Papa kwa Chuo Kikuu cha Sapienza:"Ni Ulimwengu gani tunawaachia vijana?
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV amefanya ziara yake ya kichungaji katika Jumuiya ya elimu ya Chuo Kikuu cha Sapienza cha Zamani sana Roma na barani Ulaya, tarehe 14 Mei 2026, ambapo alipokelewa kwa shangwe kuu katika Ulimwengu wa Kitaaluma wa vijana kutoka Ulimwengu mzima ambapo takribani zaidi ya watu 5,000 walimpokea katika nafasi za ndani, za kikanisa na Ukumbi Mkuu. Na katika ukumbi mkuu wa chuo walikaa watu 1000 na waliobaki walitazama kupitia Skrini zilizowekwa Nje.
Katika hotuba yake katika Ukumbi huo mkuu, Papa alitoa tafakari pana iliyojumuisha wasiwasi kuhusu silaha za serikali zilizofichwa kama mikakati ya "ulinzi"; himizo la kutumia akili na ujasiri katika kutafuta haki, amani, na ulinzi wa Dunia, na kuchagua njia ya matumizi ya teknolojia kila wakati; na mwaliko wa kusikiliza na kutochochea kutoridhika kwa vijana wengi wenye tafsiri potofu za kuwa walimu. Baba Mtakatifu alianza na salamu kwa Mkuu wa Chuo, Mamlaka za Kisiasa na Kiraia, Maprofesa, Watafiti, na Wafanyakazi wa Ufundi na Utawala, na zaidi ya yote, Wanafunzi! “Nilifurahi kukubali mwaliko wa kukutana na jumuiya ya chuo kikuu cha Sapienza - Chuo Kikuu cha Roma.”
Chuo Kikuu ni Kitovu cha ubor awa taaluma mbalimbali
Chuo Kikuu chao kinatambuliwa kama kitovu cha ubora katika taaluma mbalimbali na, wakati huo huo, kwa kujitolea kwake kwa haki ya kupata elimu, ikiwa ni pamoja na wale wenye rasilimali chache za kifedha, watu wenye ulemavu, wafungwa, na wale ambao wamekimbia maeneo ya vita. Kwa mfano, Papa alisema anavyothamini sana ukweli kwamba Jimbo la Roma na Chuo Kikuu cha Sapienza vimesaini makubaliano ya kufungua njia ya kibinadamu ya chuo kikuu kutoka Ukanda wa Gaza. Kwa hivyo ni muhimu kwa Papa Leo XIV, ambaye “nimekuwa Askofu wa Roma kwa zaidi ya mwaka mmoja, kuweza kukutana nanyi." Papa Leo XIV katika hotuba yake alipenda kuzungumza kwanza na Wanafunzi alafu kuelekeza wakunzi.
Mstakabali bado ni uandikiwa hakuna wa kuwaibia
Akiearejea alisema “Njia za jiji la chuo kikuu, ambazo nilitembea ili kufika hapa, hupitiwa kila siku na vijana wengi, waliojaa hisia zinazokinzana. Nakufikiria wakati mwingine ukiwa huru, unafurahi na ujana wako, ambao, hata katika ulimwengu wenye matatizo uliojaa dhuluma mbaya, hukuruhusu kuhisi kwamba mustakabali haujaandikwa na kwamba hakuna mtu anayeweza kukuibia. Kwa hivyo, masomo mnayofanya, urafiki mliouunda kwa miaka mingi, na kukutana na wataalamu mbalimbali wa mawazo ni ahadi ya kile kinachoweza kutubadilisha kuwa bora, hata kabla ya ukweli unaotuzunguka.Wakati hamu ya ukweli inakuwa utafiti, ujasiri wetu katika masomo unashuhudia tumaini la ulimwengu mpya.
Uhusiano wa Mtakatifu Agostino
Papa alieleza juu ya kuwa na uhusiano na mwanzishi wa Shirika lake kwamba, “Mnajua kwamba nimeunganishwa kiroho na Mtakatifu Agostino, ambaye alikuwa kijana asiyetulia: pia alifanya makosa makubwa, lakini hakuna hata moja ya shauku yake ya uzuri na hekima iliyopotea. Katika suala hilo, nilifurahi kupokea maswali mengi kutoka kwenu: mamia! Ni wazi, haiwezekani kuyajibu yote, lakini nayaweka akilini, nikitumaini kwamba kila mtu atatafuta fursa zaidi za mazungumzo. Hii pia ndiyo sababu mapadre wa vyuo vikuu wapo, ambapo imani hukutana na maswali yenu,” Papa alisisitiza
Hatupaswi kupuuza wasiwasi wa mapambano ya vijana
Papa alifafanua suala lingine kuwa “Lakini pia kuna upande wa kusikitisha wa wasiwasi: hatupaswi kupuuza ukweli kwamba vijana wengi wanapambana. Kila mtu hupata nyakati ngumu; hata hivyo, wengine wanaweza kuhisi kama haziishi. Leo, hii inategemea zaidi na vitisho vya matarajio na shinikizo la kufanya kazi. Ni uongo ulioenea wa mfumo uliopotoka, ambao unapunguza watu hadi idadi, unazidisha ushindani na kutuacha kwenye mizunguko ya wasiwasi. Ugonjwa huu wa kiroho unaowapata vijana wengi unatukumbusha kwamba sisi si jumla ya kile tulicho nacho, wala dutu iliyokusanywa bila mpangilio katika ulimwengu kimya. Sisi ni hamu, si algoriti! Papa aliongeza "Hasa hadhi hii maalum ya sisi, inanifanya nishirikishe maswali mawili nanyi.”
Ninyi ni nani?
Katika hilo la kwanza Papa Leo XIV aliuliza: “Kwenu vijana, wasiwasi huu unauliza: "Nyinyi ni nani?" Kiukweli, kuwa sisi wenyewe ni dhamira kuu ya maisha ya kila mwanaume na mwanamke. "Nyinyi ni nani?" ni swali tunalouliza kimya kimya kwa Mungu; swali ambalo sisi pekee tunaweza kujibu, kwa ajili yetu wenyewe, lakini ambalo hatuwezi kujibu peke yetu. Sisi ni vifungo vyetu, lugha yetu, utamaduni wetu: sababu kubwa zaidi ni kwa nini ni muhimu kwamba miaka ya chuo kikuu iwe wakati wa kukutana vizuri.
Ni Ulimwengu gani tunawaachia vijana?
Kwa hivyo, kwa wale walio wazee na vijana wasioridhika huuliza: "Tunaacha ulimwengu wa aina gani?" Kwa bahati mbaya, ulimwengu uliopotoshwa na vita na maneno kama ya vita. Huu ni uchafuzi wa akili, ambao kutoka ngazi ya kijiografia huvamia kila uhusiano wa kijamii. Kwa hivyo, kurahisisha kunakoleta maadui lazima kurekebishwe, hasa katika vyuo vikuu, kwa kuzingatia ugumu na utumiaji wa busara wa kumbukumbu. Hasa, mkasa wa karne ya ishirini haupaswi kusahaulika,” Papa alionya. Kilio cha "hakuna vita tena!" cha watangulizi wangu, kinachoendana sana na kukataliwa kwa vita kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Italia, kinatuhamasisha kwenye muungano wa kiroho na hisia ya haki inayoishi mioyoni mwa vijana, na wito wao wa kutojifunga ndani ya itikadi na mipaka ya kitaifa.”
Kuongezeka kwa matumizi ya kijeshi Ulimwenguni hasa Ulaya
Kwa mfano, Papa aliongeza “ katika mwaka uliopita, ukuaji wa matumizi ya kijeshi duniani kote, na hasa barani Ulaya, umekuwa mkubwa sana: Utengenezaji upya wa silaha unaoongeza mvutano na ukosefu wa usalama, unaopunguza uwekezaji katika elimu na huduma za afya, unaodhoofisha uaminifu katika diplomasia, na kuwatajirisha wasomi ambao hawajali chochote kwa manufaa ya wote, haupaswi kuitwa "ulinzi."
Umakini wa kutumia akili unde
Kadhalika Papa alisisitiza: “Zaidi ya hayo, ni lazima tufuatilie maendeleo na matumizi ya akili Unde katika nyanja zote mbili za kijeshi na za kiraia, ili isiwanyime watu majukumu ya kuchagua na kuzidisha janga la migogoro. Kinachoendelea Ukraine, Gaza, maeneo ya Palestina, Lebanon, na Iran kinaonesha mageuzi yasiyo ya kibinadamu ya uhusiano kati ya vita na teknolojia mpya, yanayoelekea kwenye maangamizi. Acha utafiti, ugunduzi, na uwekezaji viende kinyume: viwe "ndiyo" kali kwa maisha! Ndiyo kwa maisha yasiyo na hatia, ndiyo kwa maisha ya vijana, ndiyo kwa maisha ya watu wanaolilia amani na haki!
Ikolojia
Baba Mtakatifu akiendelea alisema “ eneo la pili la ahadi ya pamoja linahusu ikolojia. Kama Papa Francisko alivyotuambia katika Waraka wake wa Laudato Si', "kuna makubaliano makubwa ya kisayansi kwamba tunashuhudia ongezeko la joto linalosumbua mfumo wa hali ya tabianchi" (n 23). Zaidi ya muongo mmoja umepita tangu wakati huo, na licha ya nia njema na juhudi kadhaa katika mwelekeo huo, hali haionekani kuimarika.
Amani inayoondoa na kupokonya silaha
Katika hali hii, Papa ametoa mwaliko “hasa, vijana “msikubali kujiuzulu, bali mbadilishe wasiwasi wenu kuwa unabii.” Hasa wale wanaoamini wanajua kwamba historia haiangukii mikononi mwa kifo bila matumaini, bali inalindwa kila wakati, chochote kitakachotokea, na Mungu anayeumba uhai kutokana na kitu chochote, anayetoa bila kuchukua, anayeshiriki bila kula. Leo, matumizi ya dhana ya umiliki na utumiaji hovyo yanafungua njia kwa dhana mpya ambayo tayari inachipuka: eleweni, mjifunzeni, na mlinde haki!
Papa amewahimiza kwamba “Pamoja nami na kaka na dada wengine wengi, iweni mafundi wa amani ya kweli: amani inayoondoa silaha na kupokonya silaha, nyenyekevu na vumilivu, hivyo mkifanya kazi kwa ajili ya maelewano miongoni mwa watu na ulinzi wa Dunia.” Papa alieleza: “Kuna haja ya kili na ujasiri wenu wote. Kiukweli, unaweza kuwasaidia wale watakaokuja baada yenu kuanzisha upya upeo wa kweli wa maana, ili tusiishie kwenye picha nyingine ya haraka ya hali tunayojikuta nayo. Lazima tubadilike kutoka kwenye utafsiri hadi vitendo: kwa kuwa jamii yenye watoto wachache zaidi haizingatii sana, tunashuhudia kwamba ubinadamu una uwezo wa mustakabali, unapoujenga kwa hekima."
Kikuu ni mhalia pa kujifunza a kuunda mawazo
Papa aliwageukia wakufunzi kwamba Chuo Kikuu chenu, ambacho kina jina la Mungu, ni mahali pa kujifunza na kujaribu, ambapo kimeunda mawazo muhimu kwa karne nyingi. Hasa, nyinyi maprofesa mnaweza kukuza mawasiliano yenye matunda na akili na mioyo ya vijana: hili ni jukumu gumu, hakika, lakini la kusisimua. Ni muhimu kuwaamini wanafunzi wenu. Kwa hivyo, mjiulize mara nyingi: Je, ninawaamini?
Kufundisha ni aina ya upendo
Kufundisha ni aina ya upendo, kama vile kumwokoa mhamiaji baharini, maskini mtaani, au dhamiri iliyokata tamaa inavyopaswa kuwa. Ni kuhusu kupenda maisha ya mwanadamu kila wakati, kuthamini uwezo wake, ili kuzungumza na mioyo ya vijana, bila kutegemea ujuzi wao pekee. Kisha ufundishaji unakuwa ushuhuda wa maadili katika maisha ya mtu: ni kujali ukweli, ni hisia ya kukaribishwa kwa kile ambacho hakijaeleweka bado, ni kusema ukweli. Baada ya yote, kungekuwa na maana gani katika kumfundisha mtafiti au mtaalamu ambaye anashindwa kukuza dhamiri yake mwenyewe, hisia ya haki, na kuheshimu kile ambacho hakiwezi na kisichopaswa kudhibitiwa?
Maarifa hayatumiki kufika malengo ya kitaalamu tu ni kujitambua mtu ni nani?
Kiukweli, Papa Leo XIV alisisitiza: “maarifa hayatumiki kufikia malengo ya kitaaluma tu, bali pia kutambua mtu ni nani. Kupitia madarasa, mafunzo ya vitendo, mwingiliano na jiji, tasnifu, na udaktari, kila mwanafunzi anaweza kupata motisha mpya kila wakati, kuleta utaratibu katika masomo na maisha, kwa zana na malengo." Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alisema: "Wapendwa, ingawa ninawatia moyo katika zoezi hili la kila siku, ziara yangu inakusudiwa kuwa ishara ya muungano mpya wa kielimu kati ya Kanisa la Roma na Chuo Kikuu chenu maarufu, ambacho kilizaliwa na kukua ndani ya Kanisa." Papa aliongeza "Nawahakikishia nyote ukumbusho wangu katika sala, na kwa moyo wote naomba baraka za Bwana ziwe juu ya jumuiya nzima ya Sapienza. Asante!"
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
