206.05.27Papa alikutana na Bwana  Pedro Sanchez Perez-Castejon, Waziri Mkuu wa Serikali ya Hispania. 206.05.27Papa alikutana na Bwana Pedro Sanchez Perez-Castejon, Waziri Mkuu wa Serikali ya Hispania.   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akutana na Waziri Mkuu wa Hispania:kuna haja ya uharaka wa kuendelea kuunga mkono amani

Papa Leo XIV,Jumatano Mei 2026 na Waziri Mkuu wa Hispania mjini Vatican,ambapo baadaye walikutana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Parolin.Wakati wa majadiliano,walijadili hitaji la kukuza mazungumzo yenye matunda kati ya Kanisa mahalia na mamlaka za serikali,yanayotegemea heshima ya pande zote na yanayolenga kuhamasisha manufaa ya wote,athari za migogoro ya kimataifa na uhamiaji na uharaka wa kujitolea kuendelea kuunga mkono amani.

Vatican News

Baba Mtakatifu, Jumatano tarehe 27 Mei 2026, katika Jumba la Kitume la Vatican alimpokea Pedro Sánchez Pérez-Castejón, Waziri Mkuu Hispania, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akiambata  na Askofu kuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa  Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Papa akutana na Waziri Mkuu wa Hispania
Papa akutana na Waziri Mkuu wa Hispania   (@Vatican Media)

Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Jimbo, Ofisi ya Vyombo vya habari ya Kiti Kitakatifu imbainisha “kuridhika kulioneshwa kwa Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu ijayo,” kuwa ni “ ishara ya uhusiano mzuri kati ya Vatican na Hispania.”

Kisha katika mkutsano huo “ masuala kadhaa yenye maslahi ya pamoja, kama vile hitaji la kukuza mazungumzo yenye matunda kati ya Kanisa mahalia na mamlaka za serikali,” vilirejewa, lakini pia “kati ya vipengele mbalimbali vya asasi za kiraia, vinavyotegemea kuheshimiana na vinavyolenga kuhamasisha manufaa ya pamoja.”

Waziri Mkuu wa Hispania baadaye alikutana na Katibu Mkuu wa Vatican.
Waziri Mkuu wa Hispania baadaye alikutana na Katibu Mkuu wa Vatican.   (@Vatican Media)

Katika taarifa hiyo aidha inabainisha kuwa “Mazungumzo yaliendelea na masuala ya kimataifa, hasa yakirejea athari za migogoro ya kimataifa, uhamiaji, umuhimu wa ushirikiano wa pande nyingi na heshima kwa sheria za kimataifa, pamoja na uharaka wa kujitolea kuendelea kuunga mkono amani.”

Papa akutana na Waziri Mkuu wa Hispania

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

27 Mei 2026, 17:01