Papa Leo XIV,Misa kwa Makardinali:Vita havistahili kamwe mwanadamu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza Ibada ya Misa ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Makardinali katika Basilika ya Mtakatifu Petro, tarehe 26 Juni 2026 huku akiwakabidhi makardinali vigezo vitatu vya utambuzi:kushiriki uhuru wa kweli katika imani, kukaribisha zawadi ya amani katika umoja, na kuishi kwa maelewano katika utii.” Kwa kutazama migogoro na mivutano ya kimataifa, Papa alisema Vita havibarikiwi kamwe na Mungu.”Katika ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Pili uliotishwa na Papa, baada ya ule wa Januari iliyopita ambao vikao vemeanza asubuhi katika Ukumbi wa Paulo VI na na vitahitimishwa tarehe 27 Juni 2926.
Nguzo za Kanisa
"Tumefika kuadhimisha Misa ya Ekaristi hii kutoka kila sehemu ya dunia: pamoja na maisha yetu, kwa hivyo tunamtolea Mungu jumuiya na watu tunaobeba mioyoni mwetu, pamoja na mipango na uzoefu wetu wa kichungaji, wa furaha na changamoto. Aina mbalimbali za mapenzi na mawazo" ambayo yamejikita katika Kristo, "uzima wa kweli" ambao hutiririka neema na Ukweli, "maji yenye rutuba" kwa Mkutano Mkuu ambao unafunguliwa katika usiku muhimu wa kukaribisha sherehe za Watakatifu Mitume Petro na Paulo. Tuache pamoja katika kumbukumbu hii, ambayo inakumbusha nguzo za Kanisa Katoliki na la Roma, wamisionari wawili waliouawa kishahidi ambao mahubiri yao yalikuwa muhimu sana katika maisha yao kiasi kwamba yakawa sehemu ya Maandiko Matakatifu.
Mifano ya Watakatifu Petro na Paulo
Papa Leo XIV alirudi kwenye somo, akitafakari katika mahubiri yake kuhusu maneno ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho na kuhusu "karama tofauti", huduma na shughuli za kikanisa, sawa na "matawi ya mzabibu ambapo Bwana anamimina Roho Mtakatifu katika Kanisa lake, kulingana na umoja unaolingana na kigezo cha manufaa ya wote, ambacho hufanya huduma zote za kikanisa kuwa nzuri na za kufurahisha. Kwa hivyo, dalili ya kwanza kati ya tatu zinazotolewa kwa ajili ya kutambua kazi inayoendelea: kwanza kabisa, Papa Leo XIV alisema, mfano wa Watakatifu Petro na Paulo unatutia moyo kushiriki uhuru wa kweli katika imani. Ni uhusiano na Bwana Yesu hasa unaotuweka huru kutoka katika dhambi na hofu. Imani ni ile fadhila, isiyopaswa kuchukuliwa kirahisi, ambayo huipatia Kanisa uhai, kwa sababu inalingana na neema inayolisha matawi ya mzabibu. Kanisa lililo hai ni Kanisa linaloamini, kupitia kipaji cha Roho Mtakatifu aliyemiminwa mioyoni mwetu: Kanisa hili huzaa matunda mengi.
Kuomba zawadi ya amani katika umoja
Kwa njia hiyo Papa Leo XIV alihimiza kuomba zawadi ya amani katika umoja. Ingawa mwaliko wa imani, ambayo tuko huru kweli, unatolewa kwa watu wote, mivutano na migogoro ya kimataifa inaumiza sana familia ya wanadamu, Papa alikumbusha: hata hivyo, kwamba hakuna uhaba; kiukweli,wa mipango na uzoefu vinaongezeka katika Kanisa na duniani vinavyohitaji heshima kwa utu wa binadamu, haki, sheria, na kwa ajili ya ubinadamu tu. Katika Kipengele hiki cha mwisho, Papa Leo XIV alisisitiza, kuwa ni sababu ya matumaini, kwa sababu kinathibitisha uzuri wa kazi ya Mungu, ambaye utukufu wake duniani, mwanadamu ndiyo ishara. Na ishara hii inapojeruhiwa, "sote tumejeruhiwa. Inapoharibiwa, sote tunateseka. Inapouawa,sote tunahisi tumeraruliwa."
Vita havisahili kamwe mwanadamu
Kwa njia hiyo Papa alisema kwamba, “vita havistahili kamwe mwanadamu, na havibarikiwi kamwe na Mungu, kwa sababu Muumba ametujalia akili na utashi wa kutatua migogoro kama wanadamu na si kama wanyama, labda walio na silaha za kiteknolojia nyingi. Familia ya wanadamu ni umoja, ambao hutangulia watu na mtu mmoja mmoja. Na, sio ukweli wa kibiolojia tu bali ni kanuni ya maadili. Amani ni wajibu wa haki, anaelezea, kwa sababu sisi ni familia moja ya kibinadamu, ubinadamu mzuri unaompata Kristo ambaye ni Kichwa na Mkombozi wake. Akikumbuka waraka uliochapishwa mnamo Mei 15 iliyopita, Papa Leo XIV alisisitiza kudumu kwake katika njia iliyochomwa na Mtakatifu Paulo VI na ustaarabu wa upendo, licha ya Vita Baridi, mbio za silaha, na kukosekana kwa usawa mkubwa wa kiuchumi ulioashiria enzi hiyo. Hata leo, inawezekana kufikiria njia mbadala: hivyo, ushuhuda wa Kikristo unakuwa unabii wa ulimwengu mpya, Uinjilishaji na huduma, mpango wa kitamaduni na kijamii unaohamasisha kikamilifu maendeleo ya binadamu.
Aliyekufa na kufufuka, ni mzabibu wa kweli anayezaa matunda
Upatanisho katika utii ni agizo la tatu alilotoa Papa Leo XIV kwamba: utekelezaji wa Sinodi, unawaalika kila mtu kuendelea katika umoja wa imani, katika kukuza amani, katika utii kwa Neno lililo hai, ambaye ni Yesu. Kuwa mwanadamu, Neno moja linajieleza katika lugha zote kwamba; amekufa na kufufuka, yeye ndiye mzabibu wa kweli, uzaa matunda kupitia tamaduni zote ambazo Wakristo hubadilisha kutoka ndani. Kwa njia hiyo, katika kazi ya pamoja, ushirika hufupisha sinodi ambayo wote waliobatizwa hushiriki, katika umoja wa Watu wa Mungu, Papa alisisitiza, kwamba “sinodi na ushirika ni aina za udugu wa Kikristo." Kwa mwanga huo, msaada unaotoka kwa makardinali katika utekelezaji wa huduma ya Petro unampata ndani yangu yule anayeomba, si yule anayeamuru, Papa alihitimisha, kwa sababu mamlaka ya ukuu ni sahihi kwa yule anayesikiliza na kwa hivyo anaongoza tu, kwa yule anayejifunza na kwa hivyo anafundisha tu, akimfuata Mwalimu mmoja kila wakati.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
