Kardinali Emil-Paul Tscherrig. Kardinali Emil-Paul Tscherrig. 

Papa Leo XIV anamkumbuka Kardinali Tscherrig na upendo wake mkubwa kwa Kanisa

Papa Leo XIV ametuma salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Kardinali Paul Emil Tscherrig, ambaye amefariki Jumanne Mei 12 akiwa na umri wa miaka 79,akielezea shukrani kwa huduma yake ya uaminifu kama mwakilishi wa Papa katika nchi mbalimbali na baadaye kama mjumbe wa Mabaraza kadhaa ya Kiti Kitakatifu na kumwita"mhudumu wa Injili aliyependa Kanisa."

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa salamu za "rambirambi zake za dhati" baada ya kupata habari za kifo cha Kardinali Paul Emil Tscherrig, wa Uswiss aliyewahi kuwa Balozi wa Vatican nchini Italia na Jamhuri ya San Marino, ambaye amefariki Jumanne tarehe 12 Mei 2026, akiwa na umri wa miaka 79. Katika telegramu, Papa aliwasilisha mawazo yake kwa familia ya Kardinali na kwa Jumuiya ya Jimbo la Sayuni, ambapo Kardinali Tscherrig alibatizwa, na akakumbuka kwa shukrani "utumishi wake wa uaminifu kama mwakilishi wa Papa katika nchi mbalimbali na baadaye kama mjumbe wa mabaraza kadhaa ya Kiti Kitakatifu."

Baba Mtakatifu alikumbuka kwamba Kardinali "alitenda kwa ukarimu" na "alishuhudia upendo kwa Kanisa na kwa Mrithi wa Petro." Hatimaye, Papa Leo  XIV alihitimisha ujumbe huo kwa kukabidhi roho "ya mhudumu huyu wa Injili" kwa Mungu, ili aweze "kumkaribisha katika nuru isiyojua machweo," na kuomba maombezi ya Bikira Maria, huku akituma baraka za kitume kwa wote waliokumbwa "na msiba huu wa ghafla."

Muda Mrefu katika balozi za Vatican

Kardinali Paul Emil Tscherrig alizaliwa Unterems, Uswiss, mnamo tarehe 3 Februari 1947. Alipewa daraja la Upadre mwaka 1974 na baadaye akapata shahada ya uzamivu katika sheria. Papa Yohane Paulo II,  alimteua katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican mwaka 1978 kama Katibu wa Ubalozi wa Vatican, akihudumu Uganda, Korea Kusini, Mongolia, na Bangladesh. Mwaka 1996, aliteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Burundi, na Askofu Mkuu wa Kanisa la Voli. Aliwekwa wakfu wa kiaskofu na Katibu Mkuu wa Vatican wa wakati huo, Kardinali Angelo Sodano mnamo Juni 27 mwaka huo. Utumishi wake katika Ubalozi,  kisha ukampelekea kuteuliwa kuwa Balozi wa  Vatican huko Trinidad na Tobago, Jamhuri ya Dominika, Jamaica, Grenada, Guyana, Mtakatifu Lucia, Mtakatifu Vincent na Grenadines, na Bahamas mwaka 2000.

Kuanzia 2001, pia alihudumu Barbados, Antigua na Barbuda, Suriname, na Mtakatifu Kitts na Nevis. Mwaka 2004, alichukua nafasi ya ubalozi huko Korea Kusini na Mongolia, ikifuatiwa na kazi katika nchi za Kaskazini na kisha Argentina, na hatimaye, hadi 2024, alihudumu kama Balozi wa Vatican nchini Italia na San Marino, wa kwanza asiye Mtaliano kushikilia wadhifa huo. Papa Francisko alimteua kuwa Kardinali katika katika Mkutano Mkuu wa Makardinali kunako tarehe 30 Septemba  2023.

Papa atuma rambi rambi

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

12 Mei 2026, 16:36