2025.09.04 Eduard Profittlich 2025.09.04 Eduard Profittlich 

Eduard Profitlich,shahidi wa imani dhidi ya vichaa wa vita

Askofu mkuu Mjesuit,mfiadini wa utawala wa Kisovieti,aliyetangazwa mwenyeheri huko Estonia na Kardinali Schönborn:maisha yake ni mfano wa wakati unaofaa,kuonesha njia ya Mkristo wakati wa mateso."

Vatican News

Ni sawa kwamba mchungaji abaki na kundi lake na kushiriki furaha na huzuni zao ... Nina hakika kabisa kwamba, ikiwa Mungu anatembea pamoja nami, sitakuwa peke yangu kamwe." Ndivyo alivyoandika Mjesuit Eduard Profitlich, Askofu Mkuu wa kwanza wa Estonia, aliyetangazwa kuwa mwenyeheri asubuhi ya tarehe 6 Septemba 2025, huko Tallinn. Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, yaliongozwa na Kardinali Christoph Schönborn, wa Austria akimwakilisha Baba Mtakatifu. Katika mahubiri yake, Kardinali alinukuu maneno ya Mwenyeheri mpya kutoka katika barua kwa familia yake. Alikuwa ameituma kwao wakati mgumu sana mnamo 1940, wakati wanajeshi wa kisoviet walikuwa wameiteka Estonia, na kuzuia shughuli za Kanisa.

Kuwa tayari kutoa maisha

Padre huyo alikuwa na chaguo la kurudi Ujerumani, nchi yake ya kuzaliwa, lakini aliamua kubaki na waamini wake. Uamuzi uliogharimu maisha yake kunako tarehe 27 Juni 1941, alikamatwa na kupelekwa Kirov, Urusi, ambako aliteswa na kuhukumiwa kifo kwa mashtaka ya ujasusi. Unyanyasaji aliopata gerezani ulisababisha kifo chake mnamo tarehe 22 Februari 1942, kabla ya kunyongwa. "Kwa kundi lake, kondoo wake, Padre Profitlich alikuwa tayari kutoa maisha yake," Kardinali Schönborn alisema, akionesha "furaha ya Kristo" ambayo askofu mkuu mwenyeheri alifanya uamuzi wake. Kisha mshereheshaji alikumbuka hali ya kushangaza huko Ulaya katika miaka ya 1940, "kufunguliwa kwa nguvu za kuzimu" kwa sababu ya "labda vita vya kichaa zaidi ambavyo vimewahi kuwepo," pamoja na utawala wa Kinazi  wa Htler huko Ujerumani na utawala wa Kikomunisti katika Muungano wa Kisovieti wa Stalin.

Mateso 

"Kambi za mateso na gulags zilikuwa onesho la dharau kuu kwa ubinadamu," Kardinali aliendelea, akikumbuka "heshima," iliyozaliwa kwa imani, ambayo Profitlich alijisalimisha kwa watesi wake. Kutangazwa mwenyeheri leo kwa Askofu mkuu wa Kijesuit, kulifanyika "wakati ambapo majeraha ya zamani yanatishia kufunguka tena," kwani "vita ni sehemu ya maisha machungu ya kila siku" ya Ulaya Mashariki, kutokana na mzozo unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine. Zaidi ya hayo, Kardinali Schönborn alikumbuka "vita vya tatu vya dunia" ambavyo mara nyingi vilichukizwa na Papa Francisko na kusisitiza kwamba mgogoro huu "pia unajumuisha mateso ya Wakristo duniani kote." Katika hali hii, kwa hiyo, ushuhuda wa wale waliobarikiwa wapya unaonekana "wenye thamani hasa kwa wakati huu," kwani "anaonyesha njia ya Kikristo katika nyakati za mateso."

Ni Mungu pekee anayejua majina yote

Akisisitiza zaidi kwamba "kutangazwa mwenyeheri hakuelekezwi kwa mtu mmoja," Kardrinali huyo alikumbuka sala za waamini wake waliomuunga mkono Profittilch, hadi aliamua kubaki katika nchi ya Baltic licha ya hatari: ndiyo yake haikuwa "ndiyo" ya kibinafsi tu, bali pia "ndiyo" ya "Kanisa kwa mapenzi ya Mungu," kwa sababu "utakatifu wa kibinafsi wa Kanisa, utakatifu ni Kristo."Kisha Schönborn alitaja mipango miwili mahususi: ya kwanza, iliyofanywa mnamo Septemba 4 huko Tallinn na Mapadre wa Dominikani, ilikuwa usomaji  usiokatizwa, kwa muda wa saa 24, wa majina ya waathiriwa wengi wa kambi za magereza za kisovieti. Ya pili ni ya Jubilei Kuu ya 2000, wakati Mtakatifu Yohane Paulo II aliomba kundi la wanahistoria kuanza kuandaa mashahidi wa karne za hivi karibuni. “Ni Mungu pekee anayejua majina yote” ya wafiadini hao, Kardinali huyo alimalizia, akikazia kwamba damu yao “ndiyo mbegu inayotokeza Wakristo.”

06 Septemba 2025, 15:40