2025.07.26 Kardinali Tagle Cardinal Tagle(Na John Rhey Nicolas, TV Maria). 2025.07.26 Kardinali Tagle Cardinal Tagle(Na John Rhey Nicolas, TV Maria). 

Kard.Tagle:Urafiki unafichua uso wa Yesu na Kanisa

Kardinali Luis Antonio Tagle na Kardinali Jose Advincula waliwasihi Wakatoliki katika Mkutano wa 12 wa Ufilipino kuhusu Uinjilishaji Mpya kukumbatia urafiki wa kweli na usindikizaji wa subira kama njia muhimu za uinjilishaji, ufuasi wa Kikristo, na ushirika.

Na Padre Kasmir Nema,SVD na Leahna‘Yana’Villajos - Manila.

Urafiki halisi si uhusiano wa kibinadamu tu bali ni njia ya uinjilishaji wenye upendeleo, njia inayofanya uso wa Yesu na Kanisa uonekane katika maisha ya watu, Kardinali Luis Antonio Tagle Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji  alisema wakati wa Mkutano wa 12 kuhusu - Uinjilishaji Mpya (PCNE XII) nchini  Ufilippino, mnamo tarehe 24  Julai 2026 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Tomas huko Manila. Akizungumza katika mazungumzo ya "Moyo kwa Moyo: Urafiki na Usindikizaji na aliwahimiza Wakatoliki kukuza urafiki unaojulikana kwa ukweli, upendo, na usindikizaji mwaminifu. Mazungumzo hayo yaliwakutanisha viongozi wa kidini na walei Wakatoliki, wakiwemo Sr. Mary Joanine Bolisay, SPC, Padre Dean Jerome Cruz, Ndugu Artemio Manuben, OFS, Anne na Billie Dumaliang, na Joy Cancio, ambao walishiriki uzoefu binafsi wa urafiki na usindikizaji katika miito yao.

Mkutano wa Uinjilishaji huko Manila
Mkutano wa Uinjilishaji huko Manila

"Rafiki wa kweli ana ujasiri wa kukuambia mambo ambayo hutaki kusikia"

Katika mazungumzo, Kardinali Tagle alisisitiza kwamba urafiki wa kweli unahitaji uwazi, uvumilivu, na ujasiri wa kusema ukweli kwa upendo. "Usiogope kujenga urafiki. Mbegu za urafiki unazopanda sasa zitakuwa mavuno ya wito katika siku zijazo." Alibainisha kuwa marafiki wa kweli si vyanzo vya faraja tu bali pia ni marafiki walio tayari kutoa mwongozo wa kweli. "Wakati mwingine, rafiki wa kweli ana ujasiri wa kukuambia mambo ambayo hutaki kusikia," alisema.

Kardinali Tagle alisisitiza kwamba, urafiki pia una mwelekeo wa kimisionari. "Hatupaswi kupuuza jukumu la urafiki katika kufanya uso wa Yesu, uso wa Kanisa, kuwa halisi kwa watu," alisema. Pia aliunganisha urafiki na uwakili wa Kikristo, akielezea utunzaji wa uumbaji na kwa kila mmoja kama jibu halisi kwa upendo wa Mungu. "Kujali uumbaji na kwa kila mmoja kama jibu kwa Mungu Muumba wetu, hilo ni tendo la urafiki," alisema. Alihitimisha mazungumzo,  yake akiwakumbusha washiriki kwamba kila urafiki wa kweli wa Kikristo huanza na Kristo. "Kilichotuleta pamoja hapa ni urafiki wetu wa pamoja na Bwana, ambaye alikuwa wa kwanza kutuona kama marafiki zake," alisema.

Mkutano kuhusu uinjilishaji huko Manila
Mkutano kuhusu uinjilishaji huko Manila

Urafiki unasindikizana, haulazimishi kamwe

Majadiliano yalifuata Misa ya ufunguzi wa mkutano, ambapo Askofu Mkuu wa Manila Jose, Kardinali Advincula alitafakari mada ya mwaka huu 2026, "Sangkay"—neno la Kifilipino likiwa na maana urafiki, na kuwaalika Wakatoliki kukumbatia mtindo wa uinjilishaji unaotokana na kusindikizana kwa subira. Akitazama maisha ya Bikira Maria, Kardinali Advincula alisema urafiki halisi wa Kikristo una sifa ya upole, uvumilivu, na ushirikiano. Badala ya kuwalazimisha imani  wengine, alisema, Wakristo wanaitwa kutembea pembeni mwao kwa upendo. "Maria anatukumbusha kwamba, katika urafiki wa kweli, upendo haulazimishwi kamwe bali usikindikiza tu. "Marafiki wa kweli wanajua jinsi ya kusubiri, kwa sababu kusubiri pia ni upendo." Askofu Mkuu aliwahimiza waamini kusindikizana na wale ambao shauku yao ya imani inaweza kuwa imedhoofika, wakiamini kwamba Mungu anaendelea kufanya kazi kwa uvumilivu katika kila moyo wa mwanadamu. Pia aliwakumbusha washiriki kwamba utume wa Kanisa umejikita katika urafiki na Kristo. "Yesu ametuita tuwe marafiki zake, na si watumwa wake," alisema. "Sisi ni marafiki tunaoshiriki utume wake." Kanisa lililojengwa juu ya urafiki wa kweli, ni lile ambalo hakuna mtu yeyote anayetembea peke yake.

Kugundua upya urafiki katika ulimwengu uliogawanyika

Katika toleo la 12 la Mkutano wa Ufilipino kuhusu Uinjilishaji Mpya uliwaleta pamoja Maaskofu, Mapadre, watawa, na waamini walei ili kutafakari urafiki kama kielelezo muhimu cha ufuasi wa Kikristo na utume. Waandaaji walisema mada ya mwaka huu inajibu awamu ya utekelezaji wa Kisinodi kuhusu Sinodi, ambayo inaitaka Kanisa kuimarisha uhusiano na Mungu, na kila mmoja, na viumbe vyote. Katika ulimwengu unaozidi kutawaliwa na mgawanyiko na utengano, mkutano huo ulilenga kuwasaidia Wakatoliki kugundua upya urafiki kama njia ya kuelekea ushirika, usindikizaji wa uinjilishaji.

Kardinali Tagle Urafiki

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

27 Julai 2026, 14:27