2026.05.25 Uwakilishi wa Chama cha Klub ya wapanda Farasi wa Barcellona 2026.05.25 Uwakilishi wa Chama cha Klub ya wapanda Farasi wa Barcellona  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Mkristo si mfadhili rahisi ni mtu mwenye huruma

Baba Mtakatifu Leo XIV, Mei 25 alikutana na wanachama wa Klabu ya Wapanda Farasi wa Barcelona,Hispania wanaojishughulisha na kazi za upendo ambapo aliwalika wamkazie macho Kristo kwa sababu ni katika walio hatarini zaidi ndipo uwepo wake unapatikana na kwamba Mkristo si mfadhili tu bali ni mtu anayetafuta mema ya wengine.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatatu tarehe 25 Mei 2026 alikutana na wanachama wa“Círculo Ecuestre’ yaani Klabu ya Wapanda Farasi wa Barcelona nchini Hispania. Akianza Hotuba yake, kama kawaida alianza na ishara ya Msalaba na kuwatakia amani wote. Aliwakaribisha ambao wamesindikizwa na Kardinali Juan José Omella Omella wa Jimbo Kuu la Barcelona ambao walipendelea kukutana na Mfuasi wa Mtume Petro katika fursa ya maadhimisho ya kuanzishwa kwa mfuko wa chama chao. Aliwashukuru kwa ishara ya ukaribu huo.

Klub ya wapanda Farasi
Klub ya wapanda Farasi   (@VATICAN MEDIA)

Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea alisema kuwa “Kila mwamini katika Kristo ameitwa kuweka uhai wake wazi kwa matendo ya Roho Mtakatifu, akiwa na mtazamo wa utayari usiochoka wa kuishi upendo wa Kikristo, fadhila ya kitaalimungu ambayo kwayo tunampenda Mungu kuliko vitu vyote na wengine kama sisi wenyewe, hasa kutokana na upendo kwa Mungu. Kwa njia hiyo mwamini Mkristo Ndiyo, kwa hivyo si mfadhili rahisi, bali ni mtu mwenye huruma, anayependa bila ubinafsi na anayetafuta kwa bidii ustawi kamili wa wengine.

Kujitoa kwao kumtumikia Mungu na wengine

Kupitia kujitolea kwao binafsi kumtumikia Mungu na wengine, wakiwa tayari kuwasindikiza kwa uvumilivu na huruma, Papa alisema kuwa awapatie ukuaji katika upendo wake na awabariki sana wao na wapendwa wao. Kwa kuhitimisha Papa aliwaba Baraka akisema “Na baraka ya Mwenyezi Mungu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ishuke juu yenu na ibaki nanyi daima.”

Papa na Klabu ya Barcelona

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

25 Mei 2026, 11:36