Papa Leo XIV Agosti 22 atatembelea Jamhuri ya San Marino
Katika muktadha wa Ziara katika Jimbo la Rimini na Mkutano wa Watu(Meeting),Papa Leo XIV pia atatembelea Nchi Ndogo ya Jamhuri ya San Marino.
Vatican News
Ziara za Papa Leo XIV nchini Italia sasa zinajumuisha kusimama hata katika Jamhuri ya San Marino. Kulingana na taarifa ya Mkuu wa Nyumba ya Kipapa, inabinisha kuwa kwa kukubali mwaliko wa Kapteni Matteo Rossi na Lorenzo Bugli, Papa atafanya ziara ya kichungaji katika nchi hiyo ndogo asubuhi ya Jumamosi, tarehe 22 Agosti 2026. Wakati huo huo alasiri ya siku hiyo kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali, ziara ya Papa itaendelea katika Mkutano wa Watu(Meeting) na Jiji la Rimini.
28 Mei 2026, 17:02
