Kard.Grech:Awamu ya tatu ya mchakato wa Sinodi iwe hatua ya mbele katika Kanisa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, amelialika Kanisa “kufanya kila juhudi kuhakikisha kwamba, awamu ya tatu ya mchakato wa Sinodi inapiga hatua zaidi katika mang’amuzi na uelewa wa sinodi”, Hamasa hii inakuja katika dokezo lililochapishwa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Kipapa Vatican kunako tarehe 15 eptemba 1965 na Mtakatifu Paulo VI.
Katika barua hiyo, Kardinali Grech anasema kwamba Papa Francisko alifafanua sinodi kama “njia ya upendeleo ya kupata ushirika katika Kanisa.” Hisia hizi pia zimeungwa mkono na Papa Leo XIV, ambaye katika Sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 14 Septemba alisisitiza “hali ya kinabii” ya Mtakatifu Paulo VI katika kuunda Sinodi ya Maaskofu mwaka 1965, wakati Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ulikuwa unakaribia mwisho. Papa alisema anatumaini kwamba “maadhimisho ya miaka 60 ya Baraza hili litahamasisha kujitolea upya kwa umoja na utume wa Kanisa." Matumaini hayo yalisisitizwa tena na Kardinali Grech katika dokezo lake, linalokuja wakati wa hatua ya tatu ya mchakato wa sinodi ambayo Papa Francisko aliizindua katika ngazi mahalia mwaka 2021. Kuanzia majimbo na makanisa mahalia, mchakato huu ulijumuisha hatua tatu ambazo zilisababisha vikao viwili vya makusanyiko jijini Vatican mwaka 2023 na 2024. Mikutano hii ilitoa Hati ya Mwisho, ambayo Kardinali Grech anahimiza Makanisa mahalia na mihimili yao ya kikanda kuangalia sasa, ili kujaribu mapendekezo yake.
Mtazamo wa kinabii wa Papa Paulo VI
Kardinali Grech alianza maelezo yake kwa kuangalia mizizi ya Sinodi, kuanzia Papa Paulo VI alipoanzisha Sinodi ya Maaskofu kwa njia ya Barua yake binafsi ya Kitume ya motu “Sollicitudo.” Kardinali Grch anaandika kuwa alianzisha chombo hiki, ili kujibu maombi ya Mababa wa Baraza ili kuhusisha Baraz ala Maaskofu katika haki ya kiti cha Petro ya kuomba kwa Kanisa zima." Kardinali alieleza kwamba Papa Paulo VI alilijalia Kanisa “taasisi kuu inayowakilisha uaskofu wote, yenye uwezo wa kukuza umoja na ushirikiano kati ya maaskofu wa dunia nzima na Askofu wa Roma” na “kumsaidia kwa ushauri” katika masuala na maswali yenye umuhimu mkubwa kwa Watu wa Mungu.
Upyaishaji wa maisha ya kikanisa
Tangu wakati huo, Mikutano Mikuu 16 ya Kawaida, Mikutano Mikuu 3 ya Kawaidia na Mikutano Maalum 11 imefanywa. Kardinali Grech alieleza kwamba Mapapa wote tangu Baraza hilo kuanzishwa wamekubali mapendekezo au hati za mwisho zilizotungwa na makusanyiko mbalimbali na kuzitumia kutoa Nyaraka za kitume za baada ya sinodi zilizoandikwa kwa ajili ya Kanisa, hati ambazo “zimechangia sana kufanya upya maisha ya kikanisa.”
Mabadiliko ya Papa Francisko
Hata hivyo, katika miaka hii 60, Sinodi ya Maaskofu pia imepitia “mageuzi makubwa,” alisema Kardinali Grech. Hii ni shukrani kwa kila mmoja wa Papa,na hasa Papa Francisko, ambaye "alitaka kubadilisha Sinodi kutoka tukio lililotengwa kwa ajili ya mkutano wa maaskofu hadi mchakato katika hatua, ambapo Kanisa zima linashiriki." Hii ilisababisha awamu ya kwanza ya mashauriano na Watu wa Mungu, kisha hatua mbalimbali za "upambanuzi" zilizofanywa na Mabaraza ya Maaskofu, Mabaraza ya Bara na Mikutano Mikuu ya Kawaida, ambayo ilifanyika Roma mnamo Oktoba 2023 na 2024.
Baba Mtakatifu Francisko alikwisha ashiria mabadiliko haya yajayo kunako mwezi Oktoba 2015, wakati wa hotuba yake kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Sinodi ya Maaskofu katika Ukumbi wa Paulo VI. Hapo, Kardinali aliandika, kuwa alifafanua "masharti ya mabadiliko ya Sinodi kutoka tukio hadi mchakato". Hii inahusisha usikilizaji "wa kukubaliana" ambapo "kila mtu ana kitu cha kujifunza", Grech anaendelea, kutoka kwa watu, Chuo cha Maaskofu, kwa Askofu wa Roma. "Kila mtu akimsikiliza mwingine; na wote wakimsikiliza Roho Mtakatifu", kadinali anasisitiza, akiongeza kwamba maneno ya Papa basi yaliongoza katiba ya kitume Episcopalis Communio, iliyotangazwa miaka saba iliyopita, mnamo Septemba 15, 2018.
Utendaji wa Sinodi
Njia ya upendeleo kwa ushirika katika Kanisa Kardinali Grech alisisitiza kwamba uzoefu wa miaka ya hivi karibuni umeonyesha kwamba “utendaji wa sinodi ndiyo njia ya mapendeleo ya kupata ushirika katika Kanisa.” "Tulijionea uzuri na nguvu ya mchakato huu wakati wa awamu mbili za kwanza za Mkutano Mkuu wa Kawaida wa XVI, ambamo tulisikiliza kile ambacho Roho alikuwa akiliambia Kanisa, tukijifunza kusikilizana," anasisitiza. Imekuwa "safari ya kusisimua," iliyoashiriwa na hatua za "upambanuzi wa kikanisa" na kutiwa muhuri na maendeleo na kura kwenye Hati ya Mwisho, ambayo Papa Francis "aliidhinisha mara moja na kuikabidhi kwa Kanisa kama sehemu ya majisterio ya kawaida." Kwa hiyo, kukumbuka matukio haya yote ni “furaha kuu kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi,” anasisitiza kardinali. Wakati huohuo, ni “mwaliko wa kufanya kila jitihada ili awamu ya tatu ya mchakato wa sinodi iwe na hatua zaidi katika uzoefu na uelewaji wa sinodi.”