Kard.Parolin atakuwa Jordan kwa ajili ya kutabaruku Kanisa la Ubatizo wa Yesu!
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, kuwa mjumbe Mwakilishi wake kwa ajili ya maadhimisho ya kutabaruku kwa Kanisa la Ubatizo wa Yesu nchini Jordan. Haya yalitangazwa katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatica iliyotolewa ltarehe 2 Januari 2025. Sherehe hiyo itafanyika tarehe 10 Januari 2025.
Kanisa hilo linalojulikana kama "Bethania ng'ambo ya Jordan" kwa lugha ya wenyeji Al-Maghtas, kihalisi "huzamishwa" -, liko kwenye ukingo wa mashariki mwa Mto Jordan, kilomita tisa kaskazini mwa Bahari ya Chumvi. Maeneo hayo mawili ni tofauti ya kiakiolojia: Tell Al-Kharrar, inayojulikana pia kama Jabal Mar-Elias kulingana na historia ya Nabii Eliya aliyepaa mbinguni, na eneo la makanisa ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji karibu na mto. Hapo inaaminika kwamba ni mahali ambapo Yesu alibatizwa