206.05.28 WASHIRIKI WA MKUTANO MKUU WA UINJILISHAJI 206.05.28 WASHIRIKI WA MKUTANO MKUU WA UINJILISHAJI   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Ulimwengu una kiu zaidi ya hapo awali ya tumaini

Uinjilishaji lazima uendelee kuwa motisha ya msingi kwa kila kitendo cha Kanisa la ulimwengu na jumuiya za watu mahalia; ni kwa njia hiyo tu imani yenyewe inaweza kupatikana tena katika uzuri wake wote na kuonesha uaminifu wake vyema.Kutangazwa kwa Injili,ambayo huleta matumaini,si pendekezo la ndoto:ni ushuhuda unaovutia kwa sababu unaonesha wito wa upendo na ukweli.Alisema hayo Papa Leo XIV katika Hotuba kwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji,Kitengo cha Uinjilishaji.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alahamisi tarehe 28 Mei 2026 alikutana na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, Ktengo cha Masuala Msingi ya Uinjilishaji Ulimwenguni. Akianza hotuba yake alionesha yake kukutana nao wakiwa mwisho  mwa Mkutano wao mkuu. Kwa njia hiyo tukio hilo limempatia fursa ya kushirikishana mambo kadhaa kuhusu maisha ya Kanisa, hasa kwa miaka ijayo. Hata hivyo, kwanza kabisa, Papa Leo XIV alipenda kutoa shukrani zake za dhati kwa kazi kubwa iliyofanywa na Baraza la Kipapa wakati wa Jubilei ya mwaka jana(2025). Tulipata wakati wa neema ulioshuhudia mamilioni ya mahujaji wakimiminika Roma. Baba Mtakatifu aliuliza, jumla ya mwisho ilikuwa na mahujaji wangapi akajibiwa kuwa zaidi ya milioni 33 “Tukio hili lilihitaji juhudi kubwa ya shirika, ambayo ilijidhihirisha katika ukaribisho wa furaha katika nyanja mbalimbali na, zaidi ya yote, katika umakini wa mwelekeo wa kiroho, ikiakisi wingi wa zawadi ambazo Bwana amewamiminia waamini.

Hatima ya Mlango Mtakatifu kati ya Basilika Nne ya Kipapa

Hatima ya Mlango Mtakatifu wa moja ya Basilika nne za Kipapa  haukuzuia Mwaka Mtakatifu kutazamwa kwa kina katika Makanisa mahalia. Ulimwenguni kote tumaini limekuwa mhusika mkuu wa maisha ya Kikristo. Msisitizo unaowekwa kwa "dada mdogo," ambaye, karibu haonekani, huwavuta chini wazee wawili, imani na upendo, anahitaji kutangazwa na kuishi kwa nguvu na usadikisho. Ulimwengu una kiu zaidi ya hapo awali ya tumaini. Unatamani kuishi kwa amani na kwa uhakika kwamba kujitolea kujenga mji unaostahili watoto wa Mungu si tu kwamba kunawezekana bali pia ni kweli, kwa sababu kumejaa tumaini linalotoa malengo ya kweli, si ya uwongo. Kwa hivyo, tusiache tangazo hili, linaloungwa mkono na ahadi ya Bwana Yesu ya kubaki nasi siku zote; linaonekana katika ushuhuda tunaoitwa kutoa ili kuwa wanafunzi waaminifu wa neno lake. (cfr Mt 28,18-20).

Uinjilishaji unataka kuendlea kuwa sababu ya matendo msingi ya Kanisa la Ulimwengu

Uinjilishaji lazima uendelee kuwa motisha wa msingi kwa kila kitendo cha Kanisa la ulimwengu na jumuiya za watu mahalia; ni kwa njia hiyo tu imani yenyewe inaweza kupatikana tena katika uzuri wake wote na kuonesha uaminifu wake vyema. Kutangazwa kwa Injili, ambayo huleta matumaini, si pendekezo la ndoto: ni ushuhuda unaovutia kwa sababu unaonesha wito wa upendo na ukweli. Hatuwezi kupuuza ukweli kwamba, hasa katika nchi za Magharibi, mgogoro wa imani, pamoja na mambo mengine ya kijamii na kiutamaduni, umesababisha kutojali kwa kidini kote. Imani, kwa wengi, haionekani tena kuwa muhimu kwa maisha yao.

Hatari ya msingi, ambayo haionekani kila wakati katika uzito wake, ni kwamba pumzi ya kile ambacho ni binadamu kweli—yaani, utafutaji wa maana—itapotea. Maswali makubwa ya kuwepo bado hayajajibiwa, huku utamaduni wa kiteknolojia ambao unapaswa kujibu kila hitaji ukienea. Hata katika muktadha huu, kukutana na Kristo kunaweza kurejesha maana na thamani kamili kwa maisha ya watu, na Kanisa hugundua tena umuhimu wa kudumu wa agizo alilopokea kutoka kwa Bwana mfufuka. Hakuna anayeweza kuchukua nafasi yake katika utume huu, hata kama ni muhimu kuhakikisha msingi unaotegemeka wa mustakabali wa binadamu, mustakabali wa amani, haki, uhuru, na udugu.

Nawaalika hata ninyi kuchukua Waraka wa Evangelii gaudium

Kama ilivyoonekana wazi katika Mkutano Mkuu wa mwezi Januari iliyopita Baba Mtakatifu alisema Wosia wa Kitume wa Papa Francisko wa  Evangelii Gaudium (Furaha ya Injili) unaendelea "kuwakilisha hatua muhimu ya marejeo: hauleti tu maudhui mapya, bali unalenga kila kitu kwenye kerygma kama moyo wa utambulisho wa Kikristo na wa kikanisa" (Barua kwa Makardinali, Aprili 22, 2026). Kwa hivyo Papa Leo XIV aliwaomba pia kuchukua Waraka huo wa Evangelii Gaudium katika kazi yao,  katika ngazi zote, ili kuhamasisha utume ambao ni "msisitizo wa Kikristo na wa kerygma(Tangazo), liliozaliwa kutokana na kukutana na Kristo anayeweza kubadilisha maisha." Hitaji kubwa la kiroho linalozidi kuongezeka, hasa miongoni mwa vijana, na ambalo lilioneshwa wazi wakati wa Jubilei ya Vijana, linastahili kuzingatiwa sana. Kizazi kipya hakizuiliwi kutoka Injili; kinyume chake, wengi, wanapoigundua upya, wanatamani kuijua vyema, kwa sababu wanaona kwamba ina siri ya furaha ya kweli.

Uinjilishaji hautegemei ufanisi wa miundo

Baba Mtakatifu ana uhakika kwamba Baraza lao la Kipapa linazingatia sana swali hilo, ambalo watu wa wakati wetu wanauliza kwa msisitizo mkubwa zaidi na ambalo linahitaji jibu la kuaminika na thabiti. Uinjilishaji hautegemei ufanisi wa miundo au umuhimu wa kijamii, wala hata makubaliano ambayo yanaweza kupatikana wakati wowote. Kinachobaki ni muhimu, badala yake, kuamini mwongozo wa Roho Mtakatifu, kufuata njia anazoelekeza ili kuwaongoza wengi kwa Kristo, kwa neno lake la kuokoa, kwa upendo wake unaohuisha maisha.

Uinjilishaji lazima upimwe leo hii hata kwa hali na uenezaji wa imani kwa kizazi na kizazi

Hasa uinjilishaji leo hii, lazima pia ushughulikie hali na mienendo inayobadilika ya uenezaji wa imani kutoka kizazi hadi kizazi. Katika baadhi ya maeneo ya dunia, uenezaji huu umekoma kabisa, ukihitaji uwezo wa kukabiliana na changamoto mpya. Sababu za hali hii zinajulikana sana na nyingi; hata hivyo, matokeo yake ni "umaskini" wa kiroho miongoni mwa vizazi vichanga, ukosefu wa motisha na zana za kukuza kwa uhuru kujitolea kwa imani ambayo hutoa maana kwa maisha. Kwa bahati nzuri, ulimwenguni kote, kuna uzoefu mwingi na tofauti ambao kupitia kwake jumuiya za Kikristo, vyama, harakati, na vikundi vya kanisa hukutana na vijana, kuwasikiliza, na kushirikiana nao. Hali ya kiutamaduni iliyoenea katika jumuiya zinazotumia sana na zinazopenda matumizi hupunguza uwezo wa kujifunza kwa uvumilivu na kufuata kwa bidii safari ya kibinafsi ya kutafuta ukweli, kwa uvumilivu na jicho la kukosoa. Kila ujumbe una hatari ya kuonekana kama maoni moja tu kati ya mengi.

Kueneza kwa imani

Uenezaji wa imani, katika muktadha huu, lazima utokee kupitia kukutana na watu na jamii zinazoelezea furaha ya imani ya Kikristo na mshikamano wa mtindo wa maisha wa kiinjili. Kwa hakika si kwa kupunguza maudhui yake na kupunguza mahitaji yake ndipo Ukristo unaweza kuvutia, bali kwa kutoa ushuhuda kwa unyenyekevu na ujasiri wa "njia, ukweli, na uzima" ambao umewaongoa na kuwatakasa wengi. Kama Benedikto XVI alivyosema: "Tunachohitaji kwa wakati huu katika historia ni wanaume ambao, kupitia imani iliyoelimika na iliyo hai, humfanya Mungu aaminike katika ulimwengu huu. [...] Tunahitaji watu wanaomkazia macho Mungu, wakijifunza kutoka huko ubinadamu wa kweli. Tunahitaji watu ambao akili zao zimeangazwa na nuru ya Mungu na ambao mioyo yao Mungu huifungua, ili akili zao ziweze kuzungumza na akili za wengine na mioyo yao iweze kufungua mioyo ya wengine.

Ni waamini walioguswa na Mungu,kwa Mungu wanaweza kurudi

Ni kupitia wanadamu wanaoguswa na Mungu pekee ndipo Mungu anaweza kurudi kwa wanadamu" (Benedikto Europe in the Crisis of Cultures, Siena 2005, 63-64). Kwa hivyo, utakatifu wa maisha hubaki kuwa usemi unaoshawishi zaidi wa uzuri wa imani ya Kikristo, ambayo hupita wakati na iko wazi kwa kila utamaduni. Pia Papa alipenda kusema neno kuhusu katekesi, ambayo huainisha maisha ya Kanisa kwa dhati katika kujitolea kwake katika malezi na uenezaji wa imani. Uangalifu maalum unapewa wakatekumeni, ambao kwa idadi inayoongezeka wanaomba Ubatizo. Huduma ya furaha ya jamii katika kuwakaribisha na kuwasindikiza wakatekumeni haiwezi kuishia na sherehe ya Sakramenti. Kazi inayofuata inahitaji kiasi sawa cha uwajibikaji: ile ya kutoa mazingira yanayotimiza matarajio yaliyosababisha kushikamana na Kristo na Kanisa lake.

Kuwasindikiza wabatizwa, komunio na  wa kipaimara

Wajibu wa kuweka hai chaguo la imani lililofanywa wakati wa Ubatizo unahusisha, hasa kwa jumuiya za parokia, hitaji la kujitahidi kila wakati kwa kiwango cha juu cha maisha ya Kikristo (taz. Mtakatifu Yohane II, Waraka wa Kitume Novo Millennio Ineunte, 31), kuwahakikishia waliobatizwa karibuni nafasi ya ukuaji thabiti, matunda ya mahusiano ya kibinadamu yanayoishi katika upendo na huduma ya pamoja. Uangalifu kama huo unapaswa kuwekwa kwa vijana wa kike na kiume  wanaopokea sakramenti ya Kipaimara.  Papa aliwahimiza mipango mingi inayosindikizana nao wanapoendelea na safari yao ya imani kwa ukuaji wao wa kibinadamu na Kikristo. Mapendekezo haya yanafanywa kuwa na ufanisi wa kweli kwa uangalifu unaotolewa kwa kila mmoja wao kibinafsi, kielelezo cha upendo wa kipekee na wa kibinafsi wa Bwana. Baba Mtakatifu aliwashuru kwa huduma yao kwa huduma yake na kwa Kanisa lote, na kuwakabidhi kwa Bikira Maria, mfuasi mkamilifu na mmisionari wa Injili, kuwasindikiza na baraka zangu.”

Papa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

28 Mei 2026, 18:07