"Grace for the World."muziki na ndege zisizo na rubani kuwasha Uwanja wa Mtakatifu Petro
Vatican News
Muziki, taa, matarajio. Sio tu "tukio la kisanii," lakini pia "mpango wa kiutamaduni" wa kweli na wenye uwezo wa kuunganisha mjadala, shuhuda na sanaa: hii ni “Neema kwa Ulimwengu,” kama ilivyopewa kauli mbiu ya kuongoza tukio la kimataifa ambalo Usiku wa tarehe 13 Septemba 2025, liliwasha hisia kali katika mioyo ya watu na kujaza Uwanja wa Mtakatifu Petro na wengine kubaki nje ya Uwanja. Tukio hilo, ambalo katika siku hizi liliwaona watoa mada 15 na warsha mbali mbali kwa ushiriki wa watu mashuhuri wa kimataifa, kwenye Mkutano wa Kimataifa wa "Udugu wa Kibinadamu (12-13 Septemba, Mjini Vatican,) linapata usanisi wake wa kusisimua zaidi katika onesho hilo.
"Kukumbatia kwa ishara" kwa Ulimwengu
Lango la mzunguko wa Bernini lilifunguliwa saa 12:00 jioni, kuruhusu umma kukaa katika viti vyao kwa ajili ya jioni ya sauti na shuhuda zilizoambatana na maonesho ya kisanii ya hali ya juu. Waliochukua zamu zao jukwaani walikuwa ni Andrea Bocelli, Pharrell Williams pamoja na kwaya ya Kiinjili “Voices of Fire”, John Legend, kwaya ya Jimbo Kuu la Roma inayoongozwa na Mwalimu Padre Marco Frisina, waimbaji watatu wa Kiitaliano wa Il Volo, mwimbaji-mtunzi wa nyimbo wa Colombia Karol G, na wasanii wengine wengi waliokuwapo.
Kwa kuimarisha angahewa ilikuwa ni onesho jepesi la Ndege zisizo na rubani zinaratibiwa na “Nova Sky Stories,” pamoja na picha zilizochochewa Kutoka Makumbusho ya Vatican katika Kikanisa cha Sistine. Hili kwa mujibu wa taarifa za Vyombo vya habari , iliema kuwa ni “tukio lililowasilisha mkutano uliohitimisha na kuadhimisha "nguvu ya udugu" na kuzindua katika ulimwengu "kukumbatiana kwa ishara na kujitolea upya kwa pamoja katika ulinzi wa kazi ya Uumbaji."