2025.09.26  L'intervento di monsignor Paul Richard Gallagher 2025.09.26 L'intervento di monsignor Paul Richard Gallagher  

Gallagher:Teknolojia haipaswi kuchukua nafasi ya hukumu ya binadamu katika masuala ya maisha na kifo

Katika mjadala wa wazi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huko New York(UNGA80),Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa alisisitiza ukweli wa dharura wa hatari zinazozunguka maendeleo ya Akili Unde katika uwanja wa kijeshi.Alisisitiza wito wa Vatican kusitishwa mara moja kwa silaha hatari zinazojiendesha na kusisitiza hatari ya kutumia AI katika mifumo ya amri na udhibiti wa nyuklia.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika, katika hotuba yake kwenye mjadala wa wazi tarehe 24 Septemba 2025 katika Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani,  kama sehemu ya Juma la(UNGA80) kwenye  hafla iliyoandaliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,  lililoakisi juu ya "Akili Unde (AI)na amani na usalama wa kimataifa," alisema kuwa "Tunahitaji mtazamo unaozingatia binadamu kwa maendeleo na matumizi ya teknolojia zinazoibuka, hasa katika uwanja wa kijeshi, kwani haziwezi kuchukua nafasi ya hukumu ya kibinadamu katika masuala ya maisha na kifo kwa sababu yanaweza kuvuka mipaka ambayo haipaswi kuvukwa kamwe."

AI inaweza kuchochea migogoro zaidi ikiwa haitasimamia heshima ya hadhi ya binadamu

Askofu Mkuu Gallagher alisisitiza kwamba "ikiwa maendeleo na matumizi ya  Akili Unde (AI) hayatasimama imara katika kuheshimu utu wa binadamu na kutafuta manufaa ya wote, yana hatari ya kuwa vyombo vya mgawanyiko na uchokozi na kuchochea migogoro zaidi. Hili sio wasiwasi wa kufikirika au wa mbali, lakini  ni ukweli wa dharura, kutokana na ukosefu wa utulivu wa sasa wa kimataifa na ushirikiano wa haraka wa  Akili Unde katika mifumo ya kawaida na ya silaha za nyuklia," alisisitiza. Kama ilivyobainishwa mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni, Katibu wa Vatican  wa Mahusiano na Mataifa alithibitisha tena kwamba "Vatican inaunga mkono kwa nguvu zote kupitishwa kwa usitishaji wa mara moja wa uundaji wa mifumo hatari ya silaha zinazojiendesha (LAWS). Ukuzaji wa teknolojia hizi huzua wasiwasi mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa juu ya viwango vya kisheria, kibinadamu, maadili na usalama, kwa vile ni mifumo isiyo na uwezo wa kibinadamu kwa uamuzi wa maadili na utambuzi wa maadili."

Wito wa Vatican kuunda chombo kinachofunga sheria ya kuhakikisha maisha dhidi ya kifo

Mwakilishi huoy wa Vatican katika Mkutano huo  aliendelea, kusema kuwa Vatican inatoa wito wa kuundwa kwa chombo kinachofunga kisheria ili kuhakikisha kwamba maamuzi kuhusu maisha na kifo yanabaki chini ya udhibiti wa kibinadamu." Askofu Mkuu Gallagher pia aliakisi kama "sawa kuhusu kuibuka kwa kazi mbio mpya ya silaha, iliyoashiriwa na ujumuishaji wa AI  katika mifumo ya kijeshi, ikijumuisha teknolojia ya anga na ulinzi wa makombora.  Kwa Askofu Mkuu, muktadha huu unahatarisha kubadilisha asili ya silaha na vita, na kuunda kiwango cha kutokuwa na uhakika ambacho hakijawahi kutokea. Hasa, matumizi ya AI  katika mifumo ya amri na udhibiti wa nyuklia, inaweza kusababisha hatari mpya zisizojulikana ambazo huenda mbali zaidi ya mantiki dhaifu na ya kimaadili ya kuzuia."

Baraza la Usalama na jukumu Msingi wa kudumisha amani na usalama wa kimataifa

Kiongozi huyo wa Vatican  hatimaye alisisitiza kwamba Baraza la Usalama lina jukumu la msingi la kudumisha amani na usalama wa kimataifa na kwa hivyo lazima lizingatie maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia yanayofanyika katika ulimwengu wa kisasa. Akiwashukuru Korea Kusini kwa kuitisha mjadala kuhusu mada hii kwa wakati ufaao, Askofu mkuu alifafanua kuwa Akili Unde (AI ) tayari ina athari kubwa katika nyanja kama vile elimu, ajira, mawasiliano, huduma za afya na nyinginezo. Teknolojia hii, ina uwezo wa kusaidia kutimiza matarajio yaliyoongoza kuundwa kwa Umoja wa Mataifa miaka themanini iliyopita, kama vile amani, usalama, na dhamana ya uhuru na haki za binadamu, alitoa maoni yake ikiwa itatumiwa vizuri.

26 Septemba 2025, 12:52