Papa Leo XIV:"Tusali kwa Roho atuokoe na ubaya wa vita,si kwa nguvu kubwa,bali kwa nguvu ya upendo!

“Kwa moyo unaowaka tusali leo hii kwamba Roho Mfufuka atuokoe na ubaya wa vita na ushindwe si kwa nguvu kubwa,bali kwa Mwenye nguvu ya upendo.Tuombe ili aokoe ubinadamu na taabu ambayo hukombolewa,si kwa utajiri usiohesabika,bali kwa zawadi isiyoisha.”Ni katika mahubiri ya Papa katika Sherehe za Pentekoste katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican,Dominika tarehe 24 Mei 2026."Shukrani kwa Roho Mtakatifu,tunaweza kupeleka kwa wote amani ya kweli,inayookoa."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu aliongoza ibada ya misa takatifu katika Sherehe ya Pentekoste, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, lililojaa waamini elfu tano, Dominika tarehe 24 Mei 2026. Katika mhububiri yake, Papa alianza kusema kuwa kipindi baada ya Pasaka, leo hii inatufikia sherehe ya Pentekoste, utimilifu wake. Ili kuonesha umoja wa Kanisa wa tukio hilo la wokovu, Injili inatupeleka kwa upya  katika siku ya kwanza ya Juma (Yh 20,19), yaani,  siku ile mpya ambayo Yesu Mfufuka aliwatokea mitume  kwa  kuwaonesha  “ mikono na ubavu.” Bwana anajionesha mwili wake mtukufu kwa usahihi madonda yake, majeraha ya kusulibiwa.  Ishara hizi za mateso, kwa ufasaha zaidi  wa  hotuba yoyote ile, zimebadilishwa katika “Yule aliyekuwa amekufa anaishi milele.

Sherehe za Pentekoste
Sherehe za Pentekoste   (@Vatican Media)

Mitume walikuwa wamzishwa katika chumba cha karamu kuu

Kwa kuona Bwana, hata mitume walirudi kuishi tena: walikuwa wamezikwa katika chumba cha Karamu kuu, huku wamejawa hofu, lakini Yesu aliingia licha ya milango kufungwa na akawajaza furaha. Yeye anapita, kupitia kifo chetu, anafungua kaburi na kuweka wazi mahali ambapo hatukuwa na njia yetu ya kutokea. Kwa ishara yake, Kristo anaunganisha neno: “Amani iwe kwenu (Yh 20,19); na kwa haraka baadaye analivuvua mitume Roho Mtakatifu. Mfufuka amejaa maisha: baada ya kuwaonesha mwili ule kama mtu kweli, anawapatia ule wa Mungu, kama Mwana mpendwa wa Baba, aliyefanywa kuwa kaka,  kwa ajili yetu na Mkombozi. Na wakati huo huo katika Karamu Kuu mahali alipoanzisha agano jipya na milele, Yesu anavuvia Roho:  mahali pa karamu na kusalitiwa pamebadilika, kutoka kaburi la Mitume, na kugeuka kuwa kwa ajili ya Kanisa lote tumbo la ufufuko. Kwa Pentekoste ni sikukuu ya kipasaka na sikukuu ya mwili wa Kristo ambaye kwa neema yake  ni sisi. Kwa kusheherekea fumbo hili, Papa Leo XIV alipenda kusiama na kutafakari mantiki tatu.

Papa aliongoza Misa ya pentekoste
Papa aliongoza Misa ya pentekoste   (@Vatican Media)

Roho Mfufuka ni Roho wa amani

Awali ya yote, Roho wa Mfufuka ni Roho wa amani. Kiukweli katika Pasaka yake Kristo anafanya amani kati ya Mungu na ubinadamu, na Roho Mtakatifu anaingia katika mioyo na kuenea katika Ulimwengu. Amani hii inakuja kutoka katika msamaha na kutupeleka katika msamaha: Inaanza na msamaha uliotolewa na Yesu mwenyewe ambaye alisalitiwa na sisi, akahukumiwa na kusulibiwa. Kwa kutushangaza, kwa upendo wake, Yeye hasa, mfufuka, anasema “ Wowote mtakaowaondolea dhambi , wameondolewa ; na wowote mtakaowafungia dhambi wamefunguliwa (Yh 20,23.)”

Kwa maneno haya, Yesu anatukabidhi kazi ya kimungu, kwa sababu ni  Mungu tu anaweza kusamehe dhambi (Mk 2,7).  Mamlaka hayo yamepewa katika ishara ya upatanisho wa ulimwengu: Bwana anaeneza Roho ya amani kutoka juu hadi sehemu ya historia, kwa sababu hasimsahahu yoyote  Yule aliwakomboa wote kutokana na kifo. Roho Mtakatifu, kiukweli ni Bwana na anatoa uzima tangu mwanzo wa uumbaji, wakati alipokuwa akielea juu ya maji (Mw 1,2) na sasa, kwa ukombozi wake, anabadilisha historia ya dunia: Pentekoste kweli inatimizwa kama sikukuu ya Agano jipya, yaani kutoka agano kati ya Mungu na watu wote wa dunia.

Kunyunyiziwa maji
Kunyunyiziwa maji   (@Vatican Media)

Sheria ni gombo la amani

Wakati uvumi kutoka mbinguni, upepo na ndimi za moto katika karamu kuu, zinakumbusha ishara za zamani za Sinai (Mdo 2,2-3; Kut 19, 16-19), sheria takatifu ya Mungu inakuja kuandikwa katika mioyo, iliyowekwa na Roho kwa tabia ya upendo katika mwili wa Kristo na katika moyo wake ambao ni Kanisa. Sheria hii ni gombo la amani: ni amri mara mbili ya upendo, ambayo Roho Mtakatifu anatukumbusha kwa kila pigo la moyo. Kwa moyo wetu, tunaweza kwa hiyo kuomba: Veni Sancte Spiritus”, yaani “Njoo Roho Mtakatifu” kwa sababu Yeye alijitoa kwetu tayari. Tunaweza kuitamani, kwa sababu tayari tuliahidiwa. Tunaweza kuipokea, kwa sababu Yeye mwenyewe ni mgeni mtamu wa roho.

Wakati wa kupokea vipaji
Wakati wa kupokea vipaji   (@Vatican Media)

Roho ya Mfufuka ni Roho ya Utume

Mantiki ya pili, Papa Leo XIV alidadavua kuwa:Roho ya Mfufuka ni Roho wa utume: “Kama Baba alivyonituma” anasema Bwana “Hata mimi ninawatuma ninyi”(Yh 20,21). Tunahusishwa hivyo katika utume wa Yesu:  huo wa Yule ambye anatoka kwa Mungu na kwa Mungu unarudi kwa nguvu ya Roho, ambaye anatutangulia kwa Baba na kwa Mwana na kwake ameabudiwa na kutukuzwa, Mungu mmoja. Roho Mtakatifu ni upendo hai wa Kristo ambaye…., anatusaidia katika utume (1Kor 5,14). Wakati anawapatia Mitume uwezo wa kujieleza katika lugha mbali mbali (Mdo 2,4) na Roho hiyo hiyo anafundisha ubinadamu,  Neno la wokovu. Sasa ambapo Mitume wamepokea pulizo la Mfufuka ndani mwao, tangazo hilo linakuja kutoka katika modomo yao, lina sauti ya Petro na wale waliokuwa naye. Ni hasa katika siku ya Pentekoste, mitume walianza kutangaza Yesu msulibiwa na mfufuka: “Matendo makuu ya  Mungu”(Mdo 2,11) yanafafanua ukombozi wote, ambao unaanza na imani.

Njoo Roho Mtakatifu
Njoo Roho Mtakatifu   (@Vatican Media)

Kiukweli, kazi ya kwanza ya Roho Mtakatifu katika sisi ni imani ambayo tunasadiki: “Yesu ni Bwana.” (1Kor 12,3). Imani hii inaishi na inajieleza kwa kila tendo jema, kwa kila kazi ya huduma na ya fadhila. Matendo ya  Mungu, kwa hiyo, ni sisi, ambao tumekuja hapa leo hii kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu, kwa kualikwa katika karamu ya Bwana, kwa kuungana katika kusikiliza maneno yake na kutumwa kumshuhudia kila mahali. Baba Makatifu Leo XIV  aliendelea kusema, “sisi ni washiriki wa Injili: Kanisa lote ni kiongozi mkuu, na siyo mlinzi mtu. Kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, tangazo letu linajazwa na furaha na la matumaini, kwa sababu, sisi wenyewe  ni habari ya ulimwengu, mwanga na chumvi ya dunia(Mt 5,13-14). Kwa hakika si kwa mastahili yetu, wala kwa upendeleo, bali kwa ajili ya neno la Bwana, ambaye anatakatifuza dhambi, anatibu mkoma, anamfanya yule aliyemsaliti kuwa mtume.

Upokee Bwana sala zetu na mapaji yetu
Upokee Bwana sala zetu na mapaji yetu   (@Vatican Media)

Tunaona vizuri kuna mabadilijo yasiyopyaisha ulimwengu bali kuzeesha na makosa na vurugu

Kwa upande mmoja, tunaona vizuri, kuna mabadiliko ambayo hayapyaishi Ulimwengu, bali yanazeesha kati ya makosa na vurugu. Kwa upande mwingine, kinyume chake, Roho Mtakatifu anaangaza akili na kuchochea katika mioyo nguvu mpya ya maisha. Ndivyo inavyobadili historia kwa kufungulia wokovu, yaani zawadi ambayo Bwana pekee anashirikisha na wote. Utume wa Kanisa unathibitishwa ushirikishaji huo kwa kuubadilili ulimwengu uliokanganyikiwa katika umoja na Mungu na kati yetu. Utume huu unaanza kwa kusema ukweli wa Mungu na wa binadamu, kwa sababu Roho wa Mfufuka ni “ Roho wa Ukweli (Yh 14,17). Bwana mwenyewe alituahidi, akiomba umoja kwa ajili ya Kanisa lake, umoja uliojengwa juu ya upendo wa Mungu, kisima cha upendo wetu. Roho ambaye alizungumza kwa njia ya manabii, anahamasisha daima umoja katika ukweli, kwa sababu anaweka ndani mwetu uelewa, maelewano na ukweli thabiti wa maisha. Kama anavyofundisha mtakatifu Agostino: “Roho Mtakatifu anataka kuwa hii, iwe ishara ya uwepo wake (Hotuba 269,1): zawadi ya lugha ambayo wanaelewa katika imani moja. Mlinzi,  anatulinda kwa hiyo na kile ambacho kinaleta kizingiti cha maelewano haya: kutoka upendeleo, kutoka unafiki, na kutoka katika mitindo ambayo inazima mwanga wa Injili. Ukweli ambao Mungu anatupatia unabaki namna hii ya neno la uhuru kwa watu wote, ujumbe ambao unabadilisha kutoka ndani ya kila utamaduni.

Basilika ya Mtakatifu Petro
Basilika ya Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Roho Mfufuka hamwagiki mara moja badala yake anakuwa kila wakati

Roho wa Mfufuka kwa hakika hamwagiki mara moja, na kisha basi, badala yake anakuja kila wakati. Kama Ekaristi ilivyo uwepo wake hai wa Kristo, ambaye anatumwilisha, ndivyo hivyo Roho Mtakatifu anavyoweka chapa ndani mwetu tabia yake katika Ubatizo, unaotufanya Wakristo; katika Kipaimara ambacho kinatufanya kuwa mashuhuda, katika wakfu wa Daraja, ambalo linafanya huduma na wachungaji kwa ajili ya watu. Kila sakramenti Yeye ni dator munerum yaani, mtoaji wa zawadi, kisima cha Utakatifu ambacho kinazidisha zawadi  na karama katika sala, katika matendo ya huruma, katika mafunzo ya Neno la Mungu. Kama anavyofundisha Mtume “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa ajili ya wema wa pamoja” (1Kor 12,7) Ni katika muktadha huo kwa hiyo sisi ni Kanisa, la mwili mmoja ambao anaishi Mungu na uhudumia Ulimwengu. Shukrani kwa Roho Mtakatifu, tunaweza kupeleka kwa wote amani ya kweli, ukweli unaookoa, yaani Kristo Bwana mwenyewe.

Baraka ya Mungu mwenyezi
Baraka ya Mungu mwenyezi   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV  alisema kwa moyo unaowaka tusali leo hii kwamba Roho Mfufuka atuokoew na ubaya wa vita, na ushindwe si  kwa  nguvu kubwa,  bali kwa Mwenye nguvu ya upendo. Tuombe ili aokoe ubinadamu na taabu ambayo hukombolewa,  si kwa utajiri usiohesabika, bali kwa zawadi isiyoisha. Papa alihitimisha akisema tumuombe ili  atuponeshe na donda la dhambi, kwa ajili ya wokovu uliotangazwa kwa watu wote katika jina la Yesu. Hii ni neema ambayo inaweka ujasiri Mitume: Iingine hata kweli leo hii na daima kwa maombezi ya Maria Mama wa Kanisa.

MAHUBIRI YA PAPA PENTEKOSTE

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

24 Mei 2026, 11:30