Magofu ya nyumba nchini Ukraine. Magofu ya nyumba nchini Ukraine. 

Papa Leo XIV:Vita havitatui matatizo,lakini huyazidisha

Mwishoni mwa Katekesi Papa Leo XIV alitoa wito mpya kufuatia kuongezeka kwa kasi ya mgogoro Ukraine na Urusi.Alionyesha ukaribu wake na wale wanaoteseka kutokana na mashambulizi,"ikiwa ni pamoja na dhidi ya raia na akakumbuka kwamba mahali ambapo makombora na ndege zisizo na rubani huanguka,ndivyo matumaini yanavyoanguka."Hatimaye,aliwakabidhi watu wote waliojeruhiwa na vita ulinzi wa Maria,Malkia wa Amani.

Na Angella Rwezaula – Vatican

Mwisho mwa Katekesi ya Baba Mtakatifu, Jumatano tarehe 27 Mei 2026 , mawazo ya  Papa Leo XIV yalielekezwa kwa mara nyingine kwa nchi zilizojeruhiwa na vita, hasa wasiwasi kuhusu mzozo nchini Ukraine, ambao umekuwa ukiongezeka sana katika siku za hivi karibuni. Papa alisema: “Ninafuatilia kwa wasiwasi vita vya Ukraine, ambavyo vimeongezeka kwa kiasi kikubwa katika siku za hivi karibuni. Nataka kuonyesha mshikamano wangu na wale wote wanaoteseka kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni, ambayo pia yamelenga raia.” Papa aliongeza “ Vita havitatui matatizo; vinayazidisha. Havijengi usalama; vinazidisha mateso na chuki. Pale ambapo makombora na ndege zisizo na rubani huanguka, matumaini huvunjwa, nyumba na sehemu za ibada huharibiwa, na maisha ya watu wasio na hatia hukatizwa. Ninawakabidhi watu wote walioathiriwa na vita ulinzi wa Bikira Maria, Malkia wa Amani.”

Mashambulizi

Ripoti za mashambulizi ya Urusi usiku wa Mei 26 katika eneo la Donetsk zilitolewa. Usiku kati ya Jumamosi, Mei 23, na Dominika Mei 24, mfululizo wa mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Urusi uligonga mji mkuu Kyiv na maeneo ya jirani, na kuua watu wasiopungua wanne na kujeruhi zaidi ya 50 katika moja ya mashambulizi makubwa zaidi dhidi ya mji mkuu wa Ukraine tangu kuanza kwa vita. Urusi ilitumia ndege zisizo na rubani 600 na makombora 90, kulingana na Jeshi la Anga la Ukraine, ambapo 549 zilikamatwa na 55 zilikamatwa. Katika siku za hivi karibuni, shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine kwenye bweni la wanafunzi huko Starobilsk, katika eneo la Luhansk la Donbas linalokaliwa kwa mabavu, lilisababisha vifo vya watu 21 na 44 kujeruhiwa. Kulingana na jeshi la Ukraine, lilikuwa shabaha ya kijeshi.

Katika salamu zake kwa wamini wanaozungumza Kifaransa na Kiarabu, Papa Leo XIV aalizungumza hasa mahujaji kutoka Lebanon, nchi nyingine iliyoathiriwa na janga la vita. Pia aliwaomba wamwombe Roho Mtakatifu ili upya wa kiliturujia, waaminifu kwa Mapokeo halisi, uweze kuimarisha ushirika wa kikanisa na ushiriki kamili wa waamini." Akiwasalimu mahujaji na wageni wanaozungumza Kiingereza wanaoshiriki katika katekesi hiyo , hasa vikundi kutoka Uingereza, Ireland, Cameroon, Kenya, na Nigeria, India, Pakistan, Ufilipino, Korea Kusini, Canada na Marekani, Papa alisema, “ Amani ya Mungu na ilinde akili na mioyo yenu ili mpate kujua upendo wa Yesu Kristo na kuushiriki kwa furaha na wengine. Mungu awabariki!”

Akigeukia waamini wa Poland, Papa Leo XIV alikumbuka kwamba Mei 26, walisherehekea Siku ya Mama, akiwashukuru akina mama wote "waliowapa watoto wao zawadi ya uhai kwa ukarimu, kwa kuwafundisha upendo kwa Mungu na jirani." Mama Mtakatifu wa Mungu, aliomba, "awaombee ili wapate neema ya kifungo cha kudumu na Yesu." Kwa msaada wake, aliwaomba Wapoland wote kulinda "maisha ya kila mtu katika nchi yao, kuanzia mimba hadi kifo cha kawaida."

Wito wa papa vita Ukraine
27 Mei 2026, 15:48