Papa atasali Rozari kwa ajili ya Amani tarehe 30 Mei 2026 katika Groto ya Mama Maria wa Lourdes mjini Vatican. Papa atasali Rozari kwa ajili ya Amani tarehe 30 Mei 2026 katika Groto ya Mama Maria wa Lourdes mjini Vatican.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV atasali Rozari kwa ajili ya Amani pamoja na madhabahu Ulimwenguni

Papapa Leo XIV anatarajia kusali sala ya Maria katika Pango la Mama Yetu wa Lourdes katika Bustani za Vatican,Jumamosi Mei 30,saa 1:00 jioni masaa ya Ulaya.Sehemu nyingi muhimu za ibada zitawaalika waamini na mahujaji kujiunga na mpango unaoendelezwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji.Washiriki pia wataweza kushiriki kwenye Skrini kubwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Vatican News

Tunapokaribia kufunga mwezi Mei, uliowekwa na Mama Kanisa kusali Rozari kwa mama Maria, Papa Leo XIV anarudi kuombea amani, pamoja na ushiriki wa waamini kupitia madhabahu ya Mama Maria muhimu zaidi Ulimwenguni.  Kwa njia hiyo Papa anatarajia kusali Rozari Takatifu, akihitimisha mwezi huu wa Maria, Jumamosi tarehe 30 Mei 2026 , saa 1:00 jioni, katika Pango la Mama Yetu wa Lourdes katika Bustani za Vatican.

Baba Mtakatifu  alikuwa tayari ameomba zawadi ya amani, nia ambayo aliwahimiza waamini kusali kila wakati, wakati wa mkesha wa tarehe 11 Aprili 2026   katika Basilika ya Mtakatifu Petro.

Madhahu ulimwenguni kote yanajiunga

Kama ilivyoelezwa katika taarifa kutoka kwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, ambalo linaendeleza mpango huo kupitia Kitengo chake cha Masuala ya Msingi ya Uinjilishaji ulimwenguni na Madhabahu  mengi ulimwenguni kote yatawaalika mahujaji na waamini  kusali sala ya Maria, wakiwa wameungana kiroho na  Baba Mtakatifu.

Madhabahu ambazo tayari zinaungana ni: Madhabahu ya Mama wa Mungu (huko Zarvanytsia, Ukraine) tayari yamejiunga na sala ya amani; Madhabahu ya Kimataifa ya Mama Yetu wa Amani na Safari  Njema (huko Antipolo, Ufilipino); Madhabahu ya Mama Yetu wa Rozari (huko Fatima, Ureno); Madhabahu ya Mama Yetu Malkia wa Amani (huko Medjugorje, Bosnia na Herzegovina);

Madhabahu ya Mama Yetu wa  Lourdes (katika kijiji cha kilima huko Ufaransa); Madhabahu ya  Mtakatifu  Charbel Annaya (a Byblos, Lebanon) na madhahabu ya Kipapa ya Nyumba Takatifu (huko Loreto, Italia).

Jinsi ya Kushiriki

Unaweza kushiriki katika mpango wa maombi wa Papa katika Bustani za Vatican kwa kuchukua tiketi katika Jengo lililoko njia ya Conciliazione 7, katika siku zinazotangulia siku ya kusali Rozari Takatifu, mnamo Mei 28, 29, na 30, kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi saa 11:30 jioni. Lakini pia itawezekana kujiunga na sala hiyo kwenye skrini kubwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro siku hiyo.

Papa na Rozari 30 Mei

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

28 Mei 2026, 18:36