Kanisa la Ivory Cost limepata Askofu Mpya msaidizi wa Jimbo Kuu la Abidjan. Kanisa la Ivory Cost limepata Askofu Mpya msaidizi wa Jimbo Kuu la Abidjan. 

Papa Leo XIV amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Abidjan,Ivory Coast

Padre Aguia Jean Martial Arnaud Kouamé ni Askofu Mpya Msaidizi wa Jimbo Kuu la Abidjan nchini Ivory Cost.Alizaliwa tarehe 26 Machi 1977 huko Abidjan.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatano, tarehe 13 Mei 2026, amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Jiji la Abidjan nchini Ivory Coast Mhs. Padre  Aguia Jean Martial Arnaud Kouamé, ambaye hadi uteuzi alikuwa Paroko wa Mtakatifu Ambroise Ma vigne, kwa kumpatia makao ya Sutunurca.

Wasifu

Mheshimiwa Padre  Aguia Jean Martial Arnaud Kouamé alizaliwa tarehe 26 Machi  1977 huko Abidjan.

Majiundo yake alipata Leseni ya Falasafa na Shahada ya Kwanza ya Taalimungu katika Seminari ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Paulo VI. Alipewa daraja la Upadre kunako tarehe 15 Januari 2005 kwa ajili ya Jimbo Kuu la Abidjan.

Kisha alifunika nyadhifa mbali mbali na kuandelea na masomo  zaidi: Parokia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo huko Abidjan (2005-2008) na Mtakatifu Francis wa Assisi huko  huko Strasbourg (2008-2010); Amehitimu katika Sheria ya Kanisa na Shahada ya Uzamili katika Falsafa na Historia na Falsafa ya Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Strasbourg; Parokia ya Bonne Nouvelle huko Hem (2010-2011) na Mtakatifu Fiacre huko Dunkirk (2011-2013); Alihitimu Taalimungu ya Maadili kutoka Chuo Kikuu cha Lille (2012-2013); Shahada ya Uzamivu katika Maadili, Maadili ya Chaguo na Dini kutoka Chuo Kikuu cha Strasbourg (2013-2018); Parokia ya Notre Dame du Chêne du Pays de Fleckenstein huko Strasbourg (2013-2018); Kanisa la Mtakatifu  Xavier  huko Abobo, Abidjan (2018-2022); Paroko wa Mtakatifu Ambroise Ma Vie huko Abidjan (tangu 2022).

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

 

13 Mei 2026, 18:34