2026.05.30 Papa alikutana na Jumuiya ya Villa Nazareth 2026.05.30 Papa alikutana na Jumuiya ya Villa Nazareth  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa Villa Nazareth:Kwa amani ya kudumu,wafundisheni vijana kutenda mema!

Baba Mtakatifu ameikaribisha jumuiya ya Villa Nzareth,mjini Vatican,Jumamosi Mei 30 ambapo katika hotuba yake alihimiza wanachama wake kuendelea kutoa msaada wa kiakili,kimaadili na kifedha kwa vijana ambao wanahitaji nuru na mwongozo hasa ili kufikia umoja kati ya akili na roho,kati ya imani,masomo,taaluma na maisha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na jumuiya ya Villa Nazareth tarehe 30 Mei 2026 katika Ukumbi wa Mikutano Mikuu mjini Vatican ambayo ni taasisi ya elimu iliyoanzishwa miaka 80 iliyopita wakati wa kukaribia kwa vita vya Pili vya Dunia na Kardinali  Domenico Tardini.  Kisha kama Katibu Mkuu wa Vatican, ilikuwa kama maabara ya matumaini katika eneo ambalo wakati huo lilikuwa eneo jipya la mijini la Roma ambapo, Villa Nazareth ilihamasisha mazungumzo muhimu kati ya imani, utamaduni, na upendo, hasa kwa manufaa ya vijana walio katika hali ngumu zaidi. Papa Leo XIV katika hotuba yake alikumbuka asili ya Villa Nazareth, iliyoanzishwa ili kutoa fursa za kielimu kwa wale "wenye talanta nyingi na nia njema, lakini hawana njia muhimu za kufuata kozi ya masomo."

Ili kukuza amani wafundisheni vijana kama viongozi wa kutenda mema

Akialika Jumuiya kukumbuka daima alama za kiinjili za "Kuoshwa kwa Miguu" na "Msamaria Mwema," vipindi ambavyo vinaweza kupata msukumo kila mara, Baba Mtakatifu alisisitiza mtazamo wa Tardini kwamba: Mwanzilishi alielewa kwamba, ili kukuza amani ya kudumu, ilikuwa ni lazima kuwafunza vijana kama viongozi katika kutenda mema, kuwapa zana za kutosha kuishi maadili ya Injili katika familia zao, katika masomo, katika burudani, na katika utendaji wao wa kitaaluma. Papa anataja waraka wake wa hivi karibuni wa Magnifica Humanitas"Kinachookoa ubinadamu si kujitosheleza zaidi, bali ni uhusiano unaokomboa, ushirika unaobadilisha", na anasisitiza hitaji la kujenga sio Mnara mwingine wa Babeli, bali Jiji la Mungu, ambapo upendo na udugu wa ulimwengu wote hushikilia msimamo wake.

Jumuiya ya Villa Nazareth
Jumuiya ya Villa Nazareth   (@Vatican Media)

Kuimarisha, kukua na kueneza utamaduni

Hata hivyo, kutokana na haya yote, Papa  Leo XIV alisema "ningependa kukumbuka na kuhimiza kipengele kimoja cha mwisho cha kazi yenu nia ya kuifanya Villa Nazareth kuwa kitovu cha mawazo ya Kikristo, ambapo muunganiko wa juhudi za kiakili, kimaadili, na kiuchumi za wanaume na wanawake kutoka vizazi na matabaka tofauti ya maisha huchangia katika kuimarisha, kukua, na kueneza utamaduni unaozidi kuangazwa na mafundisho ya Injili.

Msiwe wafungwa wa kiburi na mawazo ya kutawala

Hatimaye Baba Mtakatifu anapitia kile ambacho watangulizi wake, Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili na Benedikto wa kumi na sita, waliwaambia wanachama wa Villa Nazareth, na akakumbuka mafundisho yao: wasiwe wafungwa wa kiburi na mawazo ya kutawala, bali wajihusishe kila wakati katika mazungumzo. Maelekezo ya kufuata hata katika wakati wetu: Miito hii ni halali zaidi kuliko wakati mwingine wowote leo, wakati ambapo vijana wana fursa nzuri na njia za maarifa na ukuaji, lakini pia wanahitaji sana mwanga na mwongozo, hasa ili kuunda umoja kati ya akili na roho, kati ya imani, masomo, taaluma, na maisha.

Papa akutana na Jumuiya ya Villa Nazareth
Papa akutana na Jumuiya ya Villa Nazareth   (@Vatican Media)

Kumbukumbu na misa

Ili kuadhimisha kumbukumbu yake mnamo Mei 30, Jumuiya ilisherehekea Misa iliyoongozwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican na kufuatiwa na Mkutano na  pamoja na Papa katika Ukumbi wa Mikutano Mikuu. Waalimu, wanafunzi, wanachama, wahitimu, marafiki, na wasaidizi wa kiroho walikusanyika ili kuimarishwa katika utume wao ambao ni muhimu zaidi kuliko hapo awali katika ulimwengu wa leo. Katika tukio la Villa Nazareth, utume huu umesababisha kuhitimu kwa zaidi ya wanafunzi 1,300.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

30 Mei 2026, 17:50