"Leone a Roma"Julai 1,filamu kuhusu miaka ya Prevost katika Jiji la Milele

Filamu hiyo itachapishwa katika lugha tatu (Kiingereza, Kiitaliano,na Kihispania)kwenye chaneli za Vatican News saa 12:00 jioni.Onesho la awali la waandishi wa habari walioidhinishwa litafanyika katika Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Kiti Kitakatifu katika Maktaba ya Filamu ya Vatican Jumatano, Julai Mosi,saa 11:00 jioni.

Vatican News

Baada ya “León de Perú” na “Leo from Chicago,” Radio Vatican – Vatican News inachapisha “Leone a Roma,” yaani "Leo huko Roma", makala mpya inayofuatilia miaka iliyotumiwa na Padre Robert Francis Prevost-Papa Leo XIV wa sasa, katika Jiji la Milele. Kipindi cha takriban miaka ishirini, kuanzia kuwasili kwake Italia kutoka Marekani mwaka 1981, miaka yake akiongoza pia Shirika la Mtakatifu Augustino kwa vipindi viwili, uteuzi wake kama Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu, na kuundwa kwake kama Kardinali mwaka 2023.

Miaka ya masomo, urafiki, safari, mikutano, mikusanyiko, hija, na kazi. Yote yamesimuliwa kupitia picha na video ambazo hazikuonekana hapo awali na sauti za ndugu zake, wanafunzi wenzake, marafiki wa zamani, na wanashirika la Mtakatifu  Augustino na Baraza la Maaskofu. Kwa hivyo Leo mjini  Roma inakamilisha safari ya vyombo vya habari vya Vatican vya kuchunguza zaidi sura na maisha ya Papa, ambayo ilianza na makala ya ‘León de Perú,’ iliyotolewa Juni 2025, kuhusu miaka yake ya utume katika nchi ya Amerika Kusini, na kuendelea na “Leo from Chicago,” iliyotolewa mwezi Novemba, kuhusu mizizi ya Prevost ya Marekani.

Ni toleo la Kurugenzi ya Uhariri ya Baraza la Kipapa la  Mawasiliano. Liliongozwa na waandishi wa habari Felipe Herrera-Espaliat, Salvatore Cernuzio, na Tiziana Campisi, huku likihaririwa na Jaime Vizcaíno Haro na Stefano Anella. Kwa njia hiyo saa 12:00 jioni (saa za Roma) Jumatano tarehe Mosi Julai 2026 makala haya ya (Filamu)itachapishwa kwenye chaneli ya YouTube ya Vatican News, mwanzoni kwa lugha tatu (Kiingereza, Kiitaliano, na Kihispania), na pia yatasambazwa kwa vyombo vya habari vya kimataifa kwa ombi. Onyesho la awali katika Maktaba ya Filamu ya Vatican litafanyika Jumatano tarehe Mosi Julai saa 11:00 jioni kwa waandishi wa habari walioidhinishwa na Ofisi ya Habari ya Vatican.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

27 Juni 2026, 12:00