Ziara ya Papa Leo XIV kwenda Ufaransa 25-28 Septemba 2026
Vatican News
Baada ya Hispania, Ziara ya Kitume ya Papa Leo XIV itakayofuata itakuwa tena katika nchi ya Ulaya, huko Ufaransa.
Ofisi ya Habari ya Vatican Jumamosi tarehe 16 Mei 2026 ilitangaza kuwa: "Kwa kukubali mwaliko wa mkuu wa nchi na mamlaka ya kikanisa ya nchi hiyo, na ule wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Baba Mtakatifu Leo XIV atafanya ziara yake ya kitume kwenda Ufaransa kuanzia tarehe 25 hadi 28 Septemba 2026, na atatembelea makao makuu ya Shirika hilo," taarifa ilisomeka.
Hii itakuwa Ziara ya tano ya Kimataifa ya Papa Leo XIV, kufuatia na zile za Uturuki na Lebanon (Novemba 27 - Desemba 2, 2025), Ufalme wa Monaco (Machi 28), Afrika (Aprili 13 - 23), na Hispania itakayofanyika kuanzia (Juni 6 - 12).
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
