14:50