2025.09.24  Misa ya Kardinali Parolini wakati wa siku kuu ya Padre Pio. 2025.09.24 Misa ya Kardinali Parolini wakati wa siku kuu ya Padre Pio. 

Kard.Parolin:Padre Pio ni Mtakatifu wa sasa,pamoja naye,tuombe amani

Katibu Mkuu wa Vatican aliadhimisha Misa Septemba 23 katika Kanisa la Mtakatifu Salvatore huko Lauro kwa kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Pio wa Pietrelcina.Tukikumbuka msemo wake,sala ni silaha bora tuliyo nayo,tuombe zaidi amani.Mtakatifu huyu anatufundisha kugundua tena thamani ya kiroho ya msalaba,hasa katika Mwaka huu wa Jubilei ya matumaini ambayo hayakatishi tamaa.

Isabella H. de Carvalho na Angella Rwezaula - Vatican – Vatican.

Padre Pio wa Pietrelcina ni  Mtakatifu wa wakati wetu, mtakatifu wa kisasa,  mtu wa kipekee, mpendwa na watu wa nchi nyingi, ambaye anaacha urithi muhimu wa kiroho kwa ulimwengu wa leo; na tukikumbuka maneno yake, 'sala ndiyo silaha bora zaidi tuliyo nayo,' tunaombe zaidi ya yote kwa ajili ya amani. Hivi ndivyo alianza kumfafanua Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin akimkumbuka Padre mashuhuri Mkapuchini,  wakati wa Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumbukumbu yake ya kiliturujia iliyoadhimishwa tarehe 23  Septemba 2025 katika Kanisa la Roma la Mtakatifu Salvatore huko Lauro. Parokia hiyo, ambayo ina makumbusho yenye masalia ya Padre aliyekuwa na madonda, ilikuwa imejaa waamini.

Licha ya mvua kunyesha, waliohudhuria sherehe hizo walijaza Uwanja wa mbele ambao ulikuwa umewekwa viti na vipaza sauti ili kuruhusu kila mtu kufuatilia ibada hiyo. Wawakilishi wengi wa Idara ya Ulinzi wa Raia wa Italia, ambaye mlinzi wake, pia walikuwepo. "Mtakatifu anayefundisha jinsi wakati wetu unahitaji kugundua tena thamani ya hali ya kiroho ya msalaba ili kufungua mioyo yetu, hasa katika Mwaka huu wa Jubilei unaoadhimishwa na tumaini ambalo halikatishi tamaa," Kardinali Parolin alisisitiza.

Il cardinale Parolin durante la Messa per la festa di Padre Pio

Kardinali Parolin  wakati wa misa katika siku kuu ya Mtakatifu Padre Pio

Mateso na sala

Wakati wa Misa, Katibu  Mkuu wa Vatican aliakisi mambo matatu ya utakatifu wa Padre Pio: mateso, sala, na matukio ya kiroho. Akitoa mfano wa mahubiri ya Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa kutangazwa kwake kuwa Mtakatifu mwaka 2002, Kardinali Parolin alisisitiza umuhimu wa kiroho wa Msalaba alichoishi  Mkapuchini mnyenyekevu na jinsi tunavyoweza kujifunza kutoka kwake thamani ya kuokoa ya mateso. Mtakatifu huyo alikuwa na uhusiano wa karibu kati ya mateso na upendo na akatoa maumivu yake ya kimwili na ya kiroho kwa ajili ya wokovu wa roho. Kwa Kardinali Parolin, aliongeza kuwa "kuhani kutoka San Giovanni Rotondo ni mfano wa sala, akionesha jinsi  ulivyo ufunguo unaofungua moyo kwa Mungu."

Kwa kusisitiza zaidi alisema "pia alikuwa mtu thabiti sana, ambaye alijua jinsi ya kupima wakati na namna ya kuomba, pia akitoa ushauri wa vitendo kama vile kutoendelea wakati roho na akili haziko tayari." Kadhalika " Si kutia chumvi kusema kwamba Padre Pio anachukua nafasi ya umuhimu mkubwa katika mfululizo wa sala kuu za kiroho cha Kikristo," alisisitiza Kardinali Parolin.

Le reliquie di Padre Pio nella Chiesa di San Salvatore in Lauro a Roma

Mahali palipo na aina za masalia mbalimbali ya Padre Pio katika Kanisa la Mtakatifu Salvatore huko Lauro jijini Roma

Mtakatifu anayedhihirisha Utajiri wa Injili

Hatimaye, Katibu Mkuu wa Vatican  aliakisi matukio ya kiroho ya Padre Mkapuchini, kama vile "maono yake, madonda  na eneo lake." Alisema kwamba licha ya "kutomuelewa kwa  wengi, Mtakatifu Pio alikubali kwa utiifu wa unyenyekevu, kwa usadikisho mkubwa kwamba Mungu angeruhusu ukweli ushinde katika wakati wake, na ndivyo ilivyokuwa wakati Kanisa lilipomtangaza kuwa Mtakatifu."  Katika maisha ya watakatifu, utajiri wa Injili unadhihirishwa. Haya ni mapito yenye kung'aa ya Mungu ambayo Yeye Mwenyewe amefuatilia na anaendelea kufuatilia katika historia na hivi ndivyo Padre Pio alivyokuwa, "Kardinali Parolin alihitimisha.

Il cardinale Parolin arriva per la Messa per la festa di Padre Pio

Kardinali Parolin wakati wa kufika kwa ajili ya Misa ya Siku kuu ya Padre Pio.

24 Septemba 2025, 17:00