Papa akiwa Montecassino aliombea amani ya maeneo yanayo mwaga damu na migogoro!
Vatican News
Kwa Mtakatifu Benedikto, Baba Mtakatifu aliombea amani duniani. Hii ni ishara ya Papa Leo XIV, ambaye asubuhi ya Jumatatu tarehe 20 Julai 2026, alifanya ziara ya faragha kwa Jumuiya ya watawa wa Kibenediktini na Abasia ya Montecassino. Hapo, akitafakari uzuri wa asili, katika zaidi ya mita mia tano juu ya usawa wa bahari, alisimama kusali kwenye kaburi la Mtakatifu Msimamizi mwenza wa Bara la Ulaya.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kiti Kitakatifu, iliyochapishwa kupitia Chaneli ya Telegram, ilibanisha kwamba, “Papa alimkabidhi mwanzilishi wa Shirika la Wabenediktini, "sala ya amani katika maeneo ya dunia yaliyojaa umwagaji damu na migogoro." Katika kile ambacho ni monasteri kubwa zaidi duniani na ya pili kwa ukubwa nchini Italia baada ya ile ya Mtakatifu Scolastica na Subiaco, Papa Leo XIV kisha alikula chakula cha mchana na Jumuiya hiyo na, baadaye, akarudi nyumbani kwake Castel Gandolfo, ambapo anatumia muda wake wa likizo ya kiangazi.
Hata hivyo leo hii zaidi ya hapo awali, mstari kutoka Zaburi 33 (34): "Tafuteni amani na kuifuata," ulionukuliwa na Mtakatifu Benedikto, ambaye ukumbusho wake wa kiliturujia unaadhimishwa kila ifikapo Julai 11, katika Dibaji ya Kanuni yake, inasikika!
Katika mahali hapo, palipobomolewa kabisa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na ishara ya kuuawa kishahidi kwa vita, shafla ya kutoa “Tuzo ya Pacis Nuntius ya 2026” ilifanyika siku kumi zilizopita kwa Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
