2026.07.21 XII Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu wa Asia(FABC). 2026.07.21 XII Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu wa Asia(FABC). 

Papa Leo XIV kwa Kanisa la Asia:vifungo vya ushirika viimarishwe kuwa wa madaraja

Katika ujumbe wa video kutoka kwa Papa Leo XIV ulioelekezwa kwa Maaskofu wakatika katika Mkutano Mkuu wa XII wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Asia (FABC),huko Jakarta,Indonesia,alinukuu Waraka wa Magnifica Humanitas,akihimiza kuendelea kukuza roho ya Kiekaristi kwa ajili ya umoja wa kikanisa unaotokana na upendo wa zawadi ya Bwana katika Ekaristi.

Na Angella rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliwatumia ujumbe kwa njia ya video tarehe 25 Julai 2026, kwa Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu, Asia(FABC), ulioanz tangu 20-26 Julai 2026 huko Jakarta nchini Indonesia. Baba Mtakatifu katika ujumbe huo alibainisha kuwa, "Mnapokusanyika kujadili masuala muhimu yanayoathiri maisha na mustakabali wa Kanisa Katoliki huko Asia, ninawahakikishia ukaribu wangu wa kiroho na ninaomba kwamba Roho Mtakatifu awatie msukumo na kuongoza muda wenu pamoja." Kwa kuongeza Papa Leo alisema "Mada iliyochaguliwa kwa ajili ya  Mkutano wenu Mkuu inatokana na maneno ya Yesu kwa Nathanaeli: "Utaona mambo makubwa kuliko haya!" (Yh 1:50). Kwa kuwaita Filipo na Nathanaeli wamfuate na kuwa wanafunzi wake, Bwana anajiita mpatanishi pekee kati ya Mungu na wanadamu (taz. Yh 1:51)."

Kukuza roho ya Ekaristi katika makanisa

Kwa njia hiyo, Papa Leo XIV alisema kuwa: "Kama wanafunzi wake leo, hii tunajua kwamba Yesu si chanzo cha ushirika wetu na Mungu tu, bali pia sisi kwa sisi. Hakika, katika Barua yangu ya Magnifica Humanitas iliyochapishwa hivi karibuni, niliandika kwamba 'mshikamano wa Kikristo hupata chanzo chake katika fumbo la Kristo na huzaliwa kutokana na ushirika wetu katika sakramenti, hasa Ekaristi (taz n. 88).' Kwa sababu hiyo, Papa aliongeza "ningependa kuwatia moyo kuendelea kukuza roho ya Ekaristi katika Makanisa yenu mahalia, yaani, roho ya umoja wa kikanisa unaotokana na upendo unaotokana na zawadi ya Bwana katika Ekaristi."

Papa anawaombea zawadi za hekima na nguvu za Bwana 

Kwa hivyo ni  matumaini ya Papa Leo XIV,  "kwamba vifungo vya ushirika ndani na kati ya Makanisa mahalia, vitaimarishwa na kuwa ishara kubwa zaidi ya uwepo wa Mungu katika nchi zenu tofauti, hivyo kuwasaidia kuwa wajenzi wa madaraja pamoja baranoi kote Asia." Papa Leo kwa kuhitimisha alisema " Wapendwa marafiki, nikiwakabidhi nyote na kazi yenu kwa maombezi ya Bikira Maria, Mama wa Kanisa, ninawaombea kwa moyo mkunjufu zawadi za hekima na nguvu za Bwana. Na baraka ya Mwenyezi Mungu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, iwashukie na kubaki nanyi daima.  Amina."

PAPA KWA FABC

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

25 Julai 2026, 10:40