2026.05.30 Papa akutana na wajumbe wa Mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus Pro Pontifice. 2026.05.30 Papa akutana na wajumbe wa Mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus Pro Pontifice.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XVI:lazima kuishi uhuru na mazungumzo yanayojengwa katika ukweli

Baba Mtakatifu Leo XIV,Jumamosi tarehe 30 Mei 2026 alikutana mjini Vatican na wajumbe wa Mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus Pro Pontifice na kuakisi umuhimu wa Mafundisho Jamii ya Kanisa katoliki katika ulimwengu uliogawanyika."Ubinadamu ulioshirikishwa ni dawa ya vita na mgawanyiko."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Leo XIV alifanya mkutano na wanachama wa Mfuko wa Kipapamwa  Centesimus Annus Pro Pontifice,  Jumamosi tarehe 30 Mei 2026 mjini Vatican. Karibu watu 400 wanashiriki katika Mkutano Mkuu wa Mfuko huo kwa 2026 na Mkutano wa Kimataifa. Katika hotuba yake, Papa aliwasihi Wakatoliki kutumia Mafundisho jamii ya Kanisa Katoliki ili kujibu masuala yanayokabili jamii, ikiwa ni pamoja na vita, utengano, na migawanyiko ya kijamii. Papa alibainisha kuwa mkutano wa kila mwaka wa Mfuko huo uliambatana na kuchapishwa hivi karibuni kwa waraka wake wa Magnifica humanitas. "Katikati ya udhaifu, tumaini jipya linaibuka," alisema. "Hata mgawanyiko unapoonekana kukua, dhehebu moja ambalo bila shaka linatuunganisha sote linaonekana: ubinadamu wetu wa pamoja."

Wakati wa shida,mwanadamu hurudi katika swali msingi

Papa Leo XIV alisema nyakati za shida humwita mwanadamu kurudi kwenye maswali ya msingi ambayo yamechochea mioyo ya vizazi: "Tunaelekea wapi? Tunataka kujielekeza kwenye lengo gani? Ni mwelekeo gani tunapaswa kuchagua kama watu na kama jamii ya wanadamu?" Maswali haya, alisema, yanafichua utafutaji wa ukweli wa wanadamu na kuamsha kiu yetu kwa Mungu na maana. Pia yanaelekeza kwenye vipengele vya ndani zaidi vya mwanadamu, hasa "zawadi zilizotolewa na Mungu za akili na uhuru," ambazo kupitia hizo wanaume na wanawake wanaweza kujua ukweli na kuchagua kilicho kizuri.

Uhuru wa kweli unapata utimilifu tunapoishi zawadi ya nafsi

Baba Mtakatifu  akitafakari kuhusu uhuru, alionya dhidi ya kuupunguza hadi "uwezo wa kufanya kile ambacho mtu anachotaka." Papa alisema uhuru wa kweli hupata utimilifu tu tunapouishi kama zawadi ya nafsi na uwazi kwa wengine. Wakati uhuru unakuwa kamili kwa njia ya ubinafsi, aliongeza, unapoteza maana na heshima yake ya asili. Papa aliunganisha maono haya na miji miwili iliyoelezwa na Mtakatifu Agostino: Jiji la Mwanadamu, lililojengwa juu ya kiburi na kujipenda, na Jiji la Mungu, lililojengwa juu ya upendo wa Mungu na kutokuwa na ubinafsi. Papa Leo XIV alisema, Jiji la Mungu limejengwa juu ya mahusiano na kuwezesha kujenga ustaarabu wa kweli wa upendo.

Mgogoro unaokabili demokrasia za kisasa

Papa Leo XIV aidha alikumbuka mgogoro unaokabili demokrasia za kisasa,  kuwa  chanzo cha kweli kinatokana na mgogoro wa anthropolojia, kwa kuwa binadamu wamemsahau Mungu na hivyo jinsi ya kupendana. Licha ya hayo, Papa Leo XIV alisema,  Wakristo hawapaswi kukata tamaa. Badala yake, tunaitwa kufanya sehemu yetu kupitia uaminifu thabiti katika maisha ya kila siku. Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alikumbusha Wanachama wa Mfuko wa Centesimus Annus Pro Pontifice kwamba mazungumzo yaliyojengwa katika ukweli yanahitajika ili kuunda ustaarabu uliojengwa juu ya upendo. "Kuzingatia utu wa asili wa kila mtu, huruhusu ubinafsi na maslahi maalum kushinda kwa niaba ya manufaa ya wote."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

30 Mei 2026, 10:55