Papa Leo XIV:Kard Tscherrig alijitolea kama mwanadiplomasia na zaidi kama mchungaji wa Kanisa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, Ijumaa alasiri tarehe 15 Mei 2026, aliongoza misa ya mazishi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Kardinali Paul Emil Tscherrig, wa Uswisi ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 79 mnamo tarehe 12 Mei 2026. Katika mahubiri yake Papa alimfafanua kama Kardinali, “kaka, mwanadiplomasia, mchungaji, ambaye alihudumia Kanisa la ulimwengu kwa kazi ambayo mara nyingi haikuwa ya kuvutia, lakini hata hivyo ilikuwa ya bidii na yenye kuhitaji juhudi.” Papa alifamfafanua Kardinali mpendwa ambaye, miongoni mwa majukumu yake mbalimbali, aliongoza Ubalozi wa Vatican nchini Italia na San Marino kuanzia 2017 hadi 2024, wa kwanza asiye Mwtaliano kushika wadhifa huo. Aliundwa kuwa Kardinali na Papa Francisko katika Baraza Kuu la Makardinali la tarehe 30 Septemba 2023, mwaka huo huo pamoja na Robert Francis Prevost aliyepokea ukardinali.
Kumtumikia Bwana wa ukarimu
Na kwa hiyo Papa Leo XIV ali msindikiza kwamba: "Kaka huyu katika mkutano mkuu na mzito na Bwana ambaye alimtumikia kwa ukarimu, pamoja na Rafiki ambaye alitembea kando yake kwa uaminifu katika maisha yake yote, zaidi ya nusu yake alitumika katika huduma ya Kiti cha Ubalozi wa Vatican kwa Uwakilishi mbalimbali wa Kipapa na katika Sekretarieti ya Vatican." Papa Leo katika mahubiri hayo alimweleza alivyokuwa mvumilivu na kijikana kuwa: "Kujitolea kwake kama mwanadiplomasia, na zaidi kama mchungaji wa Kanisa," kumemwona ndugu yetu huyu akifanya kazi kwa miaka mingi, kwa uvumilivu na kutokuwa na ubinafsi, kukusanya watu waliokabidhiwa utunzaji wake kwa utii, hata kukabiliana na vikwazo na changamoto ambazo mwakilishi wa papa anaitwa kukumbatia kwa manufaa ya wote."
Uzoefu wa kidiplomasia katika nchi mbali mbali
Papa Leo XIV alikumbuka tena uzoefu mkubwa wa kikanisa na kimataifa wa Kardinali Tscherrig huko Burundi, Trinidad na Tobago, na mataifa kadhaa ya Caribbean, Korea Kusini, Mongolia, na baadaye Sweden, Denmark, Finland, Iceland, Norway, na Argentina, hatimaye akawasilisha Italia na San Marino. "Uzoefu mkubwa wa kikanisa na kimataifa, unaoshuhudia upatikanaji wake na uwezo wake wa kubadilika, katika upendo wake kama Mchungaji, katika mazingira tofauti sana: maeneo na watu aliotumwa, kwa niaba ya Baba Mtakatifu, kuunganisha uhusiano wa ushirika kati ya Makanisa mahalia na Kiti Kitakatifu, pamoja na kuimarisha vifungo vya urafiki." Baba Mtakatifu aliendelea kuwa: “Sasa Kardinali Paul Emil anakutana na Bwana wake na tunamsindikiza katika kifo hiki cha ajabu” huku akitumaini kwamba, “wakati huu unaweza kuwa fursa ya kutafakari na kutia moyo, kuthamini wema alioutoa, kwa neema ya Mungu, kwa imani na kujitolea. Dunia Yetu inahitaji wahudumu wa Bwana wa kuitikia wito wake.
Kufanya matumaini yasitawi na matarajio mema ya watu
Katika mahubiri yake Papa Leo XIV alinukuu hotuba ambayo Papa Francisko alikutana na Tscherrig huko Buenos Aires na ambaye aliwahimiza wanadiplomasia "kufanya matumaini yastawi karibu nao, kama jibu la hamu na matarajio mema ya watu. "Ni mwaliko, ambao sisi pia tunaweza kuukubali leo hii kuutekeleza popote tunapoitwa kuwatumikia na kuwapenda kaka na dada zetu. Dunia yetu inahitaji sana wajumbe ambao wanaweza kuisaidia kupata tena uaminifu, na ushuhuda mzuri wa wale ambao Mungu amewachagua kama wahudumu wake unaweza kutusaidia katika kuitikia wito huu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
