Papa Leo XIV alizindua na kubariki Taasisi ya Borgo Laudato si kunako 2025. Papa Leo XIV alizindua na kubariki Taasisi ya Borgo Laudato si kunako 2025.   (@Vatican Media)

Oktoba,Papa atatoa tuzo ya kwanza ya"Nishani ya Leo XIV"kwa ajili ya uendelevu

Kwa kuandaliwa na Chuo Kikuu cha Villanova,Taasisi ya Kiagostinian mahali alipohitimu Robert Prevost shahada ya hisabati mwaka 1977,heshima hii mpya ya Kimataifa itawatambua watu binafsi na mashirika yanayohamasisha uendelevu,uwajibikaji wa kiikolojia na maendeleo fungamani ya binadamu.Itawasilishwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Villanova kuhusu Uendelevu,utakaofanyika Roma na Castel Gandolfo kuanzia tarehe 12- 15 Oktoba 2026 na kuwasilishwa huko Borgo Laudato Si'.

Vatican News

Chuo Kikuu cha Villanova na Ofisi yake ya Uendelevu kimeanzisha tuzo ya Nishani ya Papa Leo XIV kwa ajili ya  Uendelevu, heshima mpya ya kimataifa ambayo itawatambua watu ambao wamejipambanua katika uongozi wao kwa kuhamasisha uendelevu, uwajibikaji wa kiikolojia, na maendeleo fungamani ya binadamu. Nishani hiyo inawaenzi wahamasishaji ambao kwa kazi yao wameonesha maono kamili ya uendelevu, kuunganisha utunzaji wa mazingira, haki ya kijamii, kujali watu walio katika mazingira magumu, na usimamizi wa wajibikaji wa rasilimali za kiuchumi na asilia." Tofauti na tuzo za kidunia, hii inathamini ikolojia fungamani kama agizo la kimaadili la kuwatunza waliotengwa, na kuziba pengo kati ya sayansi kali na imani ya maadili. Wapokeaji wa Tuzo hii wanaweza kutoka katika uwanja wowote au taaluma yoyote na watachaguliwa kulingana na matokeo yao yaliyooneshwa katika kuhamasisha ulimwengu endelevu na wenye usawa zaidi.

Nishani  itakabidhiwa na Papa huko  Castel Gandolfo mwezi Oktoba

Nishani ya kwanza ya Papa Leo XIV kwa ajili ya Uendelevu itatolewa na Papa Leo XIV huko Castel Gandolfo, wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Chuo Kikuu cha Villanova kuhusu Uendelevu, kwa mada: "Kujibu Kilio cha Dunia na Maskini," ambao utafanyika kuanzia  tarehe 12 hadi 15 Oktoba 2026. Mkutano huo utawakutanisha takriban washiriki 300, wakiwemo wasomi, watafiti, wawakilishi wa Kanisa, taasisi, na viongozi kutoka sekta za umma na za kibinafsi, katika jukwaa la taaluma mbalimbali lililoundwa kuhama kutoka katika mazungumzo hadi hatua halisi na za ushirikiano. Mshindi wa Nishani ya kwanza atatangazwa mnamo Septemba 2026, kabla ya Mkutano na sherehe rasmi ya tuzo katika Ukumbi wa Borgo Laudato Si' huko Castel Gandolfo.

Tuzo ya kuhamasisha usimamizi wa Mazingira na Manufaa ya Wote

"Nishani ya Uendelevu ya Papa Leo XIV inaonesha imani iliyoshikiliwa sana katika Chuo Kikuu cha Villanova: kwamba kutunza nyumba yetu ya pamoja na kujaliana haviwezi kutenganishwa," alisema hayo  Rais wa Chuo Kikuu cha Villanova Padre Peter M. Donohue. "Kwa kuwatambua viongozi ambao kazi yao inahamasisha utunzaji wa mazingira na manufaa ya wote," aliongeza, "tunatumaini kuhamasisha matokeo yenye maana na ya kudumu katika jamii  ulimwenguni kote."

Chuo Kikuu cha Villanova na Robert Prevost

Chuo Kikuu cha Villanova, taasisi ya Wakatoliki ya Agostinian, inashiriki uhusiano maalum na Papa. Papa Leo XIV, wakati huo Robert Prevost, alipata shahada ya kwanza katika hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Villanova mnamo 1977, na baadaye Chuo Kikuu kilimpatia shahada ya udaktari wa heshima katika masomo ya ubinadamu mnamo 2014. Nishani hiyo ilianzishwa kama heshima ya kudumu ya kila baada ya miaka miwili iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Villanova, ikisisitiza kujitolea kwa taasisi hiyo katika kuhamasisha mipango endelevu ya kimataifa na kuhamasisha ikolojia  fungamani. Itawasilishwa kama sehemu ya ratiba rasmi ya Mkutano wa Kimataifa wa Uendelevu wa Villanova.

Kamati ya Uteuzi wa Wateule

Kwa Tuzo ya kwanza ya 2026, wateule walitathminiwa na kamati ya uteuzi iliyojumuisha wanachama wa Baraza la Uongozi wa Uendelevu la Chuo Kikuu, kufuatia mchakato mkali wa tathmini ambapo wagombea walitathminiwa kulingana na vigezo vya uendelevu wa pande nyingi. Kuanzishwa kwa Nishani hiyo kunakuja wakati ambapo ufahamu unaoongezeka wa uhusiano mkubwa kati ya changamoto za mazingira na kijamii. Tuzo hii inaonesha maono ya uendelevu ambayo hayazidi ulinzi wa mazingira  tu lakini, yakikumbatia harakati pana za ustawi wa binadamu, haki ya kijamii, na uwajibikaji wa muda mrefu kwa vizazi vijavyo.

Mkutano wa Kimataifa wa Uendelevu

Mkutano wa Kimataifa wa Uendelevu wa 2026 utafanyika kati ya Chuo cha Baba wa Kanisa,  Agostino jijini  Roma na Borgo Laudato Si' huko Castel Gandolfo. Kuandaa mkutano huo huko Roma kunauweka katikati ya mafundisho ya kijamii ya Kikatoliki na kutumia uhusiano wa kipekee wa kitaasisi wa Villanova na Shirika la Kiagostionian na Vatican, kuunganisha sayansi ya mazingira na uongozi wa maadili duniani. Mkutano huo unaendelea katika mazungumzo na washirika kadhaa wa kitaasisi, ikiwa ni pamoja na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu na kwa usaidizi wa Kituo cha Laudato Si' cha Mafunzo ya Juu. Taasisi ya Vatican  iliyoanzishwa na Papa Francisko ili kuhamasisha uundaji wa ikolojia fungamani, elimu endelevu  na mipango iliyoongozwa na Laudato Si'.

Baggio:Kwa ajili ya ikolojia inayoitikia kilio cha dunia na maskini

Kardinali Fabio Baggio, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Juu cha Laudato Si', alikaribisha mpango huo, akielezea: "Nishani ya Papa Leo XIV ya Uendelevu inawaheshimu watu ambao maisha yao yanashuhudia uhusiano usioweza kutenganishwa kati ya utunzaji wa uumbaji na kukuza utu wa binadafungamani inayoitikia kwa matumaini kilio cha Dunia na kilio cha maskini."

Mkutano ukiwaalika watafiti kuhamasisha mitazamo mipya

Ukiongozwa na mafundisho ya Papa Francisko katika Waraka wake wa Laudato Si' kuhusu Utunzaji wa Mazingira, na Laudate Deum, (Sifa kwa Bwana) na mafundisho ya Papa Leo XIV, hasa wito wa "Dilexi Te," yani "Nilikupenda" wa kuwatunza maskini na waliotengwa, Mkutano wa Kimataifa wa 2026,  kuhusu Uendelevu unaozingatia muunganiko unaoongezeka kati ya uharibifu wa ikolojia na ukosefu wa usawa wa kijamii. Lengo lake ni kushughulikia mgogoro huu kwa kuwaalika watafiti kukuza mitazamo mipya kuhusu uendelevu katika sayansi, falsafa, uuguzi, sheria, uchumi, uhandisi, masomo ya ubinadamu, na zaidi.

MKUTANO WA VILLANUOVA HUKO CASTEL GANDOLFO NA ROMA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

20 Julai 2026, 15:59