2025.09.30: Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa,Septemba 29,aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini New Zeland. 2025.09.30: Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa,Septemba 29,aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini New Zeland.  

Ask.Mkuu Rugambwa alikuwa Mtu wa imani thabiti,upendo wa kichungaji na busara!

Askofu Mkuu Novatus Rugambwa kwa sababu ya upendo alionesha akiwa hai na tumuone mtu aliyepita kutoka mautini na kuingia uzimani na mema mengi ya upendo aliyoyapeleka au kuyawezesha yafike kwa wengi.Ni Mahubiri ya Kardinali Rugambwa wakati wa mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa katika Kanisa Kuu la Bukoba,Tanzania,Septemba 30.Misa ilishirikisha Maaskofu na waamini kutoka ndani na nje ya nchi.

Na Patrick  P. Tibanga-Radio Mbiu – Kagera.

Waamini Wakatoliki wametakiwa kumuenzi kwa mema aliyotenda Askofu Mkuu Novatus Rugambwa kwa kutenda matendo ya kumpendeza Kristo kama alivyofanya katika uhai wake kwa kumshuhudia Kristo pasipo kukata tamaa. Rai hiyo ilitolewa na Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora nchini Tanzania wakati wa  Homilia yake kwenye adhimisho la Misa Takatifu ya Mazishi ya Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, iliyoadhimishwa tarehe 30 Septemba 2025 katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mama Mwenye Huruma, Jimbo la Bukoba, Tanzania. Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, alisema kupitia maisha aliyoyaishi Askofu Mkuu Novatus Rugambwa alikuwa mtumishi ambaye aliwapenda ndugu na kuonesha akiwa hai na waamini wamuone kama aliyepita kutoka kwenye mauti na kuingia katika uzima.

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatusi Rugambwa

Wakati wa Mazishi ya Askofu Mkuu Novatusi Rugambwa

Akidadavua masomo yaliyosomwa,  Kardinali Rugambwa, alisema,  Natufurahi kwani yale anayoyasema Yohane katika Waraka wake wa kwanza tuliyosikia hivi punde kuwa “Sisi tunajua ya kuwa tumepata na tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu.” Ni maneno ambayo yanampamba vizuri sana ndugu yetu huyu, ambaye kwa sababu ya upendo wake mkubwa usiyobagua, aliuonyesha wakati akiwa hai, natumuone kama mtu ambaye alishapita kutoka mautini na kuingia uzimani. Mwadhama alisema,  kuwa kwa mema mengi ya upendo aliyo yapeleka au kuyawezesha yafike kwa wengi. Askofu mkuu Novatus. Hakuwa kama hawa wabaya wanaosemwa kwenye Somo hilo,  yaani wale ambao hawapendi na hivyo wakakaa katika mauti,  wale wanao wachukia ndugu zao na kwa namna hiyo wakawa wauaji. Yeye alikuwa kinyume na hao, hakuwa muuwaji, bali mtu aliye leta maisha, furaha na matumaini kwa watu wengi aliokutana nao.

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatusi Rugambwa

Wakati wa Mazishi ya Askofu Mkuu Novatusi Rugambwa

Kardinali Rugambwa aliendelea kusisitiza kuwa: Wana Jimbo la Bukoba tukianza na Maaskofu, Mapadre, Wawekwa Wakfu na Waamini Walei, mnayafahamu hayo na mnaifahamu furaha na matumaini aliyo waletea watu mbali mbali ndugu  yetu huyu Askofu Novatus  kwa mema mengi aliyo watendea, watu binafsi na jumuiya mbali mbali zilizomo hapa Jimboni, ambazo  zimebaki na alama nyingi ambazo kwazo nawaomba tumkumbuke na kumuombea daima ili Mwenyezi Mungu ampokee katika ufalme wake wa mbinguni, kama anavyotaka yeye mwenyewe kwa wote mliyoyafanya mapenzi yake.

Wakati wa Miza ya Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Wakati wa Misa  ya Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Kardinali Prose aidha alisema kwamba: Sitaki kuyataja mengi aliyoyafanya na ninayo yafahamu mimi, yaliyo hapa Jimboni Na hivyo hivyo ninavyo mfahamu kaka yangu huyo Novatus, asingependa  kusikia yanasemwa hayo aliyoyafanya kwani hakuwa na tabia hiyo ya kujitangaza Na najuwa kua aliyafanya hayo alisukumwa na Upendo wa pekee aliyokuwa nao na mengine yametajwa katika utangulizi  juu ya maisha yake. Moja tu, ambalo ninapenda niliseme kuhusu hadhi na hili la upendo wake ni mchango wake mkubwa, aliyoutoa kwa kufanaya Kanisa hili Kuu la kijimbo la Mama Bikira Maria Mwenye Huruma lipendeze na kuwa hivi kama lilivyo.

Misa ya Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Misa ya Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Upendo wake hapa Tanzania, haukubaki katika Jimbo la Bukoba tu, bali umeenea hata kwenye majimbo mengine nchini Tanzania na hata kwenye jamii yetu ya Tanzania kwa ujumla. Kwa hili la mwisho linatosha kuyasoma yaliyokwisha andikwa kuhusiana na moyo wake wa huruma na upendo aliouelekeza kwa watoto maskini na akawezesha kuwapata Masista,  ambao wapo wanafanya utume kwa faida ya vijana wanaotoka katika familia maskini, wakiwezeshwa kitaaluma na kiufundi kwenye masomo yao ya amali kwenye shule zao huko Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Jimbo Kuu la Dodoma. 

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Nilifarijika niliposoma homilia aliyoitoa Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya kumuaga Askofu Mkuu Rugambwa, iliyo adhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, siku ya Alhamis, tarehe 25 Septemba 2025. Pamoja na kuitaja hiyo fadhila ya upendo, tuliyoisisitiza hapo mwanzo, Kardinali Parolin alimweleza Askofu Mkuu Rugambwa kama “mtu aliyekuwa na imani thabiti, upendo wa kichungaji na busara, vilivyo mpatia nguvu na kumsaidia katika utumishi wake wa kidiplomasia, na katika mahusiano baina ya watu wa mataifa, mtu wa uwadilifu, huruma, uvumilivu, unyenyekevu, na mwenye kujitoa sadaka, na kwamba hayo yalimwezesha kufanikiwa katika utumishi wake na huduma alizozitoa."

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Taboara  kadalika alisema: Ndugu zangu, tunalia na kuhuzunika kwani tumepata pengo na tutaukosa mchango wake, tulioufahidi daima, wakati huo huo, tukione kifo chake kama changamoto na furaha kwetu, tumshukuru Mungu aliyetupa zawadi hii ya mtumishi wake, mwenye vipaji na uwezo mkubwa uliyojaa imani na fadhili za Mungu, ni furaha kwetu kwani Askofu Mkuu Rugambwa, alikuwa ni zawadi popte alipo hudumia, na kuonyesha kuwa ni rahisi kuipata  kuileta furaha ya Mungu na utukufu wake na tukaanza kuonja tukiwa bado hapa duniani. Kifo chake pia kinatuachia changamoto, ambayo ni kazi ya kujitahidi kufuata. Nyayo zake na kuwa tayari kuyafanya yale mema aliyoyatenda na yakaonekana wazi mbele za watu.

Wakati wa Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Wakati wa Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Kwa kuhitimisha Kardinali Rugambwa alisema: Mwisho, kifo cha ndugu yetu huyu, aliyerudi kwa muumba wake katika umri wa miaka 67 na siyo 80 wala 90 au 100, kitukumbushe kuwa, maisha yetu hapa duniani hupita haraka, kama rafiki yangu mmoja alivyoniambia siku moja, kwamba “sisi tunatembea na kifo nacho kimo ndani mwetu.”  Tunapaswa kumbe tujiweke tayari daima, kama wale wanawali watano wenye busara tuliyowasikia kwenye sehemu ya Injili tuliyosoma leo, kifo,  yaani Bwana harusi, kinapokuja kitukute tukiwa tumejiandaa na tuwe tayari kuingia naye harusini, huko kwenye furaha ya milele isiyo na mwisho."

Salamu za rambi rambi

Katika salamu za rambirambi, kutoka kwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Angelo Accattino alisema: “Kanisa linamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha ya Marehemu Askofu Mkuu Novatus Rugambwa ambaye alilifahamu Kanisa la Ulimwengu kupitia majukumu yake mbalimbali.”

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa,ndugu jamaa na marafiki wakiwa pamoja

Kwa upande wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Tanzania (TEC),  Mhashamu Wolfugang Pisa, alisema kuwa: Kanisa “linasherekea maisha ya Marehemu Askofu Mkuu Novatus Rugambwa ambaye ni shujaa kwa namna alivyojitoa bila kujibakiza, kuzunguka dunia nzima kupeleka habari njema.”

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa:Maaskofu wakiwa na jeneza kwenda maziko

Naye Mhashamu Jovitus Francis Mwijage, Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba katika salamu zake kwa Waamini alisema “maisha ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa yamekuwa shule ya imani na upendo na kuwa unyenyekevu wake ni fundisho kwa imani ya Kanisa Katoliki.”

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatusi Rugambwa

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatusi Rugambwa

Marehemu Askofu Mkuu Novatus Rugambwa aliyekuwa Balozi wa Vatican akimwakilisha Baba Mtakatifu katika nchi mbalimbali, alifariki dunia kunako tarehe 16 Septemba,2025 akiwa na umri wa miaka 67 na alizikwa katika makaburi ya Kanisa Kuu Bukoba. Sehemu ambayo tayari kuna kaburi la Kardinali Laurean Rugambwa, pamoja na Askofu Nestori Timanywa.

Raha ya milele uwape Ee Bwana na Mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani Amina.

01 Oktoba 2025, 11:08