2026.07.22 Papa alitembelea Monasteri ya Mtakatifu Benedikto huko Subiaco. 2026.07.22 Papa alitembelea Monasteri ya Mtakatifu Benedikto huko Subiaco.  (@Vatican Media)

Subiaco,Papa Leo XIV atembelea Monasteri za Mtakatifu Benedikto na Mtakatifu Scholastica!

Saa sita mchana Julai 22,akitokea Madhahabu ya Utatu Mtakatifu huko Vallepietra,Papa Leo XIV alipitia Monasteri ya Mtakatifu Benedikto huko Subiaco.Baada ya kutafakari mbele ya picha ya Mtakatifu Francis na kubusu sanamu ya Mtakatifu Benedikto,alisali Sala pamoja na watawa.Hatimaye,alipanda hadi Monasteri ya Mtakatifu Scholastica,ambapo alikula chakula cha mchana na Jumuiya ya Wabenediktini na kutembelea mazingira na Konventi kabla ya kurudi Castel Gandolfo.

Vatican News

Asubuhi ya Jumatano tarehe 22 Julai 2026, Papa Leo XIV aliondoka kwenye Madhabahu ya Utatu Mtakatifu, mojawapo ya sehemu za ibada zinazoheshimiwa zaidi katika Vilima vya Kati vya  Mkoa wa Lazio na yapata saa sita mchana kwa gari walifika kwenye Monasteri ya Mtakatifu Benedikto huko Subiaco,ikiwa ni  kilomita thelathini kutoka hapo.

Papa akisali mbele ya Sanamu ya Mtakatifu Francis wa Assisi
Papa akisali mbele ya Sanamu ya Mtakatifu Francis wa Assisi   (@Vatican Media)

Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican ilitangaza kwenye akaunti yake ya Telegram kwamba, "wakati wa ziara yake kwenye Monasteri hiyo alisimama kimya kimya akitafakari mbele ya sanamu ya karne ya 13 ya Mtakatifu Francis wa Assisi. Na katika Pango Takatifu, alibusu goti la sanamu ya Mtakatifu Benedikto, kama ilivyo desturi, na akasali  Sala ya Bwana pamoja na wale waliokuwepo."

Papa katika Monastero ya Wabenediktini huko Subiaco
Papa katika Monastero ya Wabenediktini huko Subiaco   (@Vatican Media)

Hatimaye, alipanda hadi Monasteri ya Mtakatifu Scolastica, ambapo alisimama kwa chakula cha mchana na jumuiya ya Wabenediktini na kutembelea mazingira ya watawa. Baada ya saa 10:00 jioni, Papa Leo XIV na wenzake waliondoka kurudi Castel Gandolfo.

Un altro momento della visita di Papa Leone XIV ai Monasteri benedettini di Subiaco

Wakati wa Kutembelea Monasteri ya Wabenediktini wa Subiaco (@Vatican Media)

Furaha na Shukrani za Jumuiya ya Wabenediktini

"Jumuiya ya Wabenediktini ya Subiaco inakaribisha kwa furaha na shukrani ziara ya Mtakatifu Leo XIV katika Monasteri Takatifu, mahali ambapo Mtakatifu Benedikto alianza safari yake ya kiroho." Hivi ndivyo Abate wa Kawaida wa Subiaco, Dom Mauro Meacci, alivyoliambia Shirika la habari za Kanisa la Italia(SIR.)"Uwepo wa Baba Mtakatifu," aliendelea, "unafufua uhusiano kati ya Kanisa na karama ya Wabenediktini, ukimkumbusha kila mtu umuhimu wa sala, kusikiliza Neno, na kutafuta amani."

Ujumbe wa Papa kwa Jumuiya ya Monasteri ya Mtakatifu Benedikto aliyoacha kwenye kitabu cha wageni
Ujumbe wa Papa kwa Jumuiya ya Monasteri ya Mtakatifu Benedikto aliyoacha kwenye kitabu cha wageni   (@Vatican Media)

Ujumbe ulioachwa na Papa kwa jumuiya ya watawa

Katika kitabu cha wageni cha Monasteri ya Mtakatifu Benedikto, Papa aliandika: "Ombeni na mfanye kazi... Ushuhuda wa watawa wa Benedikto ni halali na muhimu sana katika Kanisa na katika ulimwengu wa leo. Ninaishukuru jumuiya hii kwa mapokezi yao mazuri, na ninawaalika kusali pamoja na Kanisa lote kwa ajili ya amani duniani. Ni ninatoa baraka yangu katika siku kuu ya Mtakatifu Maria Magdalena."

Mazingira ya Ndani ya Konventi ya Watawa
Mazingira ya Ndani ya Konventi ya Watawa   (@Vatican Media)

Na katika kitabu cha wageni cha Monasteri ya Mtakatifu Scholastica, aliandika: "Ninamshukuru Bwana kwa neema ya kuweza kutembelea mahali hapa patakatifu, katika siku kuu ya kiliturujia ya Mtakatifu Magdalena, aliyekuwa wa kwanza kutangaza Ufufuko wa Bwana."

Un momento della visita del Papa nel complesso monastico di San Benedetto a Subiaco

Wakati wa kutembelea Jengo la Monasteri ya Mtakatifu Benedikto huko Subiaco(@Vatican Media)

PAPA SUBIACO

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

22 Julai 2026, 18:30