Papa Leo XIV akumbuka jaribio la kuuawa kwa Papa Yohane Paulo II,miaka 45 iliyopita

Akiwa katika Uwanja Mtakatifu Petro,Papa Leo XIV alikumbuka jaribio la mauaji kwa Papa Yohane Paulo II mnamo Mei 13, 1981,siku tunayokumbuka Mama Yetu wa Fatima.Papa alizungumza juu ya Maria,akisisitiza ukweli wake wa kihistoria kama mwanamke kijana aliyeitwa kuishi uzoefu wa ajabu.Kwa Mama Yetu,Papa alimkabidhi kilio cha amani watu wanaosumbuliwa na vita.

Na Angella rwezaula – Vatican.

Tarehe 13 Mei 2026 imekumbusha tukio la Jumatano ya miaka 45 iliyopita,  wakati wa Katekesi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa juu ya Kigari chake cheupe akisalimia waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja huo,  alitelemka kwanza na kutembea ili kutoa heshima sehemu ya tukio la jaribio la kuuawa kwa mtangulizi wake, Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili kunako tarehe 13 Mei 1981.

Papa alitelemka kwenye kwenye eno la  jaribio
Papa alitelemka kwenye kwenye eno la jaribio   (@Vatican Media)

Katika eneo hilo, lililowekwa bamba la marumaru nyeupe hatua chache kutoka Mlango wa Shaba, Papa Leo XIV, aliweza simama mara baada ya kufika hapo na kusali kwa muda mfupi kimya kimya, akapiga magoti na kugusa nembo ya Karol Józef Wojtyła. Picha ya mfano katika kumbukumbu ya tukio hilo ambalo, zaidi ya miongo minne iliyopita, lilishangaza ulimwengu mzima, ambao ulikusanyika katika maombi kwa ajili ya kupona haraka kwa Papa huyo Mtakatifu.

Baba Mtakatifu akiwaelekea mahujaji wa kutoka Tanzania mara baada ya Katekesi
Baba Mtakatifu akiwaelekea mahujaji wa kutoka Tanzania mara baada ya Katekesi   (@Vatican Media)

Katika salamu kwa lugha ya Kiingereza mara baada ya Katekesi, pamoja na salamu kwa  wanaozungumza kiingereza kutoka: Uingereza, Ireland, Tanzania, India, Indonesia, Canada Marekani, Papa alisema: “Leo tunakumbuka ukumbusho wa Mama Yetu wa Fatima. Katika siku hii, miaka arobaini na tano iliyopita, jaribio lilifanywa dhidi ya maisha ya Papa Yohane Paulo II na kwa sababu hizo katekesi yangu leo ilikuwa ni kwa ajili ya  Bikira Maria Mwenyeheri. Wakati huo huo, hivi karibuni tutasherehekea Kupaa kwa Bwana, ambapo kunaashiria kuingia kwa ubinadamu wake mbinguni. Tunaposubiri kuja kwa Yesu mara ya pili katika utukufu, na tujikabidhi kwa Bikira Mwenyehri kama Mitume.” Na zaidi Papa alimkabidhi Kilio cha watu waliokumbwa na vita."

Mahujaji kutoka Tanzania
Mahujaji kutoka Tanzania   (@Vatican Media)

Tukabidhi Kilio cha amani kwa Mama kutoka kila seemu ya dunia

Baba Mtakatifu Leo XIV aidha akizungumza na mahujaji wanaozungumza Kireno alisema: "Leo, sikukuu ya kiliturujia ya Bikira Maria wa Fatima, tunaelekeza macho yetu kwenye mahali  Patakatifu, ambapo Mama Yetu alitoa ujumbe wa amani kwa wachungaji wadogo watatu. Katika mahali hapo, penye upendo mkubwa kwa Ukristo, mahujaji wengi kutoka mabara matano wanakusanyika leo: uwepo wao ni ishara ya hitaji la faraja, umoja, na matumaini ya watu wa wakati wetu. Tukabidhi kwa Moyo Safi wa Maria kilio cha amani na maelewano kinachoibuka kutoka kila sehemu ya dunia, hasa kutoka kwa watu wanaosumbuliwa na vita. Baraka zangu kwa wote!"

Mahujaji kutoka Pande mbali mbali za dunia
Mahujaji kutoka Pande mbali mbali za dunia   (@Vatican Media)

Kwa upande wa wanaouzungumza kiarabu Papa alisema: "Tupyaishe "ndiyo" yetu kwa Bwana na mapenzi yake, tukimtumaini, kama Maria, ambaye atatupatia uzima mpya. Bwana awabariki nyote na awalinde daima kutokana na maovu yote."

Katekesi ya Papa na siku kuu ya Mama Maria wa Fatima

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

13 Mei 2026, 13:12