Ujumbe wa Papa Leo XIV kwa Harakati ya Kiekumeni:pelekeni Injili kwa watu wote

Tunaweza kuupatia ulimwengu mpya wa amani uhai,anasema Papa Leo XIV katika ujumbe wake kwa njia ya Video kwa Harakati ya Kiukumeni duniani kote iliyoko kwenye maombi kuanzia Mei 14-24.Papa anawatia moyo katika dhamira yao ya"kushiriki Injili kwani sio jambo ambalo tunaweza kulikalia kimya."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kabla ya tukio la maombi ya Harakati ya kiekumeni ya"Ufalme Wako Ufike,” Baba Mtakatifu Leo XIV alituma ujumbe kwa njia ya video kwa washiriki wote, akiwahakikishia ukaribu wake wa kiroho. Tukio hilo, ambalo linafunguliwa kuanzia tarehe 14 hadi 24 Mei 2026, ni harakati ya maombi inayowaalika Wakristo ulimwenguni kote kusali pamoja kuanzia Alhamisi ya Kupaa kwa Bwana hadi Dominika ya Pentekoste ili watu wengi zaidi wamjue Yesu. "Ufalme Wako Ufike"(TKC) ni Harakati ya Kiekumeni ilianza mwaka 2016 na imekua na kuwashirikisha zaidi ya Wakristo milioni moja katika karibu 90% ya mataifa ulimwenguni kote, ikijumuisha madhehebu na tamaduni 85 tofauti.

Mungu yuko pamoja nasi

Katika ujumbe wake kwa njia ya video, Papa Leo XIV kwa lugha ya kiingereza anatafakari msemo wa kiutamaduni wa kipindi cha Majilio: “Njoo, Emanueli.” Kwa hilo, Wakristo wanataka kukamilisha unabii wa Isaya wa kuzaliwa kwa Emanueli, kumaanisha Mungu yuko pamoja nasi. Katika kipindi hicho chote cha kusubiri, Papa Leo XIV anaakisi  jinsi sala na nyimbo zetu zinavyozidi kuwa za haraka kwa Mungu kushuka kati yetu, kutuokoa kutoka katika dhambi na yote yanayoweza kutudhuru. Anabainisha kuwa tunataka Mungu aponye kile kilichovunjika ndani yetu kibinafsi na duniani.

“Ingawa tunajua kwamba Mungu ni mwenyezi na ana uwezo wa kupita kiasi, bado tuna ujasiri wa kutosha kumwomba awe pamoja nasi kweli, si mbali, bali karibu,” Baba Mtakatifu anasisitiza. Hata hivyo, wakati mwingine, tunasahau kwamba tunamhitaji Mungu na jinsi Yeye pekee anavyoweza kutosheleza matamanio yetu ya ndani na kutotulia kwetu kwa ndani."Katika nafsi ya Yesu Kristo, Mungu ameshuka ili kuwa karibu nasi katika mwili. Sasa, kupitia Roho Wake Mtakatifu Yuko pamoja nasi.

Aleluya ni wibo wa kipindi na njia ya shukrani kwa ufufuko wa Yesu

Katika siku hizi 50 za Pasaka, "Aleluya" inakuwa wimbo wa kipindi  na njia ya kutoa sifa na shukrani kwa ufufuko wa Yesu. "Bado yuko Mungu pamoja nasi", Papa Leo XIV anasisitiza tena  huku akionesha kwamba hata marafiki zake wa karibu hawakumtambua kila mara baada ya ufufuko Wake. Ingawa Yesu alirudi kwa Baba wa Mbinguni, “Hakutuacha yatima.” Kupitia kipaji cha Roho Mtakatifu, Yeye anabaki kuwapo kwetu sote katika Kanisa. Baba Mtakatifu anaendelea: “Kristo, ndiye kila kitu kwetu. Ndani Yake, tunapata utimilifu wa uzima na maana yake. Papa anabainisha zawadi hii si kitu tunachoweza kujiwekea. Badala yake, ni kitu cha kutangaza kwa ujasiri.”

Novena ya Harakati ya Ufalme Wako Ufike

Kwa njia hiyo Novena ya "Ufalme Wako Ufike," inatoa fursa nzuri ya kushiriki Habari Njema na kuomba kwamba wengine pia waje kukutana na upendo wa kuokoa na ukombozi wa Mungu uliofunuliwa katika Yesu.” Papa Leo anahitimisha ujumbe wake wa video akisimulia mahubiri yake ya Mkesha wa Pasaka mwaka huu: “Mkutano ambao tunataka kutoa ushuhuda kupitia maneno ya imani na matendo ya upendo tunafanya hivyo kwa “kuimba” na maisha yetu “Aleluya” tunayotangaza kwa midomo yetu (Mtakatifu Agostino, Mahubiri 256, 1).

Kuwa na hamu ya kujetokea kuwapelekea Injili watu wote

Kama wanawake katika Injili siku ya Dominika ya Pasaka, Baba Mtakatifu Leo XIV anabainisha kwamba tunapaswa kuwa na hamu ya "kujitolea" kuwapelekea watu Injili  ulimwenguni kote. "Sisi pia tunaweza kutoa uhai kwa ulimwengu mpya wa amani na umoja kama 'kundi la watu na bado [...] mtu mmoja, kwani ingawa kuna Wakristo wengi, Kristo ni mmoja'" (Mtakatifu Agostino Maoni ya Zaburi, 127:3). Papa anahitimisha kwa kuwapa Baraka nyingi kutoka kwa Mungu wote.

KARAKATI YA KIEKUEMENI YA UFALME WAKO UFIKE

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

14 Mei 2026, 13:18