Papa Leo XIV kwa Maonyesho ya Vitabu,Torino:Utamaduni ujenge mazungumzo na maelewano
Vatican News
"Kuna mahitaji ya fasihi inayosaidia kutambua tena hadhi ya kila mtu, hasa walio hatarini zaidi, na ambayo inazidi kuwa shule ya udugu na amani." Hili ndilo tumaini la Papa Leo XIV katika ujumbe uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ambao ulielekezwa kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Torino nchini Italia, Kardinali Roberto Repole katika fursa ya uzinduzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu, yanayofanyika huko Torino, Mji Mkuu wa Mkoa wa Piemonte kuanzia Mei 14 hadi 18.
"Ulimwengu uliookolewa na Watoto"
Salamu hiyo ilisomwa asubuhi ya Alhamisi tarehe 14 Mei 2026 na mkurugenzi wa Maonyesho hayo, Annalena Benini, wakati wa hafla ya ufunguzi wa tukio hilo, ambalo mada yake mwaka huu 2025 imechukuliwa katika kazi ya mwandishi Elsa Morante isemayo: "Ulimwengu Uliookolewa na Watoto." Papa alielezea mada iliyochaguliwa kwa toleo la mwaka huu kama "muhimu sana na la wakati unaofaa." "Katika wakati unaoonekana kufunikwa na hofu ya vita," Papa aliongeza, "na baridi ya kutojali, watoto, wenye uwezo wao wa asili wa kutazama ulimwengu kwa macho mapya, wanawasha mwanga wa matumaini katika jamii."
Kuhamasisha uelewa mpya wa umujimi wa kujenga mazungumzo
Kwa kutuma baraka zake, Papa Leo XIV alielezea matumaini "kwamba tukio hilo litahamasisha uelewa mpya wa umuhimu wa utamaduni katika kujenga mazungumzo na maelewano." Maneno ya ujumbe huo yalirudia yale ambayo alisema hivi karibuni Papa wakati wa kukutana na wafanyakazi katika hafla ya maadhimisho ya miaka mia moja ya Jumba la Uchapishaji la Vatican(LEV), ambalo pia linashiriki likiwa na kibanda na matukio mbalimbali.
Kusoma ni kulisha akili
Mnamo tarehe 7 Mei 2026, Papa Leo XIV alikuwa amekumbusha kwamba: "kusoma ni kulisha akili, husaidia kukuza hisia ya ukosoaji iliyo wazi na iliyojengeka vizuri, na husaidia kujilinda dhidi ya misimiamo mikali na njia za mkato za kiitikadi." Na alikuwa amewahimiza: "kila mtu kusoma vitabu, kama dawa dhidi ya mawazo yaliyofungwa, ambayo yanaoneshwa katika mitazamo migumu na maoni yanayopunguza uhalisia."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
