Papa na kijana Ignacio Gonzalves. Papa na kijana Ignacio Gonzalves. 

Mkumbatio wa Papa na Ignacio huko Castel Gandolfo:“Nilimweleza kuwa nimepona”

Katika umati wa watu nje ya Villa Barberini huko Castel Gandolfo kulikuwa na familia ya mvulana wa Kihispania mwenye umri wa miaka 15 aliyelazwa hospitalini katika kiangazi 2025 kwa sababu saratani,katikati ya Jubilei ya Vijana.Papa Leo XIV alikuwa amemwombea huko Tor Vergata na alikuwa amemtembelea katika Hospitali ya Bambino Gesù.Baada ya matibabu na mateso,lakini pia mshikamano na maombi mengi,anaendelea vizuri.Amemwambia Papa anamsubiri Madrid.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Kumbatio alilokosa jioni ya tarehe 4 Agosti 2025, wakati Papa Leo XIV alipomtembelea Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesù alipokuwa katika chumba kisichofikika yaani chumba cha wagonjwa mahututi, kijana Ignacio alifanikiwa kumpatia Papa Leo XIV jioni hii, ya tarehe 12 Mei 2026, nje ya Villa Barberini huko Castel Gandolfo. "Nilimwambia nimetibiwa, kwamba, namshukuru Mungu, niko sawa, na kwamba nitamsubiri huko Madrid," aliviambia vyombo vya habari vya Vatican. "Alifurahi sana; aliweza kunikumbatia, niliweza kusema kwaheri. Ilikuwa wakati mfupi, lakini ulikuwa mzuri... Namshukuru Mungu na mshukuru Papa!" Alisema kijana huyo.

Papa Castel Gandolfo akisalimiana na watu
Papa Castel Gandolfo akisalimiana na watu

Ugonjwa wa ghafla na sala ya Papa

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka kumi na tano alilazwa katika Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesù katika msimu wa kiangazi 2025, siku chache baada ya kufika Roma na kaka yake na dada yake ili kushiriki katika matukio ya Jubilei ya Vijana. Kile alichokielezea kama "mlipuko" kifuani mwake kilimpeleka kwenye ukingo wa kifo: ugonjwa mbaya wa saratani katika mfumo wa limfu.

Papa Leo XIV baada ya kujua tukio hilo kupitia marafiki wa pande zote, aliomba maombi kwa ajili ya kijana huyo kutoka jukwaani huko Tor Vergata, na jioni ya tarehe 4 Agosti 2025, yeye binafsi na bila kutarajia alitembelea kitengo cha wagonjwa mahututi kumsalimia baba yake, Pedro Pablo, mama yake, Carmen Gloria, kaka yake, Pedro Pablo Jr., na dada yake, Adela. Usikivu wa Papa Leo XIV ulileta historia ya mateso na matumaini na imani thabiti, mbele ya habari za kimataifa, ukitoa wimbi la maombi, mshikamano, na ukaribu kwa familia hiyo ambayo ilijikuta ikisafirishwa usiku kucha kutoka Murcia, nchini Hispania, hadi Italia ili kumtunza mtoto wao na kaka yake.

Papa akisalimu waamini
Papa akisalimu waamini

Miezi ya matibabu na mateso, lakini pia upendo na maombi

Maisha yameendelea miezi hii iliyopita, katikati ya maumivu, matibabu, kupanda na kushuka. Sasa Ignacio amepona, na yuko nje ya hospitali, mbali na mirija, IVs, na bandeji. Na alitaka kumwambia Papa Leo XIV kuwa hii kama njia ya kusema asante pia. "Nilitaka kumwambia Papa kwamba sasa nimepona ugonjwa huo. Nilipokea habari jana. Madaktari waliniambia kila kitu kiko sawa, kwamba nimemaliza matibabu, na kwamba saratani ya limfu imetoweka. Sasa tunatazama ni lini tunaweza kurudi, labda tarehe 20, lakini sijui..." alisema Ignacio, akiwa na mama yake pembeni mwake.

Mama shujaa ambaye, jioni ya tarehe 4 Agosti alizungumza na vyombo vya habari vya Vatican, uhakika wake wa msaada wa Mungu kwa mwanae, kwa ajili yake mwenyewe, mumewe, na watoto wake wengine. Usiku wa leo anamtazama mtoto mdogo wa nyumba, akitabasamu na kwa sura ya kuridhika kwa kumuona amesimama tena, akizungumza, akiwa na ujasiri, mtulivu. Walipoulizwa wanakumbuka nini kuhusu miezi hii tangu kuanza kwa ugonjwa huo, wote wawili walijibu kwa njia ile ile: "Mungu amekuwapo maishani mwetu siku zote."

Papa Leo XIV

"Asante!"

Na Papa pia alikuwepo: "Nataka kumshukuru kwa maombi..." anasema Ignacio. "Alikuwa na wasiwasi sana, aliuliza." Baada ya ziara hiyo, kulikuwa na mawasiliano zaidi kati ya Papa Leo XIV na akina Gonzalvezes: "Nilimwambia kuhusu matatizo yangu." Lakini matatizo ya kiafya tu, kwa sababu, vinginevyo, "hakuna" kilichokosekana, alimhakikishia mvulana: "Namshukuru Mungu, kila kitu kimefika. Hakuna hata kimoja kati ya nilicho nacho sasa ambacho ni changu, hakuna hata kimoja. Muujiza!" Kulingana na kijana huyo, msaada wa kupona kwake pia ulitoka mbinguni: "Babu yangu, bibi yangu, marafiki wa wazazi wangu, na pia... Mtakatifu Clara. Nilipoamka, nilimwona Mtakatifu Clara. Daktari aliyenitibu hospitali ya Bambino Gesù anaitwa Clara, kwa hivyo nadhani Mtakatifu Clara alifanya kitu.”

Msaada kutoka mbinguni na msaada wa wengi

Lakini pia watakatifu wengine, alirudia kusema mama yake. Kwanza kabisa, Mtakatifu Charbel, Mtawa wa Lebanon anayesifiwa kwa uponyaji zaidi ya 20,000. Papa alikuwa ameomba kwenye kaburi lake wakati wa Ziara yake ya Kitume  ya kwenda Beirut. Na wakati wa ziara yake huko Bambino Gesù, alikuwa ameacha masalia katika chumba cha wagonjwa mahututi. "Tulimwomba Mtakatifu Charbel msaada," alisema Carmen Gloria, "na pia Mtakatifu Carlo Acutis. Tangu mwanzo, nilikuwa na picha yake ya Mtakatifu Carlo. Pia tuliomba maombezi ya Carmen Hernández, mwanzilishi mwenza wa Njia ya Neokatekumenali, ambayo familia hiyo ni mwanachama wake.

Salfi ya Pamoja
Salfi ya Pamoja

Mbali na usaidizi wa kiroho, Carmen Gloria alishuhudia usaidizi mwingi wa kimwili: "Ilikuwa wakati wa neema. Tunajua ilikuwa neema kwa sababu isingewezekana peke yetu, katika nchi ambayo hatuijui, yenye lugha ambayo hatuzungumzi, yenye ugonjwa ambao ulionekana kuwa mbaya mara moja. Kuanzia siku moja hadi nyingine, kila kitu kilibadilika. Tuliteseka sana, lakini pia tulifarijika sana na Mungu kwa matokeo yake halisi, ya kimwili na ya kiroho. Upendo, kweli... Kulikuwa na watu walioacha nyumba zao ili tuweze kuishi huko." Nchini Hispania, familia ya Gonzalvez inasema wanabeba "ishara ya upendo wa Mungu." Mtoto  aliyeponywa, Papa karibu, mamia ya watu wakiwa tayari kuwaunga mkono. "Yote ni muujiza!"

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

12 Mei 2026, 21:30