Kutetea maisha Kutetea maisha 

Kutetea Maisha na Familia Pembeni:Mkutano wa Jubilei na Sinodi jijini Roma

Tukio hili limeandaliwa na Mtandao wa Mawazo ya Kijamii wa Kanisa la Amerika ya Kusini kwa kushirikiana na taasisi kadhaa za Vatican,kufanyika mjini Roma kuanzia tarehe 17 hadi 19 Septemba,katika Taasisi ya Kipapa ya Yohane Paulo II.Tukio hilo litasikiliza sauti na uzoefu kutoka duniani kote na kujenga madaraja ya udugu na matumaini kwa vizazi vipya.Mwishoni,washiriki watapokelewa na Papa Leo XIV.

Vatican News.

Kusikiliza, kutambua, na kuanzisha michakato ya mabadiliko ya kiutamaduni na kimuundo ili kukabiliana na changamoto zinazokabili familia katika pembezoni,hasa Amerika ya Kusini na Carribena, katika mazungumzo na maeneo mengine ya dunia, ndilo lengo la Mkutano wa Jubilei na Sinodi ya Utambuzi wa Matumaini juu ya mustakabali wa Maisha na Familia, miongoni mwa wawakilishi wa vituo vya malezi katika Mafundisho Jamii ya Kanisa katika Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribiean, utakaofanyika mjini Roma kuanzia tarehe 17 hadi 19 Septemba 2025, kwenye Makao Makuu ya Taasisi ya Kipapa ya Paulo II katika Taasisi ya Kipapa ya Yohane Paulo II.

Mkutano huu, ulioitishwa na Mtandao wa Mawazo ya Kijamii wa Kanisa la Amerika Kusini (REDLAPSI), utajumuisha wageni kutoka vituo mbalimbali katika mabara matano. Imeandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Kipapa ya Yohane Paulo II (PITJP II), Chuo cha Kipapa cha Maisha (PAV), na Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini (PCAL) na Baraza la Maaskofu la Amerika ya Kusini (CELAM),  Baraza la Kipapa  Walei, Familia na Maisha, Caritas Amerika ya Kusini na Carribean, na Shirikisho la Kidini la Amerika Kusini (CLAR) pia zinashiriki katika tukio hilo.

Katika hali ya mzozo unaoathiri mambo mbalimbali ya kielimu, kijamii na kiutamaduni, wawakilishi wa vyuo vikuu, vituo vya jumuiya, mashirika ya kijamii na ya kikanisa kutoka mabara mbalimbali wamekusanyika mjini Roma ili kusikiliza sauti na uzoefu wa wale wanaopitia hali hii na kuelewa jinsi wanavyoishi imani yao na jinsi wanavyohisi kuwa Kanisa liko karibu au mbali. Kupitia Mkutano huu wa Jubilei na Sinodi, Kanisa linapenda kufanya upya dhamira yake ya kutetea maisha na familia, kujenga madaraja ya udugu na matumaini kwa vizazi vipya.

Kwa upande wa  waandaaji, wanabainisha kuwa "kilicho hatarini katika hali hii yote ni hadhi ya maisha na familia. Kwa hiyo, hatuwezi kufumba macho na kuacha kuchunguza 'ishara za nyakati' ili kuanzisha michakato mipya ya haki, tukizingatia mienendo ya sinodi inayoendelea hivi sasa katika Kanisa la ulimwengu wote, tukiwa makini hasa na vijana. Mkutano huo utakamilika kwa Mkutano wa faragha na Papa Leo XIV."

17 Septemba 2025, 17:45