2026.08.12.Vijana wakishiriki katika Mkutano wa Kitaifa wa Vijana huko Ostrava (© CSM Ostrava 2026) 2026.08.12.Vijana wakishiriki katika Mkutano wa Kitaifa wa Vijana huko Ostrava (© CSM Ostrava 2026) 

Papa Leo XIV kwa Vijana wa Czech:Shuhudia Upendo wa Kristo katika Familia&katika Jamii

Ujumbe wa Papa Leo XIV,uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Parolin,kwa washiriki katika Mkutano wa Kitaifa wa Vijana unaofanyika kuanzia Agosti 11 hadi 16 huko Ostrava, Jamhuri ya Czech:"Mgeukieni Yesu kwa imani,ambaye ameshinda ulimwengu,"anawashauri Papa.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa mwaliko kwa  washiriki katika Mkutano wa Kitaifa wa Vijana, ulioanza, Agosti 11, huko Ostrava, Jamhuri ya Czech, na unaendelea hadi Dominika tarehe 16 Agosti 2026. Katika ujumbe huo Papa anawasihi wawe "Karibu kwa bidii uwepo hai wa Kristo na nuru ya neno lake, ili kuwa mashuhuda wa upendo wake katika familia, katika jamii, na katika mazingira mbalimbali ya maisha, kazi, na masomo." Hawa ni  zaidi ya vijana elfu tatu wa kiume na kike wenye umri wa miaka kuanzia 14 hadi 26 wanashiriki.

I giovani partecipanti all'Incontro Nazionale della gioventù di Ostrava (© CSM Ostrava 2026)

Vijana washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa vijana huko Ostrava (© CSM Ostrava 2026).

Sala na kutia Moyo

Katika ujumbe uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ulioelekezwa kwa Askofu Mkuu Josef Nuzík, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Czech, Papa anatuma "salamu zake za upendo" kwa washiriki wote na "anawatia moyo kumgeukia Bwana Yesu kwa imani, ambaye ameshinda ulimwengu."

Katika maandishi yanasomeka, "Mwokozi, anaendelea kuongoza njia ya wanafunzi wake wote, akiwapatia tumaini, furaha, na amani mioyoni mwao, kwa hivyo, mwaliko kwa vijana ni "kuwa mashuhuda wa upendo wa Mungu katika kila nyanja ya maisha na jamii." Kwa wote, Papa Leo XIV anawahakikishia "ukumbusho wa Baba katika sala" na anatuma baraka zake za kitume, akitamani "tukio hilo liwe na matokeo mazuri, fursa ya kuzaliwa kwa urafiki mpya na wa kweli katika Bwana."

I partecipanti all'Incontro Nazionale della gioventù di Ostrava (© CSM Ostrava 2026)

Washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Vijana wa Ostrava (© CSM Ostrava 2026).

UJUMBE WA PAPA KWA VIJANA HUKO OSTRAVA 2026

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

12 Agosti 2026, 15:21