Papa kwa Mattarella:Asante kwa umakini wa maisha ya kikanisa nchini Italia
Vatican News
Shukrani kwa "umakini wa kila mara" ambao "maisha ya kikanisa na kijamii" ya Italia yanasindikizwa na kwa kuwategemea watakatifu wake walinzi, Francis wa Assisi na Catherine wa Siena. Hivi ndivyo Papa Leo XIV alivyozungumza na Rais wa Jamhuri ya Italia, Sergio Mattarella, katika telegramu iliyotumwa tarehe 23 Julai 2026, wakati wa siku yake ya kuzaliwa miaka 85 iliyopita. Salamu hii, maandishi yanaendelea, "inaambatana na baraka ya kitume iliyotolewa kwa familia yake, washirika, na "Italia pendwa" yenyewe."
Ziara ya Papa Leo XIV Ikulu ya Italia
Askofu wa Roma alitembelea Ikulu ya Italia mnamo tarehe 14 Oktoba 2025, akitoa hotuba iliyolenga ushirikiano wa pande nyingi na usaidizi kwa familia barani Ulaya ambapo kiwango cha kuzaliwa kinapungua sana ambapo Papa Leo XIV alibainisha, "kinapungua sana." Baba Mtakatifu pia aliakisi vita vinavyoendelea ulimwenguni kote, akialika kutazama nyuso za wengi "waliozidiwa na ukatili usio na maana wa wale wanaopanga kifo na uharibifu bila huruma" katika vita vingi "vinavyoharibu sayari yetu," na kusikiliza kilio chao.
Rais Mattarella, kwa upande wake, alisisitiza kujitolea kwa Papa Leo XIV kwa "umoja wa utu wa mwanadamu" na mazungumzo. Ahadi hii ilirudiwa mara kwa mara na kusifiwa na Rais katika jumbe zingine zilizotumwa kwa Papa, kama vile ile ya mwaka mmoja baada ya kuanza huduma yake kama Kharifa wa Mtume Petro na wakati wa Pasaka.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
