Jubilei ya Watawa Oktoba 8-12:Ni zaidi ya Mahujaji 16,000 wamefika Roma
Vatican News.
Zaidi ya mahujaji 16,000 wako Roma kuanzia Jumatano tarehe 8 hadi 12 Oktoba 2025, ili kuadhimisha Jubilei ya ya Watawa Ulimwenguni kote ambapo miongoni mwao ni wanaume na wanawake watawa hata wandani pia, washiriki wa taasisi za Shughuli za kitume, washiriki wa Ordo virginum, wahermit na wa mashiriki "aina mpya" za maisha ya wakfu, wote wako tayari mjini Vatican ambao pia wameshiriki Katekesi ya Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.
Takriban nchi mia moja ziliwakilishwa katika hafla hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Maisha ya Wakfu, na Vyama vya Kitume ikijumuisha wajumbe wengi kutoka Italia, Poland, Ufaransa, Hispania, Ujerumani, Ureno, Kroatia, Marekani, Canada, Brazili, Argentina, Mexico, Colombia, El Salvador, Ufilipino, India, Korea Kusini, Indonesia, Nigeria na Congo na kwingineko.
Ratiba: Misa na Papa
Maadhimisho ya Jubilei yameanza, tarehe 8 Oktoba, huku matukio kadhaa yakiwa wazi kwa wote: hija kwenye Milango Mitakatifu kati ya saa 7:00 na 11:00 jioni ikifuatiwa na Mkesha wa Sala saa 1:00 Usiku katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro linaloongozwa na Kardinali Ángel Fernández Artime, SDB, Katibu Mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirikia ya Kitawa na vyama vya Kitume. Siku ya Alhamisi, tarehe 9 Oktoba, Misa itafanyika kwa wote saa 10:30 asubuhi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ikiongozwa na Papa Leo XIV. Kisha kuna Mazungumzo na mpango wa Jiji, jioni ya tarehe 9 Oktoba 2025, katika viwanja mbalimbali jijini Roma: huko Uwanja wa Mashahidi, mkutano juu ya mada: "Ahadi kwa "Wadogo" - Kusikiliza Kilio cha Maskini," katika Uwanja wa Don Bosco,, mkutano "Utunzaji na Ulinzi wa Uumbaji - Ulinzi wa Mazingira”.
Mipango mbalimbali
Kuanzia alasiri ya Alhamisi, tarehe 9 Oktoba, mipango kadhaa itafanywa na Baraza hilo la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na vyama vya Kitume kwa ajili ya mahujaji 4,000 walioidhinishwa kwa matukio haya. Kuanzia 9:00 alasiri hadi saa 11:30 jioni masaa ya Ulaya , mikutano ya kutafakari itafanyika, ikigawanywa na aina ya maisha ya wakfu: Taasisi za kitawa zitakuwa katika Ukumbi wa Paulo VI; taasisi watawa wa ndani zitakuwa katika Chuo Kikuu cha Urbaniana; taasisi za vyama vya kidunia zitakuwa katika Chuo Kikuu cha Santa Croce; wakati waliowekwa wakfu waitwao: ‘Ordo Virginum’ watakuwa katika Ukumbi Mpya wa Sinodi; na "Aina Mpya" za maisha ya wakfu zitakuwa katika Ukumbi Mkuu wa Nyumba Kuu ya Kijesuit na Vyama vya Maisha ya Kitume vitakuwa kwenye Makao Makuu ya Mama wakuu wa Mashirika (UISG.). kwa hiyo kila aina ya Waliowekwa wakfu imegawanyika sehemu yake ya mikutano.
Tukio la Jubilei litaendelea Ijumaa, Oktoba 10, kwanza kwa asubuhi kusikiliza na kutafakari mada ya "Tumaini," kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 6:00 mchana katika ukumbi wa Paulo VI. Hii itajumuisha adhimisho la Ekaristi takatifu, na hotuba ya Padre Giacomo Costa SJ, mshauri wa Sekretarieti kuu ya Sinodi ya Maaskofu, na mkutano na Papa. Kuanzia saa 9:30 alasiri hadi 12:30 jioni washiriki wataweza kushiriki katika "Mazungumzo ya Kiroho," tena yakigawanywa kwa hali zao za maisha, katika maeneo sawa na matukio ya siku ya Alhamisi, 9 Oktoba.
Usiku kuanzia saa 2:00 hadi saa 3:00 kutakuwa na wakati wa sala katika mji wa Roma ikiwa wazi kwa wote, kwa lugha mbalimbali, wakiongozwa na wanaume na wanawake waliowekwa wakfu lakini kwa kugawanyika katika lugha mbali mbali: kwa Kiitaliano katika Kanisa la Mtakatifu Maria wa Njia, kwa Kiingereza katika Kanisa Mtakatifu Silvestro, kwa Kifaransa katika Kanisa la Mtakatifu Luigi wa Ufaransa, katika Kireno katika Kanisa la Mtakatifu 'Andrea wa Valle. Kisipangola Mtakatifu Maria Juu ya Minerva.
Jumamosi, Oktoba 11, mkutano utaendelea saa 2:00 asubuhi katika Ukumbi wa Paulo VI wenye mada ya "Amani," kwa washiriki walioidhinishwa. Kufuatia hilo, kutakuwa na hotuba ya Sista Teresa Maya, CCVI, aliyekuwa rais wa Baraza la Mama wakuu Wakuu (LCWR). Kufuatia chakula cha mchana, kilichoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maisha wa Wafu na Shughuli za Kitume warsha kuhusu usuluhishi na mbinu za kudhibiti migogoro itafanyika kuanzia saa 8:30 hadi 11:00 jioni, pia katika Ukumbi wa Paulo VI, wakiongozwa na timu iliyoongozwa na Padre David McCallum SJ, mkurugenzi wa Programu ya Uongozi Makini na mjumbe wa Tume ya Mbinu ya Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu.
Jubilei itahitimishwa kwa muda wa sala katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta, lililofunguliwa kwa wote, kuanzia saa 1:00 hadi 3:00 usiku, ikijumuisha kuvuka Mlango Mtakatifu. Dominika tarehe 12 Oktoba 2025, mahujaji wa matumaini watashiriki Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Jubilei ya Tasaufi ya Bikira Maria.
Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kubaki na sasisho, tunakualika kujiandikisha hapa ili kupata habari za kila siku: cliccando qui