2026.03.04 Mkuu wa Kanisa la Armenia Aram I 2026.03.04 Mkuu wa Kanisa la Armenia Aram I 

Mkuu wa Kanisa la Armenia Aram I atatembelea Papa Mei 18

Mkutano huo,wa kwanza kati ya Papa na Mkuu wa Kanisa la Kitume la Armenia,utafanyika Vatican.Mazungumzo ya faragha na muda wa sala vimepangwa katika Kanisa la Urban VIII.

Vatican News

Jumatatu tarehe 18 Mei 2026, Mkuu wa Wakatoliki wa Kanisa la Kitume la Armenia - Kiti cha Kilikia, Aram I, atamtembelea Papa Leo XIV.

Taarifa ya Kiti Kitakatifu ilitangaza hilo Jumamosi tarehe 16 Mei 2026, ikisisitiza kwamba hii itakuwa ziara rasmi ya kwanza ya Mkuu huyo kwa Papa Leo XIV.

Mkutano huo wa faragha utafuatiwa na wakati wa sala katika Kikanisa cha Urbano VIII cha Jumba la Kitume. Mkuu huyo pia atatembelea Makao Makuu ya Baraza la Kipapa la kuhamasisha Umoja wa Wakristo na mabaraza mengine ya Curia Romana. Mnamo Mei 19, katika Taasisi ya Kipapa ya Mashariki, Aram I atatoa hotuba katika mkutano wa hadhara kuhusu 'changamoto zinazokabili Makanisa katika Mashariki ya Kati.'

Aram I atatembelea Papa

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

16 Mei 2026, 13:31