Papa Leo XIV kuanzia tarehe 6 hadi 12 Juni 2026 anafanya Hija ya 4 ya Kitume nchini Hispania kwa kunogeshwa na kauli mbiu: "Alzad la mirada" Yaani "Inua macho yako.” Yn 4:35. Hotuba kwa viongozi na wanadiplomasia Papa Leo XIV kuanzia tarehe 6 hadi 12 Juni 2026 anafanya Hija ya 4 ya Kitume nchini Hispania kwa kunogeshwa na kauli mbiu: "Alzad la mirada" Yaani "Inua macho yako.” Yn 4:35. Hotuba kwa viongozi na wanadiplomasia  (@Vatican Media)

Hija ya 4 ya Kitume ya Papa Leo XIV Hispania: Mapokezi na Hotuba Kwa Viongozi

Papa Leo XIV: Amegusia kuhusu mchango mkubwa uliotolewa na Yakobo Mtume katika mchakato wa uinjilishaji nchini Hispania, kiasi cha kuchangia taalimungu na utume wake. Papa anasema, yuko kati yao ili kuwatia shime, kupyaisha uaminifu wao, ili waweze kujikita katika mchakato wa upatanisho; ujenzi wa utamaduni wa watu kukutana, ili kukoleza ujumbe wa amani. Amegusia pia kuhusu mchakato wa watakatifu Yohane wa Msalaba na Mt. Thetesa wa Avila.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV kuanzia tarehe 6 hadi 12 Juni 2026 anafanya Hija ya 4 ya Kitume nchini Hispania kwa kunogeshwa na kauli mbiu: "Alzad la mirada" Yaani "Inua macho yako.” Yn 4:35. Kuna waandishi wa habari 80 walioko kwenye msafara wa Baba Mtakatifu nchini Hispania, wanaotoka katika nchi kumi na kati ya waandishi hawa 20 ni wale wanaotoka nchini Hispania na kutokana na muktadha huu, Baba Mtakatifu ametambua uwepo na huduma yao. Hii ni hija ya kwanza ya Kitume ya Baba Mtakatifu Leo XIV nchini Hispania na kwamba, anayo furaha kubwa kutembelea Hispania, ingawa amekuwa akitembelea Hispania mara kadhaa, lakini kwa wakati huu, anaitembelea kwa utume maalum: Anakwenda kukutana na waamini, kusherehekea zawadi ya imani, kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Kristo Yesu na wakati huo huo kusalimiana na watu wote wa Mungu nchini Hispania. Hii inatokana na ukweli kwamba, Kanisa lina ujumbe kwa kila mtu.

Hotuba kwa viongozi wa serikali, kijamii na wanadiplomasia
Hotuba kwa viongozi wa serikali, kijamii na wanadiplomasia   (@Vatican Media)

Ni katika Kumbukumbu ya Bikira Maria Mama wa Kanisa, ambayo inaadhimishwa, Jumatatu baada ya Sherehe ya Pentekoste na kwa mwaka huu ilikuwa ni tarehe 25 Mei 2026 ilibeba uzito wa pekee kwani Waraka wa kwanza wa Kitume wa Baba Mtakatifu Leo XIV: “Magnifica humanitas” yaani: “Utu wa kupendeza" Juu ya Hifadhi ya Mwanadamu Katika Enzi ya Teknolojia ya Akili Unde” kwa kifupi “MH” umezinduliwa rasmi. Katika Waraka huu wa Kitume, Baba Mtakatifu Leo XIV anazungumzia kuhusu: Mtazamo thabiti wa uaminifu kwa Injili; misingi na kanuni za Mafundisho Jamii ya Kanisa; Teknolojia na utawala. Ukuu wa ubinadamu katika nuru ya ahadi za teknolojia ya akili unde; Kulinda utu wa binadamu wakati wa mabadiliko: na hatimaye ni kuhusu: Ukweli, kazi, uhuru; utamaduni wa nguvu na ustaarabu wa upendo. Mwishoni mwa Waraka wake wa Kitume, Baba Mtakatifu Leo XIV anapendekeza programu ya maisha ya Kikristo inayosimikwa katika kiasi, lakini inayohitaji nguvu ya kuweza kukabili mabadiliko ya teknolojia wakati wowote kwa mwanga wa Injili. Njia hii inawezekana kwa waamini kutafakari mpango wa Mungu katika maisha yao, kwa kujenga na kudumisha umoja na ushirika wa Kikanisa kwa ushiriki mkamilifu katika Maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu sanjari na kujikita katika ujenzi wa Ulimwengu unaozingatia wema wa wote na kuendelea kusali katika umoja na Bikira Maria Mama wa Kanisa. Mwishoni, Baba Mtakatifu amewatakia waandishi wote wa habari walioko kwenye msafara wake safari na kazi njema na kwamba, anapenda kujikita zaidi kwa vijana ambao wana shauku, ili waweze kushiriki furaha ya imani Jijini Madrid, Barcelona na Visiwa vya Canary.

Kuna waandishi 80 walioko kwenye msafara wa Papa nchini Hispania
Kuna waandishi 80 walioko kwenye msafara wa Papa nchini Hispania   (@Vatican Media)

Akiwa njiani kuelekea nchini Hispania, Baba Mtakatifu Leo XIV amewatumia ujumbe wa matashi mema Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, huku akikumbushia safari yake ya kikazi mjini Vatican na hatimaye, amewapatia baraka zake za kitume watu wote wa Mungu nchini Ufaransa. Baba Mtakatifu pia amemtumia Rais Sergio Mattarella wa Italia salam na matashi mema, huku akijiweka chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria anayewaongoza watu wote kwa Mungu, kwani Bikira Maria ni chemchemi umoja na matumaini kwa watu wote. Baba Mtakatifu anasema, anawasindikiza watu wa Mungu nchini Italia kwa sala na sadaka yake, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Kwa upande wake, Rais Sergio Mattarella wa Italia amemjibu Baba Mtakatifu Leo XIV kwa kumshukuru kwa matashi mema na kwamba, Hispania ni nchi ambayo tangu karne ya mwanzo ukatoliki umeota na kuzamisha mizizi yake na kwamba, huu ni wakati wa kuinua macho yao mbinguni, ili kupanua wigo wao unaowatambua watu wengine kuwa ni ndugu wamoja, kama kauli mbiu ya hija hii nne ya kitume nchini Hispania inavyosema, "Alzad la mirada" Yaani "Inua macho yako.” Yn 4:35. Hija hii ya kitume katika muktadha wa Kimataifa, kuna maeneo mengi duniani yaliyokumbwa na vita, kinzani na mipasuko ya kijamii; kuna umwagaji mkubwa wa damu ya watu wasiokuwa na hatia, changamoto kubwa iliyoko mbele ya watu wengi ni kutambua na kuthamini umuhimu wa Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo na kwamba, amani ya kweli inapata chimbuko lake kutoka katika sakafu ya moyo wa mwanadamu, jambo la msingi ni kwa watu wote wenye mapenzi mema kugundua ndani mwao, maana ya jumuiya, umuhimu wa ujenzi wa utamaduni wa watu kukutana na kusaidiana.

Papa Leo XIV amepata mapokezi makubwa ya kukata na shoka
Papa Leo XIV amepata mapokezi makubwa ya kukata na shoka   (@Vatican Media)

Rais Sergio Mattarella anakiri kwamba, hija hii ya kitume inachota amana na utajiri wake mkubwa katika maisha ya kiroho, kihistoria na kitamaduni, mambo ambayo yanapewa kipaumbele cha pekee wakati huu wa hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Leo XIV nchini Hispania, sanjari na maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu Mtumishi wa Mungu Antoni Gaudì Cornet alipofariki dunia. Kazi yake inayojulikana zaidi ni Kanisa la Mapilipizi ya Dhambi la “Sagrada Familia.” Antonio Gaudí Cornet, aliyezaliwa tarehe 25 Juni 1852, pengine huko Reus, alikubali kusimamia ujenzi wa Kanisa hili mwaka mmoja mara baada ya kuwekwa kwa jiwe la msingi, kunako mwaka 1883, akiwa na umri wa miaka 31. Tangu wakati huo na kuendelea, alijisadaka maisha yake yote kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hili, Nyumba ya Ibada, ambapo alionesha ujuzi wake wa kisanii, hisia zake za maisha ya kiroho na kidini. Katika changamoto za maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, katika sera na mikakati ya kiuchumi na kijamii, Jumuiya ya Kimataifa haina budi kuendelea kuhakikisha kwamba, hata kwa siku za usoni, kunakuwepo na amani, usalama na utulivu. Vijana wa kizazi kipya wanapaswa kupewa kipaumbele cha pekee, bila kuwasahau wakimbizi, wahamiaji na wafungwa na kwamba, kuna haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kujikita katika sera jumuishi, ili kulinda na kudumisha utu, heshima na haki msingi za binadamu na kwamba, Ukanda wa Mediterrania unarejesha wito na dhamana yake ya kuwa ni mahali pa majadiliano, watu kukutana na kuonesha mshikamano wa udugu wa kibinadamu. Ni matumaini ya Rais Sergio Mattarella wa Italia kwamba, Baba Mtakatifu Leo XIV katika hija yake ya Kitume atakuwa ni mjumbe na chombo cha imani na matumaini.

Papa Leo XIV ni hujaji wa imani na matumaini kwa watu wa Mungu
Papa Leo XIV ni hujaji wa imani na matumaini kwa watu wa Mungu

Baba Mtakatifu Leo XIV mara baada ya kupata mapokezi makubwa ya Kitaifa alikwenda kumtembelea Mfalme na Malkia wa Hispania, ambako amepata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa Serikali, vyama vya kiraia pamoja na wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao huko nchini Hispania. Baba Mtakatifu Leo XIV katika hotuba yake amegusia kuhusu mchango mkubwa uliotolewa na Yakobo Mtume katika mchakato wa uinjilishaji wa watu wa Mungu nchini Hispania, kiasi cha kuchangia taalimungu na utume wake. Baba Mtakatifu anasema, yuko kati yao ili kuwatia shime, kupyaisha uaminifu wao, ili waweze kujikita katika mchakato wa upatanisho; ujenzi wa utamaduni wa watu kukutana, ili kukoleza ujumbe wa amani. Amegusia pia kuhusu mchakato wa watakatifu Yohane wa Msalaba na Mtakatifu Thetesa wa Avila. Kanisa Katoliki linapenda kujielekeza katika huduma ya upatanisho na amani, kwa kuendeleza majadiliano ya kidini na kiekumene. Tangu mwanzo anasema Baba Mtakatifu Leo XIV Hispania imepokea Habari Njema ya Wokovu, utume uliofanywa na Yakobo Mtume na umuhimu wa taalimungu kama sehemu ya mwendelezo wa utume wa Kanisa unaopata chimbuko lake katika Sherehe ya Pentekoste, mambo ambayo yamechangia katika kuleta mabadiliko katika maisha na utamaduni wa watu wa Mungu nchini Hispania, hapa ni chemchemi ya ibada mbalimbali, amana na utajiri wa muziki mtakatifu, yote haya ni matunda ya watu wa Mungu nchini Hispania kukutana na Kristo Yesu; hawa kwa hakika ni watu wanaopenda na kuthamini Injili ya uhai. Baba Mtakatifu anasema, yuko kati yao ili kuragibisha mchakato wa upatanisho na ushirikiano miongoni mwa watu wa Mataifa, kwa kujikita katika utamaduni wa watu kukutana, ili kukoleza amani, utulivu, ustawi na maendeleo ya wengi. Pia upo mvutano wa daima kati ya fikira na hali halisi ya mambo, changamoto ni kuendeleza majadiliano, ili ukweli uweze kujikita katika uhalisia wa mambo, kumbe, kuna haja ya kuendeleza mchakato wa kujitakasa, upatanisho na majadiliano; mambo msingi katika maisha.

Papa Leo XIV amemtembelea Mfalme na Malkia wa Hispania
Papa Leo XIV amemtembelea Mfalme na Malkia wa Hispania   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu amewataja Mtakatifu Yohane wa Msalaba na Mtakatifu Thereza wa Avilla ambao wamelitajirisha Kanisa ndani na nje ya Hispania na kwamba, Mwaka 2026 Mama Kanisa anaadhumisha Jubilei ya Miaka 300 tangu Mtakatifu Yohane wa Msalababa alipotangazwa kuwa Mtakatifu yaani mwaka 1726 na kilele chake ni tarehe 26 Desemba 2026 sanjari na Jubilei ya Miaka 100 tangu alipotangazwa mwaka 1926 kuwa ni Mwalimu wa Kanisa, changamoto na mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kukimbia giza la uwezo wa mwanadamu kufikiri. Hata leo hii, kile ambacho kinamwogopesha mwanadamu zaidi, ni kile ambacho kwa watu wengi huchochea giza la akili kuwa ni sababu na vurugu za hisia. Hii ndiyo sababu, hata katika maisha ya umma, kunahitajika watu ambao wanaweza kuona mwanga gizani: mwanzo mpya, kama mapambazuko ya ukweli katika kupata amani, ambacho ni kilio cha wengi kutoka katika kina chake, kwa ajili ya ufahamu mpya wa utu wa binadamu na hadhi yake isiyoweza kukiukwa, kwa ajili ya ujenzi wa ustaarabu wa upendo (taz. Magnifica humanitas, 186.)

Papa Leo XIV: Kanisa lina ujumbe kwa kila mtu
Papa Leo XIV: Kanisa lina ujumbe kwa kila mtu   (@Vatican Media)

Kwa maoni ya Mtakatifu Theresa wa Avila, uhuru wa kidini na uhuru wa dhamira lazima ulindwe, kwani ni kwa njia ya mambo haya mwanadamu anajifunza kuwa huru. Ndiyo maana kuna haja ya kuwa na tamaduni, uhuru wa ndani, elimu bora, ili kutafuta na kuambata mchakato wa upatanisho na amani; na kwa kupenda ukweli, kwani maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia anasema, Baba Mtakatifu Leo XIV yametengeza mazingira bandia, kiasi kwamba, chaguzi mbalimbali za binadamu zinatundikwa kwenye majaribu, maamuzi mbele kwani ile dhana ya kufikiri kwa makini inadhohofishwa na mafao ya watu wachache. Baba Mtakatifu anasema, Kanisa lipo kwa ajili ya huduma kwa mwanadamu kwa kuendelea kujikita katika majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni, kama ilivyokuwa katika kipindi cha miaka mingi iliyopita kwa miji ya Cordoba na Toledo, ikawa ni vituo maalum vya majadiliano, ili kujenga umoja na mshikamano wa udugu wa kibinadamu. Mtakatifu Inyasi wa Loyola katika maisha yake, alipinga maneno ya kufedhehesha na chuki kwa kujikita katika ukweli na uwazi, msamaha, kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa utu wa binadamu, amani na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote, kwa kuwajibika; kwa kuthamini athari za kibinadamu na kijamii, ili kuwajumuisha watu walioko hatarini zaidi; na kuendelea kukuza ujuzi wa kidigitali na kuendelea kuongoza tafiti mbalimbali kuelekea ujenzi wa jamii inayosimikwa katika haki na amani. MH 14. Baba Mtakatifu Leo XIV ameipongeza Hispania kwa kuendelea kuwa aminifu kwa Sheria za Kimataifa na ujenzi wa umoja, changamoto ni kuendelea kukuza na kudumisha majadiliano na uragibishaji wa kijamii nchini Hispania, ili kujenga mshikamano na amani kati ya watu; kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa mapambano dhidi ya umaskini miongoni mwa vijana wa kizazi kipya; madai ya uhuru na umoja, ili kuendeleza umoja na mshikamano Barani Ulaya, kama zawadi kwa familia kubwa ya binadamu.

Hotuba kwa viongozi
06 Juni 2026, 14:58