Papa Leo XIV:Chini ya janga la vita,Kristo ni tumaini.Katika saa ya dhambi,Kristo ni msamaha

Kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana Papa Leo XIV alitoa tafakari yake akihimiza kushiriki maisha ya Kristo hata msalabani,mzigo ni mwepesi kwa sababu Bwana hatuachi katika kile kinachotulemea:Katika utumwa,Kristo ni ukombozi.Na zawadi ya nafsi ni kutokana na upendo wa moyo wa hekima ya Yesu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza tafakari ya Injili kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 5 Julai 2026 akiwa katika Dirisha la Jumba ya Kitume, mjini Vatican. Kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatiu Petro, Papa alisema: “Injili ya Liturujia ya leo, (Mt 11,25-30), inatualika kushirikisha sifa ambazo Yesu anainua kwa Baba,:“ Bwana wa Mbingu na dunia”. Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu anaonesha upendo wake ambao kuwa kuhusisha kila kiumbe katika kushukuru huku.” Ishara ya namna hii rahisi, na furaha inafanana na mtindo wa Mungu ambaye anapenda kujionesha kwa walio wadogo, wakati anabaki amejificha kwa wenye hekima na akili  (Taz 11,25). Hakika, watu hawa wamejaa mawazo yao wenyewe kiasi kwamba wanashindwa kutambua uwepo wa Kristo, Masiha anayewatembelea watu wake. Hekima ya kibinadamu kisha inakuwa kiburi, na mafundisho uharibika na kuwa kiburi.

Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Hekima ya kweli hufuniliwa katika unyenyekevu wa mwili

Badala yake, hekima ya kweli ya Mungu hufunuliwa katika unyenyekevu wa mwili, na mafundisho yake yanaelekezwa kwa wale wanaopambana zaidi: "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo" ( Mt 11 28), asema Bwana. Kwenda kwa Yesu kunamaanisha kurudisha upendo wake na kushiriki maisha yake hadi msalabani, kama Yeye mwenyewe alivyotueleza: "Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate" (Mt 16:24). Zawadi ya nafsi kutokana na upendo ni "nira" ya Yesu (taz. Mt 11:29), yaani, mchanganyiko wa mafundisho yake, moyo wa hekima yake, ukiwaka kwa upendo kwa wote.

Kwa nini mzigo ni mwepesi 

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari hii alisema: "Kaka na dada, inawezakanaje uzito wa msalaba ukawa “mwepesi” na “laini”,(Mt 11, 30)? Ni kwa sababu moja:  Bwana anauchukua akiwa wa kwanza na sisi sote, bila kutuacha peke yetu kwa kile tunachokumbana nacho. Kwa dhati, Mwalimu, Yesu anajifanya kuwa kubeba ubinadamu uliojaruhiwa na ubaya , kwa ajili ya kuutibu. Hekima anayotupati ni tangazo la wokovu, na nira yake hutuinua kutoka kila anguko. Kwa hivyo, katika kumfuata Kristo, safari yetu si kujinyima raha kunakotufanya tujisikie vibaya: ni shule ya uhuru, kwa usahihi inayochukua janga la historia na kuangaza daima maana yake hasa katika wakati wa giza zaidi," Papa alifafanua.

Umati wa waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Umati wa waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Kwa njia ya Msalaba wa Yesu,ubaya unashindwa

Kwa hakika ni katika msalaba wa Yesu ubaya unashindwa tu: ni kwa mateso yake tu katika uchovu wetu wa kifo unapata faraja na kukumbolewa. Katika utumwa, Kristo ni ukombozi. Chini ya janga la vita, Kristo ni tumaini. Katika saa ya dhambi, Kristo ni msamaha. Hii ni hekima ya kweli, yaani, njia tunayotaka kutembea pamoja, tukiwa tumeungana kama wanafunzi katika jina lake. Yesu anatufundisha kama Mwana, kwa kugeuka kaka yetu: kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, Yeye mwenyewe anaomwonesha kwa Kanisa ukweli wa Mungu na wa binadamu, kwa sababu “wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia,”(Mt 21,27). Papa Leo XIV kwa kuhitimisha alisema kwamba “wakati tunamshukuru Bwana kwa imani yake iliyojaa upendo, tumuombe kwa maombezi ya Maria, Malkia wa amani, kwa ajili ya wema wa Kanisa na wa Ulimwengu mzima.

PAPA TAFAKARI JULAI 5

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku.  Just click here.

05 Julai 2026, 12:57